Madaktari wamjibu Antony Lusekelo...

Madaktari wamjibu Antony Lusekelo...

Mbona hatuwalaumu hawa madaktari? Tusiwe fuata upepo, tuangalie nani alikuwa na nafasi nzuri ya kuokoa maafa kati ya serikali na madaktari. Ukitaka kujua kosa la madaktari, tafakari hili:

1. Serikali isitimize wajibu wake na madaktari wasitimize wajibu wao - kuna maafa
2. Serikali isitimize wajibu wake ila madaktari wakatimiza wajibu wao - hakuna maafa
3. Serikali itimize wajibu wake ila madaktari wasitimize wajibu wao - kuna maafa
4. Serikali itimize wajibu wake na madaktari wakatimiza wajibu wao - hakuna maafa

Nilitamani kama kila mtu angekuwa na knowledge ya truth tables za logic circuit humu, ningeyachorea table maelezo yangu. Utaona kwamba maafa yatatokea pale ambapo madaktari hawajatimiza wajibu wao regardless uwajibikaji wa serikali. Kwa hiyo madaktari ndio waliokuwa na uwezo wa kuepusha vifo visivyo vya lazima, na si serikali. Mimi nitaendelea kuwalaumu madaktari

Logic zako ni Illogical (Ulizozitumia kudraw conclusion). Ni matokeo ya kukariri fallacies. NItachambua kwa mtiririko wa namba ulizoweka:
  1. Ni kweli. Hata hivyo both parties zisipotimiza wajibu ni vigumu kujua nani aliyesababisha maafa (au wote wamesababisha). Kama ni chemistry (au Biological classification) basi tunahitaji further qualitative analysis kupata distinguishing property (feature)... so the hypothesis needs testing
  2. Hii ni fallacy kwa kuwa madaktari unaowaclaim kutimiza wajibu na kuokoa maafa ilhali serikali imewatosa ni madaktari wasio na hisia na wameumbwa kwa chuma. Ni madaktari ambao wanaweza kufanya kazi bila kula, bila kulala wala hawahitaji kulipa nauli za vyombo vya usafiri. Serikali isipotimiza wajibu wake basi MAAFA NI KWA MADAKTARI ambao wana haki kama kundi ama mmoja mmoja na kwamba pakitokea daktari akafa kwa kuwa serikali imepuuzia kuwalinda dhidi ya mazingira hatarishi basi ni uhai umepotea bila kujali kafa mmoja ama mia.
  3. Ni kweli ulichosema as long as at least one of the parties hatimizi wajibu awe daktari au serikali.
  4. Ni kweli as long as both parties wametimiza wajibu wao.
Hii michezo ya kuleta theories za vitabuni ndiyo inafanya Africa wawe wazungumzaji wakati Wachina, wazungu etc wawe watekelezaji. Tuache kukariri madesa.
 
Kitabu cha yoshua bin sira kinapatikana kwenye biblia ya kikatoliki pekee, si rahisi kwa lusekelo kuijua hiyo kwani madhehebu na makanisa yenye mwelekeo wa kiprotestant hutumia biblia ambayo haina vitabu kama, yoshua bin sira, makabayo na vingine vitano. Biblia yakikatoliki ina vitabu saba zaidi kwenye agano la kale.

Vitabu hivi huitwa Deuterocanon (Kumbukumbu la kanuni).
 
Madaktari wengi wa Tanzania wako kimaslahi zaidi wala si huruma kwa mgonjwa; .................

Bado sijawa support mdrs

So cheap. Extremely cheap. Si wewe ambaye kila siku unatetea CCM? unataka kusema hao (most) CCM hawako kimaslahi ndiyo maana unawatetea? Unafiquun.
 
wapendwa,

(na bila kujipa haki ya kutoa hukumu) ....................... WALIOUA WAPENDWA WETU NI MADAKTARI!

Mungu awabariki sana wapendwa

Glory to God!

