Wakuu poleni na majukumu! Eti naombwa kujuzwa ni kwa nini asilimia kubwa ya vijana wa arusha ni watumiaji sana wa MIRUNGI? yaani wengi wao kila unayepishana nae mdomo wake umevimba upande mmoja, je kwa watalamu wa afya hili sio janga kiafya? maana niko na mtu hapa naongea nae naona yeye muda wote ni kutafuna tu na bigjee nyingi je na mikoa mingine hali ipoje? hembu tulijadili hili wakuu,,,