ukisoma sheria za kazi utajua kwamba mgomo hutokea wakati waajiriwa wanadai maslahi ambayo hayapo kisheria.mgomo ni shinikizo lisilofuata sheria na utaratibu,sasa siwaelewi nyie mnaotaka urembo wa kufuata sheria n.k mnajidanganya tu na kupiga porojo tu.mnaleta theories zisizo na kichwa wala miguu.halafu naona mnajichanganya sana kwa sababu ikija kwenye maslahi mnasema ooh daktari ni sawa na kazi nyingine kama muhasibu,mwalimu,dereva n.k lakini ikija kwenye kugoma eti daktari ni mtu muhimu hafai kugoma,stupid politics!!unafiki huu na wanafiki kama miss jud ndio chanzo cha kukosa uwajibikaji serikalini,kitu kinachotuletea maafa.hivi wewe miss jud ulitoa maoni gani kuhusu maafa ya gongo la mboto,mbagala,meli ya zanzibar,watu kupigwa risasi arusha,mbeya,mara?unaongelea nn kuhusu mama mjamzito kufariki kisa amekosa oxygen baada ya umeme kukatika na generator kukosa mafuta huku ?tuache unafiki!madaktari wamevumilia wakitegemea serikali au mwananchi atafanya kitu lakini wapi sasa wakati umefika na watu wameamka.
mpendwa,
hapo kwenye red: nimeishasema wazi kuwa yoyote anayejua vizuri sheria zinasemaje inapotokea dispute of interest kwenye essential services, atusaidie kutuweka sawa. sasa kama we mwenzetu umesoma vizuri sheria za kazi, hebu tufafanulie zinasemaje kuhusu vitu kinachoitwa hiuzo ESSENTIAL SERVICES, DISPUTES OF RIGHTS, DISPUTES OF INTERESTS na COMPULSORY ARBITRATION
nijuavyo mimi, migogoro ya kikazi inayohusisha madai yasiyo ya kisheria ndiyo ijulikanayo kama dispute of interest na migogoro ya kikazi ihusuyo madai yaliyo ya kisheria hujulikana kama dispute of rights na madai ya aina zote hizo yameainishwa utaratibu wake wa kuyadai kisheria na hata suala la mgomo (strike) limetamkwa na kuanishwa taratibu zake kisheria. kwa hiyo siyo kweli usemapo kuwa
mgomo ni shinikizo lisilofuata sheria na utaratibu!
kwenye blue: naona bado ni personal attacks zinzendelea. ni vizuri kama daktari wangu mwenye madai sahihi, ukajikita katika kujadili mada na sio kunishambulia mimi binafsi.
asante kwa kunielewa na ubarikiwe na Bwana.
Na nyie madaktari mmefanya makosa hamna cha kusema mpo deep kwenye bible wala nini maana bible hiyo hiyo imeandikwa " mtii mamlaka (serikali) kwa maana mamlaka(serikali ) zote zinatoka kwa MUNGU"
nashukuru mpendwa Kimbweka kwa kudokeza hilo.
wengi wanatafuta biblia pale tu wanapotaka ku-justify mambo fulanifulani tu lakini kamwe biblia hawaitumii kama taa ya kuongoza miguu na maisha yao kila siku! utaona hawa madaktari imewabidi hadi kufukua apokriphal account ya YBS ili mradi tu waonekane wako sawa na wajikweze juu ya fani nyingine, kitu ambacho Bwana Mungu hajawahi kukiamuru na wala hakijawahi kuingia kwenye moyo yake!
tatizo wabongo tumezoea kushabikia ili tuonekane tunaweza, but hakuja jambo la msingi hapo. kama mtu unaakili timamu na unauwezo mkubwa wa kufikiri, nadhani utakubaliana na ukweli pamoja na kuwa madaktari walikuwa wanadai haki yao lakini hawakustahiri kugoma kabisa, na damu zote za waliokufa kwa ajili ya mgomo zi juu ya mikono yao wala sio serikali.
kwa nini wabongo hatubadiliki tuweke maslay ya taifa mbele kuliko maslai binafsi, ivi wewe leo kama kaka/dada/mama/baba/shangazi/mjomba/au ndugu yako yeyote angekuwa anakata roho mbele yako pale muhimbili ili hali daktari amesimama anamwangalia ungemlilia nani, ungeenda ikulu kwa pinda kumuomba amuokoe au ungemlilia daktari pale muhimbili.
fikiri kabla ya kuandika bana. wengine yanatuuma koz tumeexperience shuruba za mgomo na tumeshuhudia madaktari wakipitapita katika varanda za hospitali ile hali wagonjwa wanateseka kwa maumivu wodini yaani hata kuwapiga sindano za kutuliza maumivu walikataa, kweli ilikuwa inaumiza sana roho kwa sie tuliekuwa pale
achilia mbali mafisadi wachache walioko madarakani wanaoiba fedha lakini lamsing lilikuwa kuokoa maisha ya watanzania.
mpendwa Gango2,
hapo kwenye red, nakuunga mkono kabisa. walilolifanya madaktari ni kujichukul;ia sheria mikononi na kwa mgomo wao wamesababisha vifo vingi vya watui wasio na hatia wala nafasi ya kuwatimizia madai yao. kwa kweli wamemuonea sana MTANZANIA MNYONGE NA KUUTWAA UHAI WAKE ILI WAPATE MASLAHI BINAFSI! huu ni ukatili wa kutisha sana kuwahi kushuhudiwa katika nchi yetu!
kwenye blue: kama kweli mtu aliyetoka nyumbani kwake kufuata huduma yako hapo hospitali, wewe unayelipwa mshahara utokanao na kodi yake, anakufa mbele ya macho yako, ukiwa na vifaa na madawa husika tena vya serikali na unajua kabisa ungeweza kufanya chochote kusaidia kuokoa maisha yake na usifanye, kwa kweli wewe ndiye muuaji na dhalimu, na hapo UPENDO wako ni sifuri kabisa, huo hauna tofauti na UJAMBAZI WA KUTUMIA TAALUMA!
inauma sana wapendwa. nitaendelea kuwaombea madaktari wote kwa Mungu.
mbarikiwe sana
Glory to God!