Madaktari wapya au kuwalipa waliopo?

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,276
17,983
Juzi hapa tumemsikia Rais Pombe akiamuru kama ilivyo siku hizi, serikali iajiri madaktari wapya 1,000.

Laweza kuwa wazo zuri. Lakini najiuliza kipi bora? Kuwalipa stahiki zao hawa waliopo wanaodai hela za kujikimu, nyongeza za madaraja, hela za likizo, uhamisho nk. au kuajiri wapya wakati waliopo wana matatizo lukuki.

Halafu tutegemee waliopo wawape muongozo wageni. Kupanga ni kuchagua. Miaka mitano hakuna ajira lakini hospital mpya zinajenjwa kila uchao. Madaktari wanatoka wapi?
 
Mpinzire,
Tatizo lipo wazi. Afya sio kipaumbele chake. Ina pigwa lip service tu. Budget billion 560 lakini mwishowe wanatoa billions 90 tu. Akili yake ipo kwenye maujenzi.

Hakuna ajira, hizo hospital mpya nani atafanya kazi?

Maendeleo lazima yawe intergrated. Ukisema hospital, umaanishe majengo, watalaam (madaktari, wafamasia, manesi, watu wa nusu kaputi, watu wa maabara), dawa na vifaa tiba. Mchanganyiko wote huo ndiyo hutengeneza hospital.

Zinaimbwa hospital majengo. We are doomed.
 
Sibonike nimekuambia sera za nchi mara nyingi zinabadilika pale rais mpya anaposhika madaraka, hilo lipo Duniani kote, haipingwi kuwa ujenzi wa miundombinu ndiyo kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi.

Ungekuwa we ndo Rais ungekuongeza mishahara ila ajira zingekuwa finyu bado ungelalamikiwa tu, wapo wanaolalamika hakuna maji, hakuna umeme, hamna barabara unahisi ungeyatatua yote ungepewa miaka 10 yakukalia hicho kiti? Katika familia yako hakuna changamoto? Unahisi kila changamoto zote utazikabili wakati mmoja? Kama Mungu aliumba dunia na vitu vilivyopo kwa siku 6 na kwa kutamka tu! Jiwe ni nani mpaka utake aguse kila sekta kwa wakati mmoja?
 
.
Juzi hapa tumemsikia Rais Pombe akiamuru kama ilivyo siku hizi, serikali iajiri madaktari wapya 1,000.

Laweza kuwa wazo zuri. Lakini najiuliza kipi bora? Kuwalipa stahiki zao hawa waliopo wanaodai hela za kujikimu, nyongeza za madaraja, hela za likizo, uhamisho nk. au kuajiri wapya wakati waliopo wana matatizo lukuki.

Halafu tutegemee waliopo wawape muongozo wageni. Kupanga ni kuchagua. Miaka mitano hakuna ajira lakini hospital mpya zinajenjwa kila uchao. Madaktari wanatoka wapi?
IMG-20200222-WA0103.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANALOGY YA UKUBWA NA UGUMU NDANI YA FAMILIA
**Baba nunua flat screen kama ya jirani.
**Baba nunua king'amuzi cha AZAM
**Baba nunua king'amuzi cha star TV
**Baba malizia kujenga ukuta wa fence
**Baba weka GPS gari yako ikiibiwa ufuatilie
**Baba oa mke mwingine mama mkorofi.
**Baba jenga nyumba ingine ya kupanga tupate hela
**Baba nipeleke boarding school English medium
**Baba nunua ma simtank mawili mengine ya lita 10,000x2 tukinge maji ya mvua kwenye gutters.
**Baba nunua bodaboda mbili zinalipa sana kukodisha.
**Baba nunua kibajaj kinaingiza kwa siku.
**Baba nitafutie shamba kilimo kinalipa ajira hakuna.
**Baba nipeleke driving
**Baba nataka kuoa
**Baba ninunulie computer ya apples
**Baba ninunulie tablet
**Baba ninunulie smart phone.ya Android

