Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Jun 24, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  WAKATI kukiwa na mgawanyiko mkubwa kwa madaktari nchini katika kushiriki mgomo ulioitishwa na Chama cha Madaktari nchini (MAT), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Said Meck Sadik amepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote katika hospitali za Jiji, yenye lengo la kuchochea watumishi wa afya kugoma.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Sadik alisisitiza kuwa Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kushiriki katika kuwashawishi watumishi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari na wauguzi kugoma.

  Sadik anaungana na viongozi wengine wa kitaifa na Mahakama Kuu ya Tanzania, kutoa amri ya kusitishwa kwa mgomo huo wa madaktari ambao ulianza jana katika baadhi ya hospitali huku huduma katika hospitali nyingine zikiendelea vizuri kutokana na madaktari na wauguzi katika hospitali hizo kutogoma.

  "Kufuatia tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi."

  Ilisema taarifa ya Mahakama Kuu kwa vyombo vya habari. Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa kufuatia maombi namba 73 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania.

  Gazeti hili lilipofika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana asubuhi lilishuhudia madaktari wakiendelea na kazi kitendo kilichoonesha kuwa hawakushiriki katika mgomo.

  Wakati hayo yakiendelea, Serikali imeendelea kuwataka madaktari wote nchini kuendelea na kazi wakati suala la kupatiwa suluhisho likiwa katika chombo cha kisheria Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.

  Pia imesema itakuwa tayari kutekeleza maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi, kuhusu mapendekezo yatakayotolewa juu ya suala zima la maslahi na haki za madaktari kama maombi yao yalivyowasilishwa.

  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Selaman Rashid, aliyasema hayo mjini Morogoro jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kuona iwapo madaktari wameamua kutekeleza mgomo wao au la.

  Akiwa hospitalini hapo, Naibu Waziri huyo alishuhudia madaktari kwa kushirikiana na wauguzi wakiendelea kufanya kazi mbalimbali za kuhudumia wagonjwa licha ya Chama cha Madaktari kutoa tamko la kuwataka wagome nchi nzima kuanzia jana.

  Uongozi wa Hospitali ya Rufaa hiyo ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa , Dk. Godfrey Mtey , ulimtembeza Naibu Waziri maeneo mbalimbali ikiwemo wodini, maabara na chumba cha kujifungulia na kuzungumza na baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakipatiwa tiba.

  "Nawaomba madaktari wote waendelee na kazi ya kuwahudumia wagonjwa wakati suala lao lipo kwenye chombo cha kisheria ...sote tumekubaliana usuluhishi wa mgogoro huu uamuliwe na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Hata hivyo alisema, Serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha maslahi ya wafanyakazi wote si kwa ajili ya madaktari pekee ili wapate mishahara kulingana na kazi wanazozifanya.

  Alisema, Serikali inapozungumzia mishahara haizungumzii kwa daktari pekee bali inazungumzia sekta mbalimbali na si kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pekee bali na wizara nyingine za Serikali.

  Aliupongeza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa watumishi wake wakiwemo madaktari kuendelea na kazi za utoaji wa huduma kwa wagonjwa. Kutoka Dodoma taarifa zinasema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dk Ezekiel Mpuya alisema jana kuwa hali ni shwari katika hospitali hiyo na hakuna mgomo.

  Akizungumza na gazeti hili, Dkt. Mpuya alisema madaktari na wauguzi walikuwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida na hakukuwa na mgomo wowote.

  "Hali ni shwari na wale wote wenye zamu wako kazini isipokuwa daktari mmoja aliyeko kwenye mafunzo leo hajaripoti sijui ana tatizo gani, lakini hapa hakuna mgomo," alisema.

  Hata hivyo hali haikuwa shwari jijini Mwanza kwani madaktari zaidi ya 200 waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando walianza mgomo rasmi jana baada ya Serikali kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu madai yao mbalimbali.