Acha unafiki. Wengi wenu huwa mnakimbilia kujinasibisha na kauli ya Bwana Yesu kuwa "usihukumu usije ukahukumiwa" ili kujipa moyo kuwa hamfanani na mfarisayo aliyemsimanga mtoza ushuru katika ibada. Kumbe ninyi ni makaburi yaliyopakwa chokaa kwa nje na ndani mkiwa mifupa mitupu, mnawazuia watu kuingia ilhali ninyi hamuingii wenyewe, mnawakusanya watu na kuwafanya wabaya maradufu.

Mnakimbilia "usihukumu usije ukahukumiwa" pale mnapoishiwa hoja ama mnapotaka kuwatetea wazembe wenzenu. Judy katika conclusions zako nilizopata kuziona this is the worst. Unaigiza kuongea busara (ama kujishusha) kumbe unafanya unafiki. Tutawatambua ninyi manabii wa uongo kwa matunda yenu.
 
Wananchi tumechangia kuua coz nihatua gan 2liyoichukua kuwaacha wale walioandamana kuishnikza serikal?hivi mnafikir serikali haiui?inaongoza kuua serkal kwa kuptisha dawa fek..............

Mjomba Andrew wadau unaowalalamikia wanapenda kuja na conclusions nyembamba. Mambo ambayo yako wazi wanayatatua kwa ushirikina, kumsingizia Mwenyezi Mungu au shetani.

Tatizo linaweza kuwa wazi kabisa na solutions zikawa wazi pia, basi viongozi au wananchi wakazembea (au kulinda maslahi yao ama ya vyama vyao) basi visingizio huwa "ni mapepo hayo." Afrika bwana, kaazi kwelikweli!!
 
Sinkala, asante sana. watu waoga kuwaambia madaktari ukweli kama alivyowaambia Lusekelo. Nadhani umesoma maoni yangu hapo juu. Madaktari wameua. ................. Nawasihi siku ingine "tafuteni" mubadala wa kudai haki bila kuuua wagonjwa. Nawasihi sana.

Lete huo unaouita "mubadala." Kitendo cha kuwaambia watu wengine "tafuteni" ni ushahidi kwako wewe mwenyewe kuwa ni mvivu wa kufikiri. Tuambie huo mbadala ni upi.
 
mlitaka madaktari waibembeleze serikali?

Watu wanaongea hisia (feelings) badala ya mantiki. Hawana majibu wanaishia kutisha watu na vifungu vya vitabu vitakatifu. Ndiyo maana Spika Makinda aliwaambia akina Mhe. T. Lissu (nnaowaheshimu) leteni hoja badala ya kutisha wabunge kwa kumtaja Rais.
 
Kinachoturudisha nyuma watu wengi ni kufananisha mifano ambayo haiendani kiutendaji wala utekelezaji. Ninamaana wewe unayewanyima watoto msosi huoni kama unaweza ukaungana na wanao ukawa unawapikia ila wanaact hawajala na linawezekana au hata mkajifanya mnautapiamlo na mnavyeti vya daktari? Sio kila tatizo linatatuliwa kwa kutesa wengine. Sina uhakika na huo usomi wako lazima utakuwa wa kukremisha au kuvuliwa ch*** ndio maana una cheti au ujuzi lakini ktk maisha ya kawaida ni zero.

Kuhusu sheria ya wapi wanapaswa kugoma nafikiri hiyo itabaki kuwa sheria na inahitaji mabadiliko sababu inaonekana iko biased na lazima kuna vifungu vinavyosema wanatakiwa wafanye kazi ktk mazingira timilifu (vifaa, ujira sahihi nk) ndio maana tunaona wanajeshi wakichukua nchi na kumpindua amirijeshi mkuu wao je ukandamizaji usikemewe ili kuepusha athari kubwa zaidi???? Tafakari

kwenye blue: kwa nini hujaona kuwa madaktari nao walipaswa kuungana na wagonjwa? tafakari

kwenye red: sijajua kwa nini umeacha hoja na kukimbilia unecessary personal attacks?? hata hivyo nimekusamehe. tuendelee kujadili. ubarikiwe sana mpendwa

kwenye green: je, unaweza kutuambia ni sekta gani katika nchi yetu serikali imeweza kupeleka vifaa timilifu, ajira sahihi nk? je, hujaona askari akiwa amevaa viatu vilivyotoboka, waalimu je, hujaona wakilala nyumba za nyasi? kwenye ofisi mbalimbali za serikali kama halmashauri zeyu nk, hujaona jinsi watumishi walivyopauka na kuchakaa? unajua hali za mabwana shamba zilivyo?

