Madaktari wamjibu Antony Lusekelo...

Madaktari wengi wa Tanzania wako kimaslahi zaidi wala si huruma kwa mgonjwa; ukiwaacha wachache sana ambao wanahangaika na mgonjwa na kufanya diagnosis vizuri na hata kuwa watafiti na wenye kujiendeleza wengi wao wanafanya mazao tuuuuuuuuuu.. unaweza kwenda kwa daktari akakupa the same diagnosis na dawa hata ugonjwa haujapona wakati umeenda kwake mara nyingi..

Naomba madaktari wawe na tabia nzuri, wajisomee, wafanye uchunguzi wa maradhi vema, riziki yao itakuwa juu kupita maelezo..

Lakini sasa hivi wengi wao ni malaya, walevi na hufanya kazi kwa mazoea tu hakuna uchunguzi wa kina na maelezo ya maana roho mbaya kama huna pesa etc...

Bado sijawa support mdrs

Hapo kwenye umalaya na ulevi si kwa madaktari tu bali hili linamhusu kila mmoja wakiwemo wanasiasa mwananchi wa kawaida na hata baadhi ya vigozi wa dini so in general binadamu wote are concern
 
ukisoma sheria za kazi utajua kwamba mgomo hutokea wakati waajiriwa wanadai maslahi ambayo hayapo kisheria.mgomo ni shinikizo lisilofuata sheria na utaratibu,sasa siwaelewi nyie mnaotaka urembo wa kufuata sheria n.k mnajidanganya tu na kupiga porojo tu.mnaleta theories zisizo na kichwa wala miguu.halafu naona mnajichanganya sana kwa sababu ikija kwenye maslahi mnasema ooh daktari ni sawa na kazi nyingine kama muhasibu,mwalimu,dereva n.k lakini ikija kwenye kugoma eti daktari ni mtu muhimu hafai kugoma,stupid politics!!unafiki huu na wanafiki kama miss jud ndio chanzo cha kukosa uwajibikaji serikalini,kitu kinachotuletea maafa.hivi wewe miss jud ulitoa maoni gani kuhusu maafa ya gongo la mboto,mbagala,meli ya zanzibar,watu kupigwa risasi arusha,mbeya,mara?unaongelea nn kuhusu mama mjamzito kufariki kisa amekosa oxygen baada ya umeme kukatika na generator kukosa mafuta huku ?tuache unafiki!madaktari wamevumilia wakitegemea serikali au mwananchi atafanya kitu lakini wapi sasa wakati umefika na watu wameamka.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Na nyie madaktari mmefanya makosa hamna cha kusema mpo deep kwenye bible wala nini maana bible hiyo hiyo imeandikwa " mtii mamlaka (serikali) kwa maana mamlaka(serikali ) zote zinatoka kwa MUNGU"
 
Na nyie madaktari mmefanya makosa hamna cha kusema mpo deep kwenye bible wala nini maana bible hiyo hiyo imeandikwa " mtii mamlaka (serikali) kwa maana mamlaka(serikali ) zote zinatoka kwa MUNGU"
kuna kitendo chochote kinachoonyesha madaktari hawakutii mamlaka?kumbuka kwamba mamlaka ina wajibu wa kuwahudumia na kuheshimu wananchi wake.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kutokana na maneno machafu yalitolewa na mchungaji huyo madaktari wamjibu na kumfundisha anthony lusekelo kuisoma biblia vizuri, kifungu cha maandiko matakatifu kinachompa daktari mamlaka ya juu.
hiki hapa

Kitabu: Biblia takatifu: Yoshua Bin Sira 38:1-15
Baadhi ya mistari inasomeka hivi:
38:1 Umheshimu daktari(tabibu), kwa kadiri ulivyo na haja nae, na kwa heshima iliyo haki yake
38:2 Kwa maana ni kutoka kwake aliye juu, daktari(tabibu) alivyoupata ufundi wake, hata na kwa mfalme atapokea ada (consultation fee)
38:3 Maarifa yake daktari(tabibu) yatamwinua kichwa chake,naye atasimama ni mkuu katika wakuu
38:6 Nae(Mungu) amewapa wanadamu maarifa, ili atukuzwe mwenyewe kwa ajili ya miujiza yake

Pia Kile Kiapo cha udaktari kinasomeka hivi:

"Wakati nikikishika kiapo hiki, na ijaliwe kwangu kuyafurahia maisha na kazi yangu. Jamii (serikali) iniheshimu na kunikumbuka(kunitukuza) , nikiwa hai au nimekufa" Mwisho wa kunukuu

Hivyo tuangalie fani hii imelindwa katika nyanja zote. Asije mtu akatudhulumu kwa namna yoyote ile hasa kwa kutumia kiapo chetu kama wafanyavyo sasa.
cleardot.gif


Wanaokimbilia kiapo wanatafuta 'scapegoat': kwani viongozi wa juu wa serikali hawakula kiapo?
 