  Katika mahojiano na gazeti hili Mwakilishi wa Kamati ya kufuatilia madai ya Madaktari hao waliyapeleka serikalini, Dk Richard Kirita alisema kwamba madaktari wa kada zote katika hospitali hiyo wapo kwenye mgomo isipokuwa baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wakuu wa idara.

  Mapema wiki hii, Kamati ndogo ya Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyokuwa ikifuatilia mgogoro dhidi yao na Serikali ilisema haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na Serikali juu ya madai yao na kuonesha nia ya kufanya mgomo wa nchi nzima kuanzia jana.

  "Ni kweli tumeanza mgomo rasmi, madaktari waliokuwa zamu leo (jana) hawajaenda kazini, hata hivyo kwa kuwa leo si siku ya kazi unaweza kudhani hakuna mgomo, lakini njoo Jumatatu ndio utapata picha halisi ya mgomo kwa sababu wagonjwa watakuwa wengi lakini hakutakuwa na huduma," alisema Dkt. Kirita.

  Hata hivyo alisema kwamba wanaendelea na vikao ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wenzao wa Dar es Salaam ili kujua ni hatua zipi zaidi wachukue kuhusiana na mgomo wao huo.

  Dkt. Kirita alisema kwamba katika kikao cha madaktari wa Bugando kilichofanyika hivi karibuni kujadili majibu ya Serikali juu ya madai yao na kuhusisha jumla ya madaktari 202 walikubaliana kwa pamoja kuanza mgomo kuanzia jana iwapo madai yao hayatatekelezwa na Serikali.

  Katika mgomo wa kwanza wa madaktari uliofanyika mapema mwaka huu madaktari walikuwa na madai mbalimbali yakiwemo ya kuboreshwa kwa huduma za afya zikiwemo dawa, vitanda na vifaa tiba, mishahara na nyumba za madaktari.

  Baadhi ya watu waliokuwa wamepeleka wagonjwa katika hospitali hiyo jana walionekana wakiwaondoa baada ya kukosa huduma kutoka kwa madaktari ambao baadhi walikuwa kwenye kikao na wengine walionekana katika vikundi vikundi wakipiga soga.

  Kwa upande wao wagonjwa katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Bugando wameiomba Serikali pamoja na madaktari walio kwenye mgomo kumaliza tofauti zao ili madaktari waweze kurejea kazini na kuwapatia huduma.

  Wakizungumza jana katika wodi namba 6 na 8, Yohana Matinde, Abel Joseph, Martha Maduhu na Pendo Saimon walisema kuwa tangu kutangazwa kwa mgomo huo jana, hawajaweza kuonana na madaktari zaidi ya kuhudumiwa na wauguzi kwa kugawiwa vidonge na sindano.

  "Tunawaomba Serikali na madaktari wamalize tofauti zao, maana endapo hali hii ya mgomo ikiendelea tunaoumia ni sisi, na pia ni vyema Serikali ingesikia madai ya madaktari ili waweze kurejea kazini," alisema Joseph.

  Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa kwa Jiji la Mwanza mgomo huo ulikuwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, tofauti na katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure ambapo madaktari na baadhi ya wauguzi walikuwa wanaendelea na kazi kama kawaida.
   
 2. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Iwapo madaktari hawapewi haki zao basi serikali yetu dhaifu iturudishie kikombe cha babu!!

  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
   
 3. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mgomo umeanza vyombo vya habari vimetishiwa ole wake atakaye tangaza kuwa mgomo umeanza. Suluhisho mahakamani ni miaka 5 mdhaifu hata kuwepo.
   
 4. O

  Optimisticforchange Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ahaaaaaa! Kumbe wao wamekunywa kikombe so wanauhakika wa kutoumwa ndo maana hawajali mgomo wa madaktari na pia bado wana uhakika wa kutibiwa India. Na ndo maana juzi badala ya kuwaongezea maslahi madaktari wameamua kujiongezea wenyewe toka mil. 7 hadi 10. Du, Ee mungu tunaomba 2015 ije haraka.
   