si afadhali hata huyo dr. anayepata posho ya 10,000/- kwa siku. polisi anapata 100,000 kwa mwezi (sawa na siku 10 tu za daktari) na hata hivyo wanakatwa 50,000 na wanapewa 50,000/ tu! nafikiri sualal hili wote tuliosikia likihojiwa hata bungeni. sasa unashauri nao wagome? je, askari magereza unajua wanafanya kazi katika mazingira gani? wanapata posho ya sh. ngapi kwa siku? wakigoma hao majambazi yakarudi mitaani yataua watu wangapi?? hebu tafakari kwa mapana ndugu yangu.

daktari huanza kazi kama afisa wa daraja la kati na sio la chini. kada nyingine huanza chini kabisa, hii limeishafafanuliwa vizuri. daktari mwenye shahada uya kwanza anaanza na mshahara karibu sawa na mtu mwenye master degree kwenye sekta nyingine. hilo unaliona ni dogo?

hatusemi kuwa wasidai haki zao, ila wajue hali halisi ya nchi yetu na wafuate sheria tulizojiwekea wenyewe kama taifa na ambazo ndio msingi wa ustaarabu wetu (civilization) kama jamii ya watu walio sawa na huru

So cheap. Extremely cheap. Si wewe ambaye kila siku unatetea CCM? unataka kusema hao (most) CCM hawako kimaslahi ndiyo maana unawatetea? Unafiquun.

mpendwa, usimjadili mtoa hoja, bali jadili hoja yake!

pia sioni kwa nini uamini kuwa kama CCM wako kimaslahi zaidi basi hilo linahalalisha madaktari wajichukulie sheria mkononi dhidi ya wagoinjwa wakioapa kuwaangalia afya zao kwa huruma na uaminifu. kumbuka mob justice waliyofanya haikuwa juu ya CCM wala serikali, bali ilikuwa juu ya wagonjwa! wana tofauti gani na 'watu wenye hasira" wanaochoma moto vibaka hadi kufa kwa kuwa tu hao vibaka wakipelekwa polisi huachiwa kwa dhamana na kuonekana tena mitaani??

kama CCM na serikali yake havifai, basi kila inapotokea fursa ya uchaguzi, tutumie haki zetu za kidemokrasia kuleta mabadiliko tunayotaka na sio kuwashukia wagonjwa wasio na hatia yoyote na kuwaua kama madaktari walivyofanya

Acha unafiki. Wengi wenu huwa mnakimbilia kujinasibisha na kauli ya Bwana Yesu kuwa "usihukumu usije ukahukumiwa" ili kujipa moyo kuwa hamfanani na mfarisayo aliyemsimanga mtoza ushuru katika ibada. Kumbe ninyi ni makaburi yaliyopakwa chokaa kwa nje na ndani mkiwa mifupa mitupu, mnawazuia watu kuingia ilhali ninyi hamuingii wenyewe, mnawakusanya watu na kuwafanya wabaya maradufu.

Mnakimbilia "usihukumu usije ukahukumiwa" pale mnapoishiwa hoja ama mnapotaka kuwatetea wazembe wenzenu. Judy katika conclusions zako nilizopata kuziona this is the worst. Unaigiza kuongea busara (ama kujishusha) kumbe unafanya unafiki. Tutawatambua ninyi manabii wa uongo kwa matunda yenu.

ooh my God!!

mbona hujadili hoja yangu, na umeamua kunijadili mimi?

mlitaka madaktari waibembeleze serikali?

binafsi nataka wafuate sheria tulizojiwekea wenyewe kama taifa la watu wastaarabu walio sawa na huru. unapofuata sheria haina maana unaibembeleza serikali. sheria ni msumeno, inaweza hata kuikata na serikali yenyewe bila kuleta maafa kwa wagonjwa wasio na hatia!

sioni vyema karne hii kuishi kwa kufuata kanuni ya survival of the fittest! kumbuka wanyonge ndio waliokufa. wenye pesa zao na nafasi za maana hata malaria wanapelekwa india, na hili madaktari wanalijua vizuri, na wengine huwasindikiza!