Watu wengine banaa!HIZI nadharia hizi zitatupeleka pabaya mwingine anasema kama ungekuwa na m wanao uko nae muhimbili na madaktari wamegoma ungejisikiaje??ni wazi ungejisikia vibaya na kwasababu unachohitaji wewe ni tiba kwa mwanao utaishia kuwalaumu madaktari,mgomo ndio silaha ya mwisho kwa mfanyakazi na sio tanzania tu sasa wewe kama ndio ungekuwa daktari tuambie ungegoma au usingegoma???nani chanzo cha mgomo??MADAI ya madaktari ni halali au sio halali???kuna mwaka waongoza ndege waligoma serikali fasta ikaleta wanajeshi wakaziba pengo, safari hii ikadhani ni rahisi ikaleta wanajeshi ikidhani itafanikiwa waaapi???hawakufua dafu na hilo ni somo kwa serikali isidhani fani zote ni sawa hapa madaktari wamewini mno.Hili ndilo tatizo la kuwa na watu wanaoangalia upande mmoja wa shilingi,hapa ni serikali NDIO CHANZO CHA MATATIZO YOTE HAYA asieelewa siku madaktari wamegoma tena kama ni rahisi vaa joho jeupe na kile kifaa cha kupimia mapigo ya moyo kifuani kazibe pengo la wagomaji ******* mnapenda kupindukia.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Dini= $

ye anapata sadaka za kutosha, embu awaache madokta nao wapate haki zao. Mbona wabunge walivyozidishiwa pesa ye hajatoa kifungu cha aya ya bible inayosema kuhusu matabaka? Ya mungu mpeni mungu, ya kaisar mpeni kaisari. Huyu mchungaji gani anayechanga kila kitu bila kujua yupi kaisari yupi mungu?
 
Watu wengine banaa!HIZI nadharia hizi zitatupeleka pabaya mwingine anasema kama ungekuwa na m wanao uko nae muhimbili na madaktari wamegoma ungejisikiaje??ni wazi ungejisikia vibaya na kwasababu unachohitaji wewe ni tiba kwa mwanao utaishia kuwalaumu madaktari,mgomo ndio silaha ya mwisho kwa mfanyakazi na sio tanzania tu sasa wewe kama ndio ungekuwa daktari tuambie ungegoma au usingegoma???nani chanzo cha mgomo??MADAI ya madaktari ni halali au sio halali???kuna mwaka waongoza ndege waligoma serikali fasta ikaleta wanajeshi wakaziba pengo, safari hii ikadhani ni rahisi ikaleta wanajeshi ikidhani itafanikiwa waaapi???hawakufua dafu na hilo ni somo kwa serikali isidhani fani zote ni sawa hapa madaktari wamewini mno.Hili ndilo tatizo la kuwa na watu wanaoangalia upande mmoja wa shilingi,hapa ni serikali NDIO CHANZO CHA MATATIZO YOTE HAYA asieelewa siku madaktari wamegoma tena kama ni rahisi vaa joho jeupe na kile kifaa cha kupimia mapigo ya moyo kifuani kazibe pengo la wagomaji ******* mnapenda kupindukia.

kamata like mkuu. Umeongea hapa. ^
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
mkuu hapo namba mbili natofautiana na wewe kwa kiwango kikubwa sana.labda nikuulize hivi unadhani daktari mwenye njaa,mwenye uchovu wa kusimama kwenye daladala,mwenye mawazo juu ya afya yake,mwenye kufikiria watoto wake watasoma vipi na anayefanya kazi katika mazingira magumu yasio na dawa au vifaa tiba ............ataweza kuzuia maafa?common sense au logic huwa haziapply kwenye mambo ya afya mkuu.

pia naweza kusema madaktari walitimiza wajibu wao kwa kusema hakuna kufanya kazi tukiwa na hali au mazingira mabovu!!!yet watu wamepoteza maisha.

tatizo wabongo tumezoea kushabikia ili tuonekane tunaweza, but hakuja jambo la msingi hapo. kama mtu unaakili timamu na unauwezo mkubwa wa kufikiri, nadhani utakubaliana na ukweli pamoja na kuwa madaktari walikuwa wanadai haki yao lakini hawakustahiri kugoma kabisa, na damu zote za waliokufa kwa ajili ya mgomo zi juu ya mikono yao wala sio serikali.

