Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

Madaktari ni vyema sana mrudi kwny meza ya majadiliano,sio vizuri nyie kuwa wakaidi na kuwa na mioyo ya kinyama mkafikia hadi kuwauwa mama zenu na hasa wazazi wanaoenda kujifungua
 
UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA.
MADAI
1. Kuboresha Huduma za afya hospitalini kwa vifaa vya upimiaji, madawa.
2. Kuboresha Mazingira Ya kazi (ukarabati wa majengo, uongezaji wa vitanda)
3. Posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) 5% kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote.
4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu 40% ( MEANING anayefanya kazi SAME, TANDAHIMBA, NYAMPULUKANO nk ni tofauti na akaaye MJINI)
5. Posho ya makazi 40% au nyumba kama ilivyo kisheria(since DOCTOR IS ENTITLED KUPATA, HII NI KATIKA SHERIA YAO WENYEWE)
6. Bima ya Afya(Green Card) kwa wafanyakazi wote wa sekta ya Afya.
7. Kuwaondoa viongozi wa juu wa W/Afya kutokana na ubadhirifu.
8. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi 30% au Chanjo(Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB)

MAKUBALIANO
1. Kuondolewa kwa viongozi na watendaji wa juu wa Wizara ya Afya
2. Kupewa nusu ya ombi la call allowance hadi pale baada ya mazungumzo(ktk kipindi cha mpito)
3. Kamati kujadili na kuona kiasi gani mshahara na posho zitaongezwa kwa kutengeneza(developing a formula)
4. Serikali kuongeza bajeti ya W/Afya ili kuongeza vifaa, na madawa.

HALI ILIVYO SASA
- HOSPITALINI: hakuna huduma za afya (matibabu, upimaji wala upasuaji), YAANI NI KWELI TUMEGOMA
- VYOMBO VYA HABARI: Kuna upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwa umma.
- MTAANI:Hofu na mashaka kwa wananchi kutokana na kutoelewa matamko yanayopingana kati ya Serikali na Tamko la madaktari

MTAZAMO
HEBU ANGALIA KATIKA MAKUBALIANO NI LIPI LIMETEKELEZWA HADI SASA?? THEN SERIKALI INAONGEZA MISHAHARA YA WABUNGE, HIVI KARIBUNI UTASIKIA SABASABA!!!
- Jumla ya madaktari wote ni chini ya 15,000 (na hapa namaanisha General practitioners and Specialists). Kwa uchache au wingi wetu tumekwisha kuona madhara ya migomo miwili iliyokwishatokea.Nashangwazwa na kuona baadhi ya watu wanaosema madaktari hatuna utu wala huruma na tunaweka maslahi yetu mbele, hivi mnajua kuwa katika nchi za East and Central Africa, Tanzania ndiyo yenye kulipa mishahara midogo kwa watu wa sekta ya Afya?? Rwanda juzi juzi(1994) walikuwa na vita lakini daktari analipwa 1500USD, au mnadhani hatujui kuna nchi za jirani na mbali tunaweza kwenda kama wenzetu (Mf. Rwanda, Botswana, Zambia, Lesotho, Egypt, SA, nk)???mnadhani kubaki kwetu Tanzania tuteseke kwa kauli eti “UDAKTARI NI WITO?”, “WATANZANIA -WATOTO, KINA MAMA, NA WAZEE WATAKUFA IWAPO TUKIGOMA”, “OOOH?? HATUTAKIWI KUGOMA”…tumeonyesha uzalendo wetu kwa kubaki hapa hapa na mazingira yetu magumu, lakini sasa IMEFIKA MWISHO..
Pediatrics(wodi ya watoto):Hakuna vifaa vya kuongezea maji/damu mwilini(cannula), hakuna mitungi ya gesi, OBGYN(wodi ya kina mama);hakuna pamba, mipira ya mikojo(urine bags), MOI, Mwaisela hakuna vitanda, Operating Theatre,OT; Hakuna gloves ,mask, kofia za kutosha, Huduma ya mionzi ya CT SCAN ni mwezi wa saba haifanyi kazi(huku mmiliki akiwa anaidai Wizara ya Afya mil.800/=Tsh)na haitakuwepo hadi atakapolipwa.
Kwa madai hayo, si lazima serikali itekeleze all at once, lakini Mshahara unazungumzika, wale mnaofanya interview, huwa hamuulizwi ni kiasi gani unategemea kuanza nacho na waajiri wenu? Doesn’t this make salary being negotiable?? Then kwanini isiwe kwetu?
Hivi ulishawahi kusikia MASS RESIGNATION????? It takes ATLEAST 12yrs kumpata huyo specialist after elimu ya sekondari, Halafu nasikia mnasema eti tufukuzwe kazi?Then what??? Kwa wale wenye mtazamo mfupi mnadhani Serikali inaweza ku-import madaktari toka nje..kwa mfano
1.Ni nchi gani itakuazima madaktari?? Kwa mshahara upi na vifaa gani? CUBA-3000USD, RWANDA-1500USD!!!
2.Hypothetically speaking, wakikusaidia madaktari, watakupatia wangapi??
3.Apartment na transport allowances utawapa kiasi gani?
4.Hivi bibi aliye Tandahimba, asiyejua Kiswahili vizuri ataweza kuongea kiingereza na hao doctors??ama utahitaji wakalimani(translators), if so wangapi??? Utawalipa??
5.Then hao madaktari watakaa hapa milele??
Then NASIKIA MTATUPELEKA MAHAKAMANI.
Utawakamata madaktari wote nchini?? Kumbuka huu mgomo hauna kikomo na hauna kiongozi!!!..hypothetically speaking ukitupeleka, tutawatibu tukiwa huko gerezani?? Waliobaki mnadhani watarudi makazini?tukirudi mnadhani tutafanya kazi? Tukifanya kazi unadhani itakuwa katika kiwango kinachotakiwa? With demoralization unategemea tutaponyesha ndugu zetu kweli, au mortality kuwa juu??? Then kwa wanafunzi walio vyuo vya tiba kama MUHAS, WBUCHS, KCMC, UDOM, HKMU, IMTU..watafanya kazi hapa nchini kwa hali hii, ama Brain drain ndiyo itazidi!!
SIASA.
Wananchi walishazoea kudanganywa, na hii imezoeleka na viongozi Fulani kushindwa kufanya wajibu wao kusingizia wanasiasa kadhaa..Hapa HAKUNA siasa ila mkiileta tutawaachia tu kwani huko hatupawezi ila viongozi mjue hakuna tena rufaa ya kwenda nje(mf. INDIA) MUHIMBILI
Hivi wananchi mnajua viongozi wanalipwa kiasi gani wanapoenda nje kutibiwa na familia???
Eti kwa sababu sekta nyingine hawawezi kugoma, ndio na sisi tusigome? Eti kwa sababu askari anayetumia SMG na kupambana na jambazi anayetumia AK47, eti kwa sababu mishahara ya walimu inacheleweshwa, ndio tusigome??? Nani kasema??
HITIMISHO:
HAPA KAZINI HATURUDI…HII IELEWEKE VIZURI…HATURUDI….MGOJA NIIWEKE VIZURI HATURUDI, ACHA MEDIA IENDELEE KUDANGANYA, LAKINI UKWELI TUNAUJUA, MWISHONI MTARUDI TU, NA THIS TIME SI TENA YA KUTUMIA BUSARA ZETU KUWASTAHI VIONGOZI NA KISHA KWENDA PALE KUONGEA NA ‘WAZEE WA DSM”
“Doctors we might be slow walkers, but we never walk back” ..Solidarity Forever