Lete huo unaouita "mubadala." Kitendo cha kuwaambia watu wengine "tafuteni" ni ushahidi kwako wewe mwenyewe kuwa ni mvivu wa kufikiri. Tuambie huo mbadala ni upi.

Watu wanaongea hisia (feelings) badala ya mantiki. Hawana majibu wanaishia kutisha watu na vifungu vya vitabu vitakatifu. Ndiyo maana Spika Makinda aliwaambia akina Mhe. T. Lissu (nnaowaheshimu) leteni hoja badala ya kutisha wabunge kwa kumtaja Rais.

mpendwa,

ni kweli ninaweza kuwa nimeandika kwa hisia. lakini pia nimegusia suala la kisheria na nimesema kuwa licha ya sheria ku-categirise huduma za afya kama essentiasl services, madaktari wameipuuza sheria na kujichukulia sheria mikononi mwao wakafanya walivyoona wao kuwa sawa na hatimaye wamewaua watanzania wenzao wasio na hatia kwa sababu zilizo ndani ya wigo wa kushughulikiwa kisheria!

kwa kweli ushabiki si mzuri, kaulize wagonjwa na wafiwa wakwambie kama wanakubali walistahili hayo yaliyowakuta huko mahospitalini wakati wa mgomo!

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Nafikiri wewe hufahamu hili lazima wachache wafe kwa ajili ya wengi hata bwana Yesu alikufa na wengi tuliokolewa. Yaani hilo haliepukiki

Josephine, mwanangu, wengi ni wapi? Madaktari tu!! madaktari ni asilimia ngapi ya watanzania wote. Na mnakufa kwa nini, kwa kudai fedha zaidi!! na si kuwa hamna mshahara, bali nyongeza. Sisis tunaoamini katika kufa kwa Yesu na kufufuka, alifia dunia nzima, si kundi dogo la watu. Hizo hela 25,000 Tsh mlizoongezewa hata mkizila mkumbuke kuna watu wanalia na kukataa kwenu kuwatibu ndugu zao mpaka wakafa.
 
So cheap. Extremely cheap. Si wewe ambaye kila siku unatetea CCM? unataka kusema hao (most) CCM hawako kimaslahi ndiyo maana unawatetea? Unafiquun.

3D unaonekana unatoa hoja kwa kutukana/kuwaona wenzako hawana ubongo etc. Arrogance ya hali ya juu!!!! Nimesoma posting zako, unakuwa na hasira na kutukana. jaribu kurekebisha tabia hiyo. yakatae mawazo ya wenzako bila kutukana- maneno ya cheap, extremely cheap unafiquun (ingawa sijui maana yake) yanaweza yakawa replaced na maneno kama sikubaliani na mtazamo wako, umekosea, etc etc
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Lete huo unaouita "mubadala." Kitendo cha kuwaambia watu wengine "tafuteni" ni ushahidi kwako wewe mwenyewe kuwa ni mvivu wa kufikiri. Tuambie huo mbadala ni upi.

Mbadala mtafuteni nyie, mnaogoma. Sisis tunaona mlivyofanya si vizuri KUUA. Nyie madaktari mna sauti ya kusikika, waulize watanzania watawapa mbadala, kama mmeshindwa kupata mbadala.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
kwenye blue: kwa nini hujaona kuwa madaktari nao walipaswa kuungana na wagonjwa? tafakari

kwenye red: sijajua kwa nini umeacha hoja na kukimbilia unecessary personal attacks?? hata hivyo nimekusamehe. tuendelee kujadili. ubarikiwe sana mpendwa

kwenye green: je, unaweza kutuambia ni sekta gani katika nchi yetu serikali imeweza kupeleka vifaa timilifu, ajira sahihi nk? je, hujaona askari akiwa amevaa viatu vilivyotoboka, waalimu je, hujaona wakilala nyumba za nyasi? kwenye ofisi mbalimbali za serikali kama halmashauri zeyu nk, hujaona jinsi watumishi walivyopauka na kuchakaa? unajua hali za mabwana shamba zilivyo?