kwa nini wabongo hatubadiliki tuweke maslay ya taifa mbele kuliko maslai binafsi, ivi wewe leo kama kaka/dada/mama/baba/shangazi/mjomba/au ndugu yako yeyote angekuwa anakata roho mbele yako pale muhimbili ili hali daktari amesimama anamwangalia ungemlilia nani, ungeenda ikulu kwa pinda kumuomba amuokoe au ungemlilia daktari pale muhimbili.

fikiri kabla ya kuandika bana. wengine yanatuuma koz tumeexperience shuruba za mgomo na tumeshuhudia madaktari wakipitapita katika varanda za hospitali ile hali wagonjwa wanateseka kwa maumivu wodini yaani hata kuwapiga sindano za kutuliza maumivu walikataa, kweli ilikuwa inaumiza sana roho kwa sie tuliekuwa pale

achilia mbali mafisadi wachache walioko madarakani wanaoiba fedha lakini lamsing lilikuwa kuokoa maisha ya watanzania.
 
hivi nyie mnakubaliana na kauli mbovu za viongozi kuendelea kutolewa kwa madaktari halafu eti waendelee kufanya kazi? Tatizo wengine mmeg'ania kwamba madaktari walikuwa na dai moja tu ambalo ni ujira.ukweli ni kwamba kulikuwa na madai mengi sana ikiwemo hizo posho,maboresho ya huduma pale mhimbili ili watu wasiendelee kupelekwa India wakati madaktari wenye utalaam uleule tunao,vile kulikuwa na swala la kuingiza vifaa bandia vya kupima ukimwi na malaria ambavyo inawezekana vimeingia kifisadi kupitia kwa mafisa wa ngazi za juu akiwemo katibu mkuu,kwahiyo wakati mwingine hilo swala posho ilikuwa kama chanzo tu cha kudai hayo mengine. Hitisho langu ni kwamba ilikuwa ni lazima wafanye hivyo maana njia nyigine za mezani watawala walizidharau.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Sioni tija ya kumjibu mtu kama yule anaewaumiza masikini kwa kula sadaka zao. Kama yeye ni mtume, nabii ninaamini anaweza kuponya magonjwa kama anavyojitangaza kilichomshinda nini yeye kwenda mahospitali na kuwaombea? Anakaa kulalamika wakati yeye ni nabii? Hapo nimemtoa maana kama nabii anawalaumu madokta wakati nae anaponya kwa miujiza si angefanya miujiza!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Pamoja na uzuri wa quotations hizo zinazowapa utukufu na kweli mnastahiri kuheshimiwa kwa kazi yenu, hakuna kifungu ambacho kinasema unaponyimwa ujira wako ufanye nini. Sidhani utatuonyesha kuwa ukinyimwa ujira UGOME na UUE kwa kutowatibu wagonjwa. Hapo kuna tatizo, kweli mnastahili kulipwa ujira mzuri, kazi yenu ni ngumu na inahitaji umakini mkubwa. Nadhani wapendwa kuanzia sasa mpange kama msipopewa ujira mfanye nini, but at the same time your major concern should be to preserve life. Then you will win muder case siku ya hukumu

Mkuu..life unayoiongelea inaweza kupotea daktari awepo au asiwepo. Madaktari ni wanadam wana maitaji yao kama binadam wengine. Please..usiwafanye madaktari hawana akili mpaka wakaamua kugoma.big up madaktari mmeshika mpini..wakiwazengua gomeni tena
 
kutokana na maneno machafu yalitolewa na mchungaji huyo madaktari wamjibu na kumfundisha anthony lusekelo kuisoma biblia vizuri, kifungu cha maandiko matakatifu kinachompa daktari mamlaka ya juu.
hiki hapa

kitabu: Biblia takatifu: Yoshua bin sira 38:1-15
baadhi ya mistari inasomeka hivi:
38:1 umheshimu daktari(tabibu), kwa kadiri ulivyo na haja nae, na kwa heshima iliyo haki yake
38:2 kwa maana ni kutoka kwake aliye juu, daktari(tabibu) alivyoupata ufundi wake, hata na kwa mfalme atapokea ada (consultation fee)
38:3 maarifa yake daktari(tabibu) yatamwinua kichwa chake,naye atasimama ni mkuu katika wakuu
38:6 nae(mungu) amewapa wanadamu maarifa, ili atukuzwe mwenyewe kwa ajili ya miujiza yake

pia kile kiapo cha udaktari kinasomeka hivi:

"wakati nikikishika kiapo hiki, na ijaliwe kwangu kuyafurahia maisha na kazi yangu. Jamii (serikali) iniheshimu na kunikumbuka(kunitukuza) , nikiwa hai au nimekufa" mwisho wa kunukuu

hivyo tuangalie fani hii imelindwa katika nyanja zote. Asije mtu akatudhulumu kwa namna yoyote ile hasa kwa kutumia kiapo chetu kama wafanyavyo sasa.
cleardot.gif


lovely...............
 