N.B Baba wa hivi hata ashuke leo mbinguni atasema mawazo yote ya maana nitayafanyia kazi ila atayafanya kwa awamu.
Kumbukeni mungu pamoja na uwezo na utukufu wake aliumba dunia kwa siku saba kila siku kwa kitu flani na bado siku ya saba akapumzika.
Mkuu wetu eleweni sio malaika ana damu na nyama kama sisi kila jambo na wakati wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi hapa tumemsikia Rais Pombe akiamuru kama ilivyo siku hizi, serikali iajiri madaktari wapya 1,000.

*******

Miaka mitano hakuna ajira lakini hospital mpya zinajenjwa kila uchao. Madaktari wanatoka wapi?

Hoja yako imefia hapo, unakiri ajira kwa madaktari wapya 1000 na hapo hapo unahoji madaktari kwenye hospitali mpya wanatoka wapi.... mpo wangapi kichwani mwako..?
 
Uwezo wa kufikiri ndiyo huo.

Hujaelewa issue nzima. Maana yake tuache kusimika majengo mapya. Tufanye ziilizopo ziwe hospital kweli - majengo, watalaam, vifaa tiba, dawa etc.

Kwenda kuajiri na kujenga majengo mapya wakati waliopo hawapati stahiki zao ni kazi bure.

Tunajua kujenga kuna 10%. Ndiyo shida yao.
 
Juzi hapa tumemsikia Rais Pombe akiamuru kama ilivyo siku hizi, serikali iajiri madaktari wapya 1,000.

Laweza kuwa wazo zuri. Lakini najiuliza kipi bora? Kuwalipa stahiki zao hawa waliopo wanaodai hela za kujikimu, nyongeza za madaraja, hela za likizo, uhamisho nk. au kuajiri wapya wakati waliopo wana matatizo lukuki.

Halafu tutegemee waliopo wawape muongozo wageni. Kupanga ni kuchagua. Miaka mitano hakuna ajira lakini hospital mpya zinajenjwa kila uchao. Madaktari wanatoka wapi?
Meko msanii hakuna ajira za madaktari wala nini,porojo tu za kwenye siasa.
 
Mkuu, wewe kitaaluma ni daktari..?

Bila shaka jibu lako ni HAPANA, na huna taarifa ya kinachoendelea kwenye kada hii.... kwa kukusaidia tu madaktari wamekuwa wakiajiriwa kila mwaka kwa kiwango kikubwa tu.

Pamoja na wimbi la uhaba wa ajira, kwenye afya nafasi zimekuwa zikitoka sana tu na wengi tu wameajiriwa.... nina uhakika na kwa tamko hilo ni neema.
 
Uwezo wa kufikiri ndiyo huo.

Hujaelewa issue nzima. Maana yake tuache kusimika majengo mapya. Tufanye ziilizopo ziwe hospital kweli - majengo, watalaam, vifaa tiba, dawa etc.

Kwenda kuajiri na kujenga majengo mapya wakati waliopo hawapati stahiki zao ni kazi bure.

Tunajua kujenga kuna 10%. Ndiyo shida yao.
We jamaa mawazo yako finyu sana, eti tuache kujenga hospital tuendeleze hizi zilizopo.. kwani umeambiwa vifaa tiba hakuna? Umeambiwa madawa hakuna? Mama yako aliyekuwa kijijini na hospital ipo 12KM na mama yako ambaye hospital ipo 200Mita nani bora kwa afya?

Mkuu Mshukuru ata huyu Rais anatambua mchango wa afya kwa kujenga vituo vingi vya afya vingi sana hasa huko kijijini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi hapa tumemsikia Rais Pombe akiamuru kama ilivyo siku hizi, serikali iajiri madaktari wapya 1,000.