si afadhali hata huyo dr. anayepata posho ya 10,000/- kwa siku. polisi anapata 100,000 kwa mwezi (sawa na siku 10 tu za daktari) na hata hivyo wanakatwa 50,000 na wanapewa 50,000/ tu! nafikiri sualal hili wote tuliosikia likihojiwa hata bungeni. sasa unashauri nao wagome? je, askari magereza unajua wanafanya kazi katika mazingira gani? wanapata posho ya sh. ngapi kwa siku? wakigoma hao majambazi yakarudi mitaani yataua watu wangapi?? hebu tafakari kwa mapana ndugu yangu.

daktari huanza kazi kama afisa wa daraja la kati na sio la chini. kada nyingine huanza chini kabisa, hii limeishafafanuliwa vizuri. daktari mwenye shahada uya kwanza anaanza na mshahara karibu sawa na mtu mwenye master degree kwenye sekta nyingine. hilo unaliona ni dogo?

hatusemi kuwa wasidai haki zao, ila wajue hali halisi ya nchi yetu na wafuate sheria tulizojiwekea wenyewe kama taifa na ambazo ndio msingi wa ustaarabu wetu (civilization) kama jamii ya watu walio sawa na huru

mpendwa, usimjadili mtoa hoja, bali jadili hoja yake!

pia sioni kwa nini uamini kuwa kama CCM wako kimaslahi zaidi basi hilo linahalalisha madaktari wajichukulie sheria mkononi dhidi ya wagoinjwa wakioapa kuwaangalia afya zao kwa huruma na uaminifu. kumbuka mob justice waliyofanya haikuwa juu ya CCM wala serikali, bali ilikuwa juu ya wagonjwa! wana tofauti gani na 'watu wenye hasira" wanaochoma moto vibaka hadi kufa kwa kuwa tu hao vibaka wakipelekwa polisi huachiwa kwa dhamana na kuonekana tena mitaani??

kama CCM na serikali yake havifai, basi kila inapotokea fursa ya uchaguzi, tutumie haki zetu za kidemokrasia kuleta mabadiliko tunayotaka na sio kuwashukia wagonjwa wasio na hatia yoyote na kuwaua kama madaktari walivyofanya

ooh my God!!

mbona hujadili hoja yangu, na umeamua kunijadili mimi?

binafsi nataka wafuate sheria tulizojiwekea wenyewe kama taifa la watu wastaarabu walio sawa na huru. unapofuata sheria haina maana unaibembeleza serikali. sheria ni msumeno, inaweza hata kuikata na serikali yenyewe bila kuleta maafa kwa wagonjwa wasio na hatia!

sioni vyema karne hii kuishi kwa kufuata kanuni ya survival of the fittest! kumbuka wanyonge ndio waliokufa. wenye pesa zao na nafasi za maana hata malaria wanapelekwa india, na hili madaktari wanalijua vizuri, na wengine huwasindikiza!

mpendwa,

ni kweli ninaweza kuwa nimeandika kwa hisia. lakini pia nimegusia suala la kisheria na nimesema kuwa licha ya sheria ku-categirise huduma za afya kama essentiasl services, madaktari wameipuuza sheria na kujichukulia sheria mikononi mwao wakafanya walivyoona wao kuwa sawa na hatimaye wamewaua watanzania wenzao wasio na hatia kwa sababu zilizo ndani ya wigo wa kushughulikiwa kisheria!

kwa kweli ushabiki si mzuri, kaulize wagonjwa na wafiwa wakwambie kama wanakubali walistahili hayo yaliyowakuta huko mahospitalini wakati wa mgomo!

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!

