Madaktari saidia ushauri hapa please | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari saidia ushauri hapa please

Discussion in 'JF Doctor' started by Ubungoubungo, Jan 22, 2009.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jamaniee, mimi na waifu wangu tunaishi vizuri sana. kwa kawaida, kwetu sisi tuliooa ni kawaida kujua kila kitu kinachoendelea kwa wake zetu. mara nyingi mke wangu akiwa katikati ya mwezi, yaani siku y akumi na tatu au ya kumi na nne baada ya bleed, siku hizi zote huwa anakuwa mkali kishenzi. tunaweza kugombana hata kwa kijiko au hata kiti tu. mida hii kwa wale wanandoa mnajua kuwa ndo yai huwa limeiva na limeteremka tayari kusubiri mbegu, yaani 13-14 days after the cycle.

  madaktari naomba mnisaidie, hivi hii ni kwanini? au kama yai limeiva wanawake wote wanakuaga wakali hivyohivyo? au ni kwangu tu. yaani siku zote huwa namvumilia tu kwasababu mida hiyo huwa ndo siku zake za kuchukia na kuwa mkali katika kila kitu. na nina uhakika ni tarehe hizo,kwasababu tuko makini sana kuhesabu tarehe ili tuzae watoto wetu kwa uzazi wa mpango, tunatumia kalenda, hatutumii kondomu wana vidonge. mara nyingi akifika siku hizo, anakuwa mkali, nisaidieni ni tatizo au ndo hormon? au nini jamani.
   
 2. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usaidiwe nini!!!!! Mimi naona iko wazi kuwa hamtumii njia nyingine za uzazi wa mpango kwa hiyo mkeo hataki kupata mimba. Ukimjigijigi atapata mimba sio. Au kuna jambo watuficha?
  Anyways, tusubiri wataalam wa akina mama nao waseme.
   
 3. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole kaka, ila hii nso naisikia kwako mwanamke kuwa mkali wakati wa ovulation period! maana mimi kwa kipindi hiko kwa kweli huwa mpole sana na kutamani niingiliwe na mwenzangu ili muwashawasha ushuke. Je, umejaribu kuomba kujigjig mda huo na reaction yake ilikuwaje?
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,125
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Inahusiana na hormone zinazokua released wakati wa ovulation, sinaathiri anavyojisikia. Hakuna la kufanya zaidi ya kushukuru umezaliwa mwanaume!
   
 5. Nyaralego

  Nyaralego JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2009
  Joined: Nov 13, 2007
  Messages: 732
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  It's just the hormones, that brings about those mood swings.
   
 6. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwanza naona kuna tatizo la jinsi unavyohesabu siku, kwa kawaida kalenda inaanza pale mwanamke anapoanza menstruation (bleed) na sio anapo maliza bleeding,hata ivyo hiyo day 13,14 ni ideal kwa watu wenye mzunguko wa siku 28 kamili. Kwa sababu kuna wanawake wanye mzunguko wa siku 24,25..........32,hadi 35 na ovulation inabadilika kulingana na mzunguko wake.
  Kwa binadamu kawaida anapokuwa kwenye ovulation huwa anahamu sana ya kuingiliwa, hivyo pengine ukali wa mwenzio ni njia anayotumia kama contraception kwa sababu hamtumii njia nyingine anpokuwa kwenye 'ovulation'.
   
 7. C

  Camfu Member

  #7
  Jan 23, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  bila shaka anakuwa mkali kwa sababu anatamani kitu nawe haumpi hivi mwasho unamnyima raha, ndio maana umekuwa mume wake ili umfae wakati wa tabu na raha hizi ndio zile nyakati za tabu kwa mke wako, mfariji kwa kumpa haki yake...
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ubungo2,
  Hiyo hali inakuja involuntarily.Hakuna haja ya kumlaumu au kumkasirikia mwenzio.Wanaume wenye uelewa huwa wapole na wavumilivu.Hormonal changes huleta hali hiyo na zikijirekebisha basi hurudia hali ya kawaida na kuwa mpole tena.Hujasikia watu wakizungumiza kuwa at times wanawake hupata kama ukichaa fulani hivi..hawatabiriki, hubadilika ghafla? Basi usipoelewa haya mambo mnaweza kuishia pabaya kwenye mahusiano yenu.Ukali huo hauishii kwako wewe mume tu..huenda hata kwa watoto na watu wengine hata kazini! Maajabu ya Mungu katika uumbaji...lazima kuna sababu!
   