 5. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  heshima yangu kwa vyombo vya habari kwisha, kama wanapgwa mkwara wanatulia.
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Dk. Ulimboka anenaMwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, alisema hawajapata taarifa zozote kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ya kuzuia mgomo huo.

  Alisema mgomo ulioanza jana haukihusishi Chama cha Madaktari nchini (MAT).Alisema wao taarifa hizo wamezisikia katika vyombo vya habari hivyo hawajui kama zinawahusu wao au MAT, na kwamba itakuwa ni vigumu kutolea ufafanuzi jambo lisilowahusu.

  Dk. Ulimboka alisema kuwa kimsingi serikali imekuwa ikipotosha dhana nzima ya mgomo huo kwani inaonyesha kuwa suala la posho ndilo linalogomewa na madaktari wakati si kweli.

  "Watu wanadhani tunapigania posho zaidi, hapana tunapigania huduma bora kwa wagonjwa, kwa sababu sifa ya kwanza katika hospitali ya rufaa ni kuhakikisha yale yanayoshindikana katika hospitali nyingine yanawezekana katika hospitali za rufaa," alisema.

  Alitolea mfano kifaa cha kupimia cha CT- SCAN ambacho kina zaidi ya miezi saba hakifanyi kazi katika Hospitali ya Muhimbili huku ikiwalazimu baadhi ya wagonjwa wanaofika kutakiwa kufanya kipimo hicho katika hospitali nyingine.

  "Wengine hawana uwezo huo, wale wanaobahatika kufika huku wanakuta kifaa hakifanyi kazi, huyu ni mgonjwa bado unamuongezea gharama nyingine, tukiyasema haya wanasema sisi hatuwajali wagonjwa," alisema Dk. Uliomboka.

  Alisema madai mengine ni pamoja na miundombinu ya hospitali kwa kile alichoeleza haziwiani na idadi ya wagonjwa na kutolea mfano wodi ya watoto katika Hospitali ya Temeke kuwa mazingira ni magumu.

  Alibainisha kuwa kitaaluma ni lazima wawahudumie wagonjwa wakiwa vitandani na inapotokea wagonjwa wakiwa chini inawawia vigumu kuwahudumia, na kwamba hayo ndiyo masuala waliyokuwa wanalalamikia.

  "Kwanini hospitali zetu ziwe sehemu ya mateso kwa wagonjwa badala ya kuwa sehemu ya faraja? Tunaambiwa tuwaandikie dawa wagonjwa, wakienda dirishani hata
  Panadol hakuna, haya hawataki kuzungumzia, wameamua kupandisha posho ya maiti wakati hata katika madai yetu hatukuwa na dai hilo," alisema.

  My take
  Aisee mie nilidhani ni posho tu kumbe mambo kibao. Hapo kwenye red aibu...nchi yenye raslimali zote hizi kukosa Panadol!!!!

  Source : Tanzania Daima Jumapili

   
 7. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  [h=6]HATIMAYE madaktari nchini jana walianza mgomo usio na kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwatimizia matihaji yao ikiwamo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi pamoja na kuwapandishia mishahara.

  Uamuzi huo wa madaktari unapingana na amri ya Mahakama Kuu Tanzania, Kitengo cha Kazi ambayo juzi ilizuia mgomo huo baada ya kupokea maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).

  Mahakama hiyo ilitoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo shauri la pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama hiyo iliyotolewa juzi jioni na kusambazwa kwenye vyombo vya habari, imewataka MAT na wanachama wake kutoshiriki kwenye mgomo huo.

  Mgomo waanza

  Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam huduma za dharura zinatarajiwa kusitishwa wakati wowote kuanzia sasa.

  Mgomo huo unaanza wiki mbili baada ya madaktari hao kuitaka serikali itekeleze madai yao la sivyo jana wangeanza mgomo usio na kikomo.

