OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
WAKATI kukiwa na mgawanyiko mkubwa kwa madaktari nchini katika kushiriki mgomo ulioitishwa na Chama cha Madaktari nchini (MAT), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Said Meck Sadik amepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote katika hospitali za Jiji, yenye lengo la kuchochea watumishi wa afya kugoma.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Sadik alisisitiza kuwa Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kushiriki katika kuwashawishi watumishi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari na wauguzi kugoma.
Sadik anaungana na viongozi wengine wa kitaifa na Mahakama Kuu ya Tanzania, kutoa amri ya kusitishwa kwa mgomo huo wa madaktari ambao ulianza jana katika baadhi ya hospitali huku huduma katika hospitali nyingine zikiendelea vizuri kutokana na madaktari na wauguzi katika hospitali hizo kutogoma.
"Kufuatia tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi."
Ilisema taarifa ya Mahakama Kuu kwa vyombo vya habari. Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa kufuatia maombi namba 73 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania.
Gazeti hili lilipofika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana asubuhi lilishuhudia madaktari wakiendelea na kazi kitendo kilichoonesha kuwa hawakushiriki katika mgomo.
Wakati hayo yakiendelea, Serikali imeendelea kuwataka madaktari wote nchini kuendelea na kazi wakati suala la kupatiwa suluhisho likiwa katika chombo cha kisheria Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.
Pia imesema itakuwa tayari kutekeleza maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi, kuhusu mapendekezo yatakayotolewa juu ya suala zima la maslahi na haki za madaktari kama maombi yao yalivyowasilishwa.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Selaman Rashid, aliyasema hayo mjini Morogoro jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kuona iwapo madaktari wameamua kutekeleza mgomo wao au la.
Akiwa hospitalini hapo, Naibu Waziri huyo alishuhudia madaktari kwa kushirikiana na wauguzi wakiendelea kufanya kazi mbalimbali za kuhudumia wagonjwa licha ya Chama cha Madaktari kutoa tamko la kuwataka wagome nchi nzima kuanzia jana.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa hiyo ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa , Dk. Godfrey Mtey , ulimtembeza Naibu Waziri maeneo mbalimbali ikiwemo wodini, maabara na chumba cha kujifungulia na kuzungumza na baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakipatiwa tiba.
"Nawaomba madaktari wote waendelee na kazi ya kuwahudumia wagonjwa wakati suala lao lipo kwenye chombo cha kisheria ...sote tumekubaliana usuluhishi wa mgogoro huu uamuliwe na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Hata hivyo alisema, Serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha maslahi ya wafanyakazi wote si kwa ajili ya madaktari pekee ili wapate mishahara kulingana na kazi wanazozifanya.
Alisema, Serikali inapozungumzia mishahara haizungumzii kwa daktari pekee bali inazungumzia sekta mbalimbali na si kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pekee bali na wizara nyingine za Serikali.
Aliupongeza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa watumishi wake wakiwemo madaktari kuendelea na kazi za utoaji wa huduma kwa wagonjwa. Kutoka Dodoma taarifa zinasema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dk Ezekiel Mpuya alisema jana kuwa hali ni shwari katika hospitali hiyo na hakuna mgomo.
Akizungumza na gazeti hili, Dkt. Mpuya alisema madaktari na wauguzi walikuwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida na hakukuwa na mgomo wowote.
"Hali ni shwari na wale wote wenye zamu wako kazini isipokuwa daktari mmoja aliyeko kwenye mafunzo leo hajaripoti sijui ana tatizo gani, lakini hapa hakuna mgomo," alisema.
Hata hivyo hali haikuwa shwari jijini Mwanza kwani madaktari zaidi ya 200 waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando walianza mgomo rasmi jana baada ya Serikali kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu madai yao mbalimbali.
Katika mahojiano na gazeti hili Mwakilishi wa Kamati ya kufuatilia madai ya Madaktari hao waliyapeleka serikalini, Dk Richard Kirita alisema kwamba madaktari wa kada zote katika hospitali hiyo wapo kwenye mgomo isipokuwa baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wakuu wa idara.
Mapema wiki hii, Kamati ndogo ya Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyokuwa ikifuatilia mgogoro dhidi yao na Serikali ilisema haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na Serikali juu ya madai yao na kuonesha nia ya kufanya mgomo wa nchi nzima kuanzia jana.
"Ni kweli tumeanza mgomo rasmi, madaktari waliokuwa zamu leo (jana) hawajaenda kazini, hata hivyo kwa kuwa leo si siku ya kazi unaweza kudhani hakuna mgomo, lakini njoo Jumatatu ndio utapata picha halisi ya mgomo kwa sababu wagonjwa watakuwa wengi lakini hakutakuwa na huduma," alisema Dkt. Kirita.
Hata hivyo alisema kwamba wanaendelea na vikao ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wenzao wa Dar es Salaam ili kujua ni hatua zipi zaidi wachukue kuhusiana na mgomo wao huo.
Dkt. Kirita alisema kwamba katika kikao cha madaktari wa Bugando kilichofanyika hivi karibuni kujadili majibu ya Serikali juu ya madai yao na kuhusisha jumla ya madaktari 202 walikubaliana kwa pamoja kuanza mgomo kuanzia jana iwapo madai yao hayatatekelezwa na Serikali.
Katika mgomo wa kwanza wa madaktari uliofanyika mapema mwaka huu madaktari walikuwa na madai mbalimbali yakiwemo ya kuboreshwa kwa huduma za afya zikiwemo dawa, vitanda na vifaa tiba, mishahara na nyumba za madaktari.
Baadhi ya watu waliokuwa wamepeleka wagonjwa katika hospitali hiyo jana walionekana wakiwaondoa baada ya kukosa huduma kutoka kwa madaktari ambao baadhi walikuwa kwenye kikao na wengine walionekana katika vikundi vikundi wakipiga soga.
Kwa upande wao wagonjwa katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Bugando wameiomba Serikali pamoja na madaktari walio kwenye mgomo kumaliza tofauti zao ili madaktari waweze kurejea kazini na kuwapatia huduma.
Wakizungumza jana katika wodi namba 6 na 8, Yohana Matinde, Abel Joseph, Martha Maduhu na Pendo Saimon walisema kuwa tangu kutangazwa kwa mgomo huo jana, hawajaweza kuonana na madaktari zaidi ya kuhudumiwa na wauguzi kwa kugawiwa vidonge na sindano.
"Tunawaomba Serikali na madaktari wamalize tofauti zao, maana endapo hali hii ya mgomo ikiendelea tunaoumia ni sisi, na pia ni vyema Serikali ingesikia madai ya madaktari ili waweze kurejea kazini," alisema Joseph.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa kwa Jiji la Mwanza mgomo huo ulikuwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, tofauti na katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure ambapo madaktari na baadhi ya wauguzi walikuwa wanaendelea na kazi kama kawaida.