 9. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi sio daktari na wala sina ushauri wowote kulingana na tatizo lako,ila napenda kuwapa pongezi sana wewe na mke wako kwa kutotumia "Kondom' na vidonge vya uzazi wa mpango.Simameni imara katika maamuzi yenu hayo.Kondom na vidonge vya uzazi wa mpango ni mipango ya kishetani yenye ajenda maalum ya kupunguza watu!Sasa kwa vile wasomi wetu wamekuwa wasomi uchwara,wameingia mikataba ya kishenzi na agents wa maruhani au mashetani kwa kujua au kwa kutokujua ili kutumaliza katika harakati zao za kuganga njaa!Narudia tena,hongereni sana.

   
  Last edited: Jan 23, 2009
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ubungo, siku ya 13-14 baada ya bleeding si wakati wa ovulation. Ovulation hutokea 2wks (on average) tangu siku ambayo bleeding imeanza. Na wakati wa ovulation Mama anakuwa mtafutaji na wala si kungoja kuchokozwa kama wakati mwingine wowote. Kwa hiyo kama hesabu zako zinaanzia siku anayomaliza ku-bleed basi wewe unaongelea kipindi ambacho hormone anazokuwa nazo wakati huo si ajabu kumsababishia mood za ajabu ajabu.

  Hata hivyo kama hesabu unazotoa ziko sahihi, basi inawezekana inatoka na suala la kutotumia contraceptives zozote na kwa hiyo hamuwezi kufanya mapenzi kipindi ambacho mama anatamani sana kufanya tendo la ndoa kama alivyosema Camfu.. (post # 7)

  Kwa hiyo jitahidi kufanya tendo la ndoa wakati huo kwa kuchukua tahadhari ili asipate mimba kama mumeamua kupanga uzazi. Rhythm withdrawal inaweza kusaidia ila ni hatari sana. Kama hamuwezi kutumia hormonal contraceptives basi kamata kondom vinginevyo mzee ufanye utaratibu wa vasectomy!!
   
 11. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
 12. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unajitesa mkuu? Kwa nini unamtesa shemeji?

  Mimi naamini manaweza kufanya mapenzi muda wowote mnaotaka. Kuridhishana sio lazima kuwe na 'intercouse'. Mnaweza mkabuni njia nyingi tu mbali na intercourse na wote mkaridhika. Tembelea jamvi la 'mambo ya wakubwa' na imani utapata mawili matatu!

  You dont need to wait for anything!
   
  Last edited: Jan 23, 2009
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hiyo inaitwa abiria chunga mzigo wako, anajua akikuchekea chekea anaweza akabakia anaugulia miezi tisa ijayo.

  Jaribu kumshawishi muanze kutumia njia za uzazi wa mpango badala ya kuhesabu vidole. Itampunguzia Stress na tensions kipindi hicho cha mpito.

  Halafu mnaozungumzia menstruation cycle ya 28 days, hata wanawake walio normal kuna miezi siku zinazidi au hupungua kwa siku moja na kadhalika. Kutegea siku ya 14 huenda hesabu ikawa si sahihi vile vile...

  BTW, nishawahi kusikia viumbe wengine wanaokuwa wakali kipindi wakiwa kwenye heat...
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jamani, mimi najua kuwa kalenda huwa naanza kuhesabu siku ya kwanza ni ile anayoanza kubleed. yaani anapoanza kubleed ndio siku ya kwanza, ukihesabu hadi hapo, ukifika siku kuanzia ya kumi na moja hadi kumi na tano, ndizo siku za yai kuwa katikati approximately. ndio maana nasema siku 14 baada ya bleed. sasa wewe hujaelewa nini? mbona hata ulichoongea ni kilekile. yaani ukianzia kuhesabu siku ile ya bleed ndo ya kwanza, zile siku utakazohesabu si ndo utaziita siku baada ya bleed? au nakosea?

  asanteni kwa ushauri wenu.