Laweza kuwa wazo zuri. Lakini najiuliza kipi bora? Kuwalipa stahiki zao hawa waliopo wanaodai hela za kujikimu, nyongeza za madaraja, hela za likizo, uhamisho nk. au kuajiri wapya wakati waliopo wana matatizo lukuki.

Halafu tutegemee waliopo wawape muongozo wageni. Kupanga ni kuchagua. Miaka mitano hakuna ajira lakini hospital mpya zinajenjwa kila uchao. Madaktari wanatoka wapi?
Ndio matokeo ya mtu mmoja kujifanya ana busara kuliko binadamu wote
 
Uwezo wa kufikiri ndiyo huo.

Hujaelewa issue nzima. Maana yake tuache kusimika majengo mapya. Tufanye ziilizopo ziwe hospital kweli - majengo, watalaam, vifaa tiba, dawa etc.

Kwenda kuajiri na kujenga majengo mapya wakati waliopo hawapati stahiki zao ni kazi bure.

Tunajua kujenga kuna 10%. Ndiyo shida yao.

Labda kama una agenda nje ya hii hoja yako, suala la maboresho ni pamoja na dawa na vifaa tiba bila kusahau wataalamu.... majengo ya hospitali ni miundombinu muhimu kuanza nayo.

Sasa kama kujengwa majengo mapya katika maeneo ambayo hayakuwepo wewe unateseka au huoni kama ni kitu, maslahi hayajawahi kuridhisha katika sekta zote na hata hivyo kauli ishatolewa na watumishi wameelewa.... tulia vijana waajiriwe kwanza acha ubinafsi wa kulialia maslahi huku wasomi wapo mtaani bila ajira.

Kwa kutumia huo ‘uwezo wako wa kufikiri’, kama maslahi ndio kitu pekee ili kuboresha huduma za afya.... ni miaka ipi maslahi yaliwahi kuwa bora katika historia ya nchi yako..?

Hakuna wakati utafikia kuwa timilifu kwa kila kitu, ila ni hatua kulingana na mahitaji ya nyakati.... hata hao madaktari walishangilia hizo ajira mpya za madaktari wenzao kwa kutambua umuhimu wa nguvu kazi.
 
Hivi ni kwanini tumechukulia hili suala la ajira kwa madaktari kama ni hisani kwao??

Je, Serikali haioni umuhimu wa afya na tiba bora kwa wananchi wake ambao ni walipa kodi??

Ndugu madaktari na serikali, hili suala la ajira mlitumie kama huduma kwa jamii na siyo hisani kwa watanzania. Pengine leo una afya njema lakini haikupi uhakika kesho yako
 
Mkuu, wewe kitaaluma ni daktari..?

Bila shaka jibu lako ni HAPANA, na huna taarifa ya kinachoendelea kwenye kada hii.... kwa kukusaidia tu madaktari wamekuwa wakiajiriwa kila mwaka kwa kiwango kikubwa tu.

Pamoja na wimbi la uhaba wa ajira, kwenye afya nafasi zimekuwa zikitoka sana tu na wengi tu wameajiriwa.... nina uhakika na kwa tamko hilo ni neema.
Tutaona taarifa za kamati za bunge ilo unalosema.
 
Mkuu, wewe kitaaluma ni daktari..?

Bila shaka jibu lako ni HAPANA, na huna taarifa ya kinachoendelea kwenye kada hii.... kwa kukusaidia tu madaktari wamekuwa wakiajiriwa kila mwaka kwa kiwango kikubwa tu.

Pamoja na wimbi la uhaba wa ajira, kwenye afya nafasi zimekuwa zikitoka sana tu na wengi tu wameajiriwa.... nina uhakika na kwa tamko hilo ni neema.
Hao madaktari wanaoajiriwa wapo hospital gani? Ukienda tu muhimbili hospital ya taifa tu foleni ya kusubiri daktari ni hatari....Huku chini ndio balaa tunahudimiwa na CO/nurses wakijifanya madaktari.
 
Back
Top Bottom