Juduth asante sana. 3D anachofanya ni personal attack, ad hominen argument. Nimemwambia humu kuwa ajifunze kujibu wenzake bila kuwatukana. Kila mmoja ana matusi, lakini wastaarabu hatufanyi hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mkuu, Pinda (serikali) alipoongea about a week ago, hakuonyesha kama serikali ipo tayari kuongeza mafao, ndio maana akaongelea impact za nyongeza hiyo kwenye bajeti ya serikali na kusema haiwezekani, madaktari hawakurudi kazini. Tarehe 9 juzi aliongea wazi kuongeza mafao ya madaktari, nao wakakubali kurudi kazini. Kwa hiyo hapo si kauli tu za serikali, ishu ni mafao, so naweza kusema madaktari walizingatia zaidi kusikia nyongeza ya mafao kuliko kauli nyingine hata zingekuwa za upole namna gani. Kwa hiyo kauli mbovu/nzuri za viongozi sio moja ya INPUT katika logic circuit yangu, ila nimeimerge ndani ya WAJIBU WA SERIKALI. So ninabaki na 2 inputs and 2[SUP]2[/SUP] outputs. INPUT zangu ni wajibu wa serikali na wajibu wa madaktari, na output zangu ni either kuwepo maafa au kutokuwepo maafa, kutegemeana na combinations za the two inputs.

Kama serikali ilikuwa na uwezo wakuwaongezea posho kwanini walisubiria mpaka wagonjwa wakafa wengi ndo wakawaongezea?
 
Hivi huyu si ndo ule mchungaji anayehubiri huku akiwa anatunzwa madhabahuni kama mwanamuziki? Anapiga neno kidogo, ananyoosha mkono anapokea fedha,ujumbe unapotea kidogo anazuga anarudi kwenye mstari.

Ukimtunza hela ndogo anakuumbua kidogo, amekuwa ni mtu asiye eleweka kidogo kwani awali amekuwa akiisema serikali ya ccm vibaya na gafla bila kuona zuri la ccm ameanza kuisifia kidogo, sijui kuna kitu gani behind kidogo
 
wapendwa,

hebu tufikiri. mume wangu anaacha hela ya dagaa kila siku nyumbani, mie kama mama nagoma kupika hao dagaa eti nimechoka kulishwa dagaa kila siku tena huku nikijua kabisa kuwa kuwashindisha na kuwalaza njaa watoto wasio na hatia ni MAUTI kwao! nashinikiza ninunuliwe samaki, mume anasema sina hela ya samaki kwa wakati huu, mimi nasema ngoja tuone. baada ya siku kadhaa bila kuwasha moto jikoni wala kupika chochote, watoto wetu wanakufa kwa njaa huku dagaa wakiwa wamejaa tele hapo nyumbani na unga haujapungua! sasa hapo muuaji ni nani?

mimi si mwanasheria, ila kadiri nijuavyo, sheria za kazi haziwaruhusu madaktari, askari, zimamoto, idara za maji na nishati (kama umeme na gesi) nk. kugoma. hizi zote zinaitwa "essential services' kisheria. ikitokea dispute of right (mgogoro wa haki) wanaweza ku-opt mediation/arbitration ila ikitokea dispute of interest (mgogoro wa maslahi), wanapaswa kuitisha compulsory arbitration (mwenye kuelewa zaidi haya mambo ya kisheria naomba anisaidie katika kuweka sawa hapa)

madaktari walikuwa na mgogoro wa maslahi na mwajiri wake (serikali) japo pia walikuwa na madai yanayoonekana kama ni ya haki yakiwa yamechanganywa humo kwenye madai ya maslahi zaidi ili kupata sympathy ya jamii. cha kusikitisha sikusikia chochote kuhusu hatua za kisheria kama zilivyoainishwa kwenye sheria za kazi, badala yake nilisikia tu "tools down"! na hata hayo ya kutaka watu fulani wafukuzwe kazi nayo twaweza kusema ni maslahi/haki za madaktari?? au madai haya niyaweke kundi gani?? nikisema ni ya kisiasa tutakuwa nimekosea?

hapo mtaona kuwa TUGHE na TUCTA walikuwa sahihi kabisa waliposema kuwa mgomo huo si halali KISHERIA kwa sababu haukufuata taratibu za kisheria. ninaamini kama taratibu zingefuatwa kisheria na documemntation yote ikawekwa sawa, basi hata siku tatu za mgomo zisingefika kabla ya maridhiano kufikiwa kati serikali na madaktari. walichofanya ni MOB JUSTICE! ni kujichukulia sheria mkononi! na wameua wapendwa wetu!