Wananchi tumechangia kuua coz nihatua gan 2liyoichukua kuwaacha wale walioandamana kuishnikza serikal?hivi mnafikir serikali haiui?inaongoza kuua serkal kwa kuptisha dawa feki,kuchakachua elimu,kuptia mauaj ya polisi,rushwa,epa nk.mbona huko hamulaumu?tunaangalia short term effects zinazooneka kirahisi ndo serkal inaamua kujtokeza,je umeshajiulza kwa nin wanafunz wanafeli sna,tatzo ni Walimu walio ktk mgomo baridi lakin hapo serkal inajua mwanafunz asiyefundshwa math. drs la 5 effects zake ztaonekana badae sna,wanaouwawa na walmu ni weng kulko na madaktar leo.ASIKUDANGANYE MTU BILA MASLAHI HAKUNA UZALENDO POPOTE,WAFISADI NCHI ALAFU WEWE UUMIE ETI UZALENDO SHENZ KABSA,sherehe miaka 50 ya uhuru wametumia mabilion kutuonesha vifaru...non sense!haki kwanza ndipo wajibu.Nchi zilzo na wananch wazalendo ni kwasabab serkal inawajal waliowake,mf. Tz ktk vita ya Kagera,nchi ilikuwa maskn lakn uzalendo ulikuwepo sabab serkal ni kwel ilikuwa maskin lakn si kwa kuwa corrupt!kufa kwa watu ni sio hoja(fallacy)tatzo ni nin na kwa nn?tafakar ajal ya meli Zenj,je abiria hawakuona kuwa wamejaa melini?,sumatra je? SERIKALI HII IPO SIKU TU...wengne nafikiri hatuelew vema au wivu tu unatusumbua dhidi ya madr. Nasisi tudai kivyetu yanayotuhusu.

Hii ni kweli amini au kataa!
 
Mbona hatuwalaumu hawa madaktari? Tusiwe fuata upepo, tuangalie nani alikuwa na nafasi nzuri ya kuokoa maafa kati ya serikali na madaktari. Ukitaka kujua kosa la madaktari, tafakari hili:

1. Serikali isitimize wajibu wake na madaktari wasitimize wajibu wao - kuna maafa
2. Serikali isitimize wajibu wake ila madaktari wakatimiza wajibu wao - hakuna maafa
3. Serikali itimize wajibu wake ila madaktari wasitimize wajibu wao - kuna maafa
4. Serikali itimize wajibu wake na madaktari wakatimiza wajibu wao - hakuna maafa

Nilitamani kama kila mtu angekuwa na knowledge ya truth tables za logic circuit humu, ningeyachorea table maelezo yangu. Utaona kwamba maafa yatatokea pale ambapo madaktari hawajatimiza wajibu wao regardless uwajibikaji wa serikali. Kwa hiyo madaktari ndio waliokuwa na uwezo wa kuepusha vifo visivyo vya lazima, na si serikali. Mimi nitaendelea kuwalaumu madaktari

Nahisi we ni moja ya wafuasi wa upepo mana unaongea bila kufikiri hakuna anayeweza kufanya kazi akiwa na njaa na pia madaktari walikuwa pia wanadai mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa ajili ya kuwalinda wagonjwa tatizo unalaumu bila kujua maana ya mgomo wa madokta so nakushauri tafuta chanzo ukishaelewa vizuri ndo uje uandike hapa usikurupuke
 
Kutokana na maneno machafu yalitolewa na mchungaji huyo madaktari wamjibu na kumfundisha anthony lusekelo kuisoma biblia vizuri, kifungu cha maandiko matakatifu kinachompa daktari mamlaka ya juu.
hiki hapa


Mtoa mada tunaomba usipotoshe umma. Kitabu cha Yoshua katika Biblia takatifu kina sura 24 tu. Kwa mujibu wa Biblia Yoshua ni mwana wa Nuni na siyo Sira. Kwa hiyo maneno uliyo nukuu ni uongo.
 
Back
Top Bottom