  Tanzania Daima Jumapili, lilitembelea hospitali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Muhimbili na zile za mkoa ambazo ni Temeke, Amana na Mwananyamala na kushuhudia kusuasua kwa huduma.

  Vitengo vya dharura katika hospitali hizo viliendelea kupokea wagonjwa huku baadhi ya madaktari wakiweka wazi kuwa kuna uwezekano wa huduma hizo kusimama katika muda wa saa 24 kuanzia jana.

  Muhimbili

  Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wagonjwa walilamikia huduma zilizokuwa zikitolewa huku wengine wakisema wametelekezwa na wauguzi waliokuwa zamu.

  Eneo la mapokezi baadhi ya askari walionekana wakiwaeleza wagonjwa waliofika kuwa huduma zimesimama na kuwasihi waondoke eneo hilo.

  Mgonjwa mmoja ambaye alionekana kuchanganyikiwa alisikika akisema kuwa alimkabidhi nchi Rais Jakaya Kikwete lakini haieleweki kiongozi huyo anakoipeleka.

  “Rais Kikwete nilikukabidhi nchi hii sasa unaipeleka wapi?” alisikika akisema.

  John Kobelo, alisema kuwa tangu juzi kijana wake alitakiwa kufanyiwa upasuaji lakini ilipofika jana aliambiwa ampatie mgonjwa wake chakula kutokana na huduma hiyo kutokuwepo.

  “Kwa kweli hali inasikitisha na kukatisha tamaa, sijui nchi hii tunaelekea wapi maana viongozi wanaamua kwa makusudi kuchezea uhai wa Watanzania,” alisikika baba mmoja akilalamika.

  Tanzania Daima Jumapili ilifika katika wodi ya Sewa Haji na kukutana na mgonjwa ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake lakini alilalamikia kitendo cha madaktari kushindwa kupita zamu kwa siku ya jana huku huduma zikiwa zimezorota.

  Katika wodi ya Kibasila gazeti hili lilikutana na baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao walikuwa wakiangaika kumhamisha mgonjwa wao aliyekuwa akilalamika kwa maumivu makali.

  Gazeti hili halikuishia hapo kwani lililazimika kufika katika Kitengo cha Mifupa (Moi) ambapo ilikutana na Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Jumaa Almasi, ambaye alisema kuwa kwa jana ilikuwa ni vigumu kuzungumzia mgomo huo kutokana na kuwa siku ya mapumziko.

  “Unajua kwa (leo) yaani jana siwezi kuzungumzia mgomo kwa kuwa tuna kliniki mbili za binafsi, labda picha kamili ya kuwepo kwa mgomo tunaweza kuipata kuanzia Jumatatu, kwa vile kuna kliniki zote,” alisema.

  Aidha, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alijikuta akishindwa kutokea katika kikao cha waandishi wa habari alichokiita ofisini kwake.

  Mwananyamala na Temeke

  Hali ilikuwa si shwari kwani baadhi ya wagonjwa walisikika wakisema kuwa hawajapata huduma na baadhi ya wauguzi wanajifanya kutoa huduma baada ya kuona wanahabari.

  Katika Hospitali ya Amana, Tanzania Daima Jumapili ilishuhudia shughuli za matibabu zikiwa zinaendelea ingawa baadhi ya wagonjwa walikuwa wakilalamika kukaa muda mrefu pasipo kupatiwa huduma.

  Mmoja wa watu waliokuwa hospitalini hapo aliyempeleka ndugu yake kupatiwa huduma baada ya kupata ajali aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa wamekaa katika eneo hilo zaidi ya saa tatu bila mgonjwa wake kupatiwa matibabu.

  “Nipo hapa na huyu afande tumemleta mtu aliyepata ajali maeneo ya Sitakishari lakini hatujahudumiwa mpaka saa hizi sasa sijui ndiyo wanagoma kisirisiri?” alisema mtu huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

  Katibu wa utawala wa hospitali hiyo, Tunu Mwachale, alisema madaktari waliotakiwa kufika zamu kwa siku ya jana wote walifika na kwamba walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida.

