Madaraka ya KULEVYA! Msafara wa mgombea urais magari 60

Madaraka ya KULEVYA! Msafara wa mgombea urais magari 60

Ndio tabia za viongozi wa nchi zetu masikini, nao wana akili za kimaskini sana.
 
Haraka haraka ni zaidi ya billion 20 kununua magari
Mafuta ni kama 13 hivi kwa miezi miwili
Kwahiyo ni kama 35Bil hivyo


Haya ndio matumizi mabaya ya rasilimali za nchi
 
hua najiuliza sana sijui watanzania wana laana gani inawatafuna, mnapata rais wa kuwakingia kifua dhidi ya raslimali za taifa bt bado mnaleta uswaz usio maana.

marekani wana rais chizi mda wote yeye ni kubwatuka mitandaoni bt ukiingia kwenye platfom zake wamarekani wengi wana msuport kweli licha ya madhaifu yake.
Mkuu so na wewe unataka tumsapoti jiwe
 
Tambua kwamba huo msafara una makundi manne:-

1. Rais wa nchi/mgombea urais
2. Vyombo vya ulinzi wa Rais
3. Viongozi waandamizi wa CCM

4. Waandishi wa habari

Pia hizo gari ( Vx V8s) Zina speed kubwa ili kuwezesha kuwahi mikutano.

Halafu CCM mnaichukuliaje? Miaka Zaidi ya 30 madarakani ishindwe kununua magari yake?
Zaidi ya 30 ndiyo miaka mingapi? Au unaficha ukweli, fisiemu ni fisiemu tu
 
Najua Kila kitu ndiyo maana nadhani wewe unahisi kuwa pesa za umma zinatumika isivyo! Ila ujue CCM Ni chamadola na kikongwe Tanzania kina vyanzo vya mapato vingi Sana, siyo Jambo la kushangaza kuona hizo VX V8s zikitumiwa kwa kampeni.

Serikali ya wanyonge au ya mabeberu?
 
Ila angekua trump mngemsifu kua ana ulinzi mkali na msafara mzuri
Serikali ya Marekani haichangii kampeni za chama chochote, kwa uwazi au kwa kificho.
 
Wanatuonyesha na sisi huku mwamanyiri tuyaone hayo maVx kama yalivyokuwa maonyesho ya bombadia pale kiwanjani
 
Haya ni matumizi mabaya kabisa ya kodi zetu kuwahi kutokea, Magufuli must go..
 
Tunasubiri tena mitano ili tubane bajeti kwa kupiga marufuku viongozi na wafanyakazi wa umma kwenda nje
 
Hahahaaa kama sijakosea hili tukio pichani lilikua ni baada ya chadema kumpokea waliyemwita Fisadi papa na kumwomba agombee urais.
Kile kitendo ndio kiliwafanya wapenzi wa Chadema akiwemo Dr slaa kutimka na chama kupoteza dira

Ila jamaa alitisha sana sijui yuko chama gani kwa sasa😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom