Waingereza wanamsemo wao unasema "The end justifies the means."
Wakati wa vita ya pili ya dunia, England hawakuwa na uhakika kama USA yupo upande wao au German. Ili wahakikishe, ilibidi wafuate maneno ya Shakespear yasemayo TO BE OR NOT TO BE (si mtaalamu kwa hilo).
Walichofanya ni kuchukua marubani 7 wa ndege za jeshi za UK na kuwapeleka USA huku ndege zao zikiwa zimepakwa rangi ya jeshi la German. Wakaambiwa kuwa wasiongee chochote watakapoulizwa kwenye radio.
Vijana wakiwa wanajua kuwa ndiyo yalikuwa makubaliano, waliondoka wakiwa na imani wanaenda fanya kazi rahisi sana. USA walipoona ndege za jeshi za German na jamaa hawajibu, wakajua kazi imeanza, wakazishughulikia sawasawa na vijana wote 7 wakafa.
UK ikawa na UHAKIKA sasa kuwa USA wapo upande mmoja nao na ni adui na German.
Kuhusu hii sentesi ya pili, nakukumbusha tu kuwa MKONO MTUPU HAULAMBWI. Kuna watu wamekufa, yes wamekufa au kuteseka sana ila vifo vyao vimeleta mabadiliko sana Tanzania. Kwa mara ya kwanza, imeonekana kuwa Tanzania unaweza kugoma na kushinda ila inatakiwa tu kuwa na UMOJA.
Viongozi wameanza kuweka akili kichwani taratibu na kuacha kuchezea watu wengine kama hawana akili. Uchaguzi ujao, sidhani kama watu watalilia kugombea ubunge kama ilivyokuwa zamani maana wengi sasa wanalia kwani wana madeni hadi yanatisha.
Daktari atimize wajibu wake, ndiyo. Ila inauma sana kama unaona mtu anakufa kwa figo wakati mashine ya kusafisha damu, kuna kifaa kidogo tu kinakosekana na akina Nyoni hawataki kununua maana wao wana mtambo wao Msasani. This is like a JOKE.
Halafu kibaya zaidi, mtu anakuja hapa na kuanza kutulisha maneno kuwa HAKUNA MAAFA.
Museven alisema "barafu/Mvuke ni maji (H20). Ila huwezi kuniambia nikiwa na kiu, ninywe Mvuke au barafu kwa sabau tu ni Maji."
2. Serikali isitimize wajibu wake ila madaktari wakatimiza wajibu wao - hakuna maafa