  Dk. Ulimboka anena

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, alisema hawajapata taarifa zozote kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ya kuzuia mgomo huo.

  Alisema mgomo ulioanza jana haukihusishi Chama cha Madaktari nchini (MAT).

  Alisema wao taarifa hizo wamezisikia katika vyombo vya habari hivyo hawajui kama zinawahusu wao au MAT, na kwamba itakuwa ni vigumu kutolea ufafanuzi jambo lisilowahusu.

  Dk. Ulimboka alisema kuwa kimsingi serikali imekuwa ikipotosha dhana nzima ya mgomo huo kwani inaonyesha kuwa suala la posho ndilo linalogomewa na madaktari wakati si kweli.

  “Watu wanadhani tunapigania posho zaidi, hapana tunapigania huduma bora kwa wagonjwa, kwa sababu sifa ya kwanza katika hospitali ya rufaa ni kuhakikisha yale yanayoshindikana katika hospitali nyingine yanawezekana katika hospitali za rufaa,” alisema.

  Alitolea mfano kifaa cha kupimia cha CT- SCAN ambacho kina zaidi ya miezi saba hakifanyi kazi katika Hospitali ya Muhimbili huku ikiwalazimu baadhi ya wagonjwa wanaofika kutakiwa kufanya kipimo hicho katika hospitali nyingine.

  “Wengine hawana uwezo huo, wale wanaobahatika kufika huku wanakuta kifaa hakifanyi kazi, huyu ni mgonjwa bado unamuongezea gharama nyingine, tukiyasema haya wanasema sisi hatuwajali wagonjwa,” alisema Dk. Uliomboka.

  Alisema madai mengine ni pamoja na miundombinu ya hospitali kwa kile alichoeleza haziwiani na idadi ya wagonjwa na kutolea mfano wodi ya watoto katika Hospitali ya Temeke kuwa mazingira ni magumu.

  Alibainisha kuwa kitaaluma ni lazima wawahudumie wagonjwa wakiwa vitandani na inapotokea wagonjwa wakiwa chini inawawia vigumu kuwahudumia, na kwamba hayo ndiyo masuala waliyokuwa wanalalamikia.

  “Kwanini hospitali zetu ziwe sehemu ya mateso kwa wagonjwa badala ya kuwa sehemu ya faraja? Tunaambiwa tuwaandikie dawa wagonjwa, wakienda dirishani hata Panadol hakuna, haya hawataki kuzungumzia, wameamua kupandisha posho ya maiti wakati hata katika madai yetu hatukuwa na dai hilo,” alisema.

  Matabibu asili wanena

  Chama cha Utabibu wa dawa za asili Tanzania (ATME) wamewataka madaktari nchini kutopoteza uhai wa binadamu wenzao kama njia ya kuishinikiza serikali kusikiliza na kuwatekelezea madai yao.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama hicho, Simba Abrahaman, alisema kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki wagonjwa ya kupata matibabu.

  Abrahaman aliwataka madaktari kukaa meza moja na serikali katika kuweza kutatua malalamiko yao na si kugoma ambapo anayeathirika ni mwananchi kwa kukosa haki hiyo ya huduma za afya.

  Aidha, katika kuhakikisha mgogoro kama huo hautokei tena siku za usoni, alisema ni vema kukaundwa mfuko wa afya ambapo wananchi wataweza kuuchangia, kwa kuwa ukweli ni kwamba wamekuwa wakiitikia kuchangia mambo mbalimbali ikiwamo vyama vya siasa, hivyo halitakuwa zito.
  [/h]
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Serikali yetu inapotosha ukweli ikitarajia public sympathy! DHAIFU!
   
 9. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kukosa Panadol!!!! bado sielewi
   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,071
  Trophy Points: 280
  Hatakama madakitari wanakosea lakini serikali inakosea zaid,

  Afya yetu hainamjadala kabisa, lakini serikali imeiweka rehani kwa kutuhadaa na mihospitali na zahati zisizo na viwango, vifaa wala madawa.

