Nimekuwa nikiwa kama kijana wa TANU Youth League, sikupenda kabisa utawala wa Nyerere wala sielewi kwanini Wabaguzi wa Ujinga wachache wamedanganywa na kutiwa mkenge kuwa eti hakuna kama yeye. Mwinyi na Mkapa nilikuwepo kwenye utawala wao ingawa sipendelei sana walivyoongoza lakini kuna mabadiliko fulani waliyanfanya ambayo Nyerere yalimshinda kabisa. Mabadiliko ya kweli tuliyaona na tunaendelea kuyaona kwa Kikwete, Kikwete nilikuwa sina uhakika na utawala wake aliposhinda kura nyingi sana kwa mara ya kwanza alipochaguliwa, lakini mara tu alipoanza kuongoza, nikajuwa kuwa huyu jamaa ni mchapa kazi na kiongozi mzuri sana, kafanya mabadilko makubwa sana katika Tanzania kuanzia kisiasa mpaka kibiashara, kielimu, kiafya kimtazamo.
Leo hii Watanzania tuna Uhuru wa kutoa maoni na kusema kuliko wakati mwingine wowote, hilo pekee ni hatua kubwa sana aliyotupigisha Kikwete.
Mimi ni mwana CCM, lakini katika demokrasia, hiyo hainizuwii kuchaguwa yeyote yule nnayeona anafaa kuiongoza hii nchi, kwa bahati mbaya kabisa na ukweli wa dhati kabisa, sioni kama Slaa au Mbowe kuwa ni viongozi wa kuweza kuongoza nchi, kwanza hakuna hata mmoja kati yao mwenye upeo na muono wa kumfanya awe Rais. Ikiwa atatokea kiongozi wa ukweli ndani ya chadema au chama kingine chochote kile au hata tukifikia kuwa na wagimbea binafsi, ambae naona huyu anafaa kuiongoza nchi au hata jimbo tu, sitosita kumpa kura yangu na kumchaguwa kwa nia njema kabisa, u CCM wangu haunifanyi niwe kipofu na kiziwi na mwenye Ubaguzi wa Ujinga.