kuhusu mashairi yaliyonukuliwa toka kwenye apocryphal souce ya Yoshua bin Sira 38:1-15, haiwapi madaktari utukufu wa aina yoyote zaidi ya watumishi wengine. kila mtumishi anastahili heshima, kuthaminiwa na kuenziwa huduma yake. hakuna mwanya hata kidogo kwenye biblia wa kutukuza baadhi ya fani. wao ni watumishi na wamepewa vipawa hivyo kutoka juu (kwa Baba yetu aliye mbinguni) ambaye ndiye mwenye kutawala katika ufalme wa wanadamu. hivyo wanapaswa kuwa wanyenyekevu siku zote wakitarajia malipo yao kutoka kwa Baba yetu sote aketiye katika kiti halisi cha enzi. hiyo taaluma yao ndiyo talanta yao!

kuhusu Anthony Lusekelo, sikumsikia alisema nini, kwa hiyo sina la kusema juu yake.

kwa kumalizia, (na bila kujipa haki ya kutoa hukumu) naaminini kwamba, serikali ilikosea kama ambavyo inakosea kila siku katika kusimamia sekta mbalimbali (kama si zote). madaktari nao walikosea katika kuwasilisha madai na malalamiko yao kwa mujibu wa sheria, lakini WALIOUA WAPENDWA WETU NI MADAKTARI!

Mungu awabariki sana wapendwa

Glory to God!

Kwahiyo serikali nayo hapo ili play part gani? Ama ndo ilo wazika?
 
Wananchi tumechangia kuua coz nihatua gan 2liyoichukua kuwaacha wale walioandamana kuishnikza serikal?hivi mnafikir serikali haiui?inaongoza kuua serkal kwa kuptisha dawa feki,kuchakachua elimu,kuptia mauaj ya polisi,rushwa,epa nk.mbona huko hamulaumu?tunaangalia short term effects zinazooneka kirahisi ndo serkal inaamua kujtokeza,je umeshajiulza kwa nin wanafunz wanafeli sna,tatzo ni Walimu walio ktk mgomo baridi lakin hapo serkal inajua mwanafunz asiyefundshwa math. drs la 5 effects zake ztaonekana badae sna,wanaouwawa na walmu ni weng kulko na madaktar leo.ASIKUDANGANYE MTU BILA MASLAHI HAKUNA UZALENDO POPOTE,WAFISADI NCHI ALAFU WEWE UUMIE ETI UZALENDO SHENZ KABSA,sherehe miaka 50 ya uhuru wametumia mabilion kutuonesha vifaru...non sense!haki kwanza ndipo wajibu.Nchi zilzo na wananch wazalendo ni kwasabab serkal inawajal waliowake,mf. Tz ktk vita ya Kagera,nchi ilikuwa maskn lakn uzalendo ulikuwepo sabab serkal ni kwel ilikuwa maskin lakn si kwa kuwa corrupt!kufa kwa watu ni sio hoja(fallacy)tatzo ni nin na kwa nn?tafakar ajal ya meli Zenj,je abiria hawakuona kuwa wamejaa melini?,sumatra je? SERIKALI HII IPO SIKU TU...

Nashukuru sana mkuu kwa mifano yako mizuri ambapo kama kuna mtu ambae hatoelewa hapo atokaa aelewe
 
Inawezekana Mzee wa upako asiwe na kifungu kilichonukuliwa katika Biblia yake, kwani nijuavyo mimi YUSHUA BIN SIRA iko katika Biblia ya Kiroma pekee. Hata hivyo cha msingi hapa ni kwamba inawezekana Mzee wa upako ameanza kuwa mwanasiasa. Maana wanasiasa wengi ni wavivu kufanya utafiti matatizo ya aina hii yakijitokeza. Mara nyingi hutegemea maelekezo ya makada na watu walio karibu nao. Ndo maana tulishuhudia Waziri mkuu akijaribu kuwalazimisha Madaktari kurejea kazini la sivyo wajihesabu kazi imekwisha bila kujua msingi wa madai yao! Sisemi Mzee wa upako apuuzwe, lakini nadhani kauli zake zisiginwe!

Je zisingatiwe kwakuwafananisha madaktari na wauwaji wa albino?
 
Back
Top Bottom