nashukuru kwa kusema kweli kwani kweli hukuweka huru
 
you idea will work only if the goverment agree to handle the situation after the finish of V8 money,unless that will be just political bse the patient will continue to suffer after that.
 
Tanzania hii....hospital zote za rufaa...CT scan hazifanyi kazi,KCMC-zaidi ya miezi minne,Muhimbili-zaidi ya miezi sita,Mbeya-hamna...kwann asiitwe DHAIFU...tuone hatma ya mahakama na madaktari,ila kura yangu kwa madaktar,kama wameweza kupandisha mshahara kwa wabunge na madiwan...kwa nn cyo wao,ndo mana hata wakina Dr.Siyame wakaingia kwenye siasa wakiamini inalipa....na sio udaktr unaopambwa kwa kibwagizo cha kazi ya "wito"...wito wakati wananjaa,watafikiriaje,na ubongo ndo mafaili yao,nahisi baba Liz ajipange tu...akubali yaishe...
 
Jamani vp hospitalini kunapatikana huduma za matibabu? Vyombo vya habari naona vimepigwa biti havisemi lolote kuhusu huu mgomo!!


Je na JF imepigwa biti? Mbona sizioni habari za huu mgomo humu jamvini?

Au ma-Dr wametii amri ya mahakama??

Bugando hali ni mbaya! Nesi mmoja rafiki yangu kaniambia hata ku-satisfy vifo tu( kuidhinisha kuwa mtu kafa) hawataki na hata wodini hakuna dr. Kuna watawa ambao pamoja na utawa pia ni madokta, manesi nk, mgomo uliopita waliendelea kutoa huduma hapo hospitalini, kwenye mgomo huu 'usio na kikomo' nao hawapatikani...unapiga simu ya sista(dokta) inaita hadi inakatika. Najua hao makanjanja wa TBcisiem wanaishia OPD, wodini hali ni mbaya.
 
Wamegoma, hali ni mbaya, nsipande bodaboda, hamna huduma huko, ohoooooo

Asante mkuu! Narudia tena, wanaJF usijaribu kupanda pikipiki kama una haraka anza safari mapema au nenda kalale huko unakoenda ili kesho uwahi miadi yako!
 
huu ushabiki wa kufurahia mgomo ni ulimbukeni wa hali ya juu kabisa,ivi bibi yako au mama yako angekuwa anaumwa ungeweza kushabikia hii kitu????

Watanzania mbona tumebadilika kiasi hiki????

mbona tumekuwa na roho mbaya hivyo????



mi naomba kati ya nyie mnaoshadadia mgomo wa madaktari mpatwe na maradhi katika familia zenu hasa wale mnaowapenda na kuwathamini
mkuu ndugu zetu wengine tumesha wazika kwa sababu ya migomo hii, ubovu wa mazinila ya kazi unaua watu madaktari wakishuhudia sasa wamegoma ili wote mshuhudie vifo hivyo.
kumbuka mimi na wewe tu wagonjwa watarajiwa tukifa katika migomo inoyodai mabadiliko yakweli, watakao kuja watatuenzi huku wakisema tumewafaa sana. Usiogope gharama
 
FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu"SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
HALI HALISI HOSPITALINI:
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
1. Madai ya madaktari yalianza lini?
2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

VYOMBO VYA HABARI:
Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
MKAKATI:
Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
2. Wanatumia pesa ya nani?
3. Last‘episode" walileta wanajeshi,
KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

MAKOLIGI (colleague)??
Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government's responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
..Solidarityforever..
 
Madakitari sasa wamesema hakuna referal India tena, wakipenda waende kwa Babu
 
Back
Top Bottom