  Waziri mkuu wa kenya alifanyiwa upasuaji wa kichwa (ubongo) chake pale Nairobi sio india, china wala ujerumani

  Vipi hapa kwetu, si waboreshe huduma ili wao nasisi sote tutibiwe hapahapa, tutawaamini vipi iwapo wao huenda nje inchi?

  Wanasiasa, mafisadi na matajiri matibabu nje ya inchi, lakini sisi walalahoi tunabakia na matibabu feki yasio na tija.

  TUACHE UOGA TUWE NA PA KUANZIA.
   
 11. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  huelewi au huamini?kama huelewi basi ujue hospitali hazina parasetamo,kama huamini nenda muhimbili utaambiwa kanunue hapo nje ya geti.yaani kile kikaratasi kitasomeka O/S
   
 12. a

  adolay JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,071
  Trophy Points: 280
  Nahapa ndo penye utata tunawalaumu madakitari ili iweje? jamani hospitali na zahati za serikali ni janga la kitaifa kila kitu ni duni, serikali lazima iboreshe mazigira yake kwa afya za watanzania wote.
   
 13. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,646
  Trophy Points: 280
  wanasema huduma kwa wazee ni bure lakini ukienda hakuna dawa.Wansema huduma kwa watu wa bima ni bure lakini ukienda hakuna vipimo stahiki.  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 14. t

  tupak Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilianza kuishangaa Tanzania kwa nini ni maskini siku nyingi sana lakini watu walikuwa hawaniandiki gazetini
   
 15. a

  adolay JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,071
  Trophy Points: 280
  Inauma sana kwa wagonjwa na kwa ndugu na jamaa wenye wagonjwa kukumbana na kadhia ya mgomo huu.

  Lakini hata vitani inchi inapoingia kupigana kuitaka haki hupeleka wanajeshi walio hai wakafa wakipigana kuitafuta haki, hivyo kama madawa, vifaa na mazingira ya matibabu ni duni basi tuingie vitani ili serikali iaache ngojela iwe na vitendo vya ufanisi.

  BORA MGOMO PENGINE TUTABORESHEWA MATIBABU, KULIKO WAKAENDELEA KUHUDUMU NA KUTOA TIBA FEKI ZISIZO NA DAWA WALA VITENDEA KAZI

  BORA WAKATAE KUTOA TIBA ZA KIINIMACHO.
   
 16. W

  William wa Ukweli Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umesomeka Uda inasikitisha sana, inauma sana na inadhalilisha sana! Chama Cha Mapinduzi kitaitisha kikao cha dharura ili Kamati Kuu ya NEC itoe kauli kwa serikali ya CCM ichukulie matatizo katika sekta ya afya kwa uzito unaostahili. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

  Penginepo tujitahidi kuwa makini, tusiingilie uhuru wa Mahakama zetu, ikiwemo kitengo cha Mahakama ya Kazi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Vipaumbele vya matumizi ya serikali ndio vinavyosababisha ukosefu wa dawa na vifaa tiba kwenye hospital zetu. Fikiria ziara ya Raisi inatengewa mabilioni katika Hali hii hakuna cha kushangaza unapokosa dawa. Hivi ukihesabu madaktari wanaofanya kazi katika hospital zetu wanafika elfu moja? I doubt cause majority are in projects and out of clinical activities. can some one issue the numbers? Am sure we will be surprised with the number.
   
 18. s

  simon james JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Songeni mbele madaktar wananch tunaunga mkono
   
 19. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,646
  Trophy Points: 280
  hii hapa yaweza kuwa taswira ya nchi kwa sasa

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 20. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kilichonishangaza ni pale hata wanajeshi wanahangaika kumhamisha mgonjwa Muhimbili......baada ya kukosa huduma. Nao bado wanachekacheka tu..............nchi hiiii imejiozea.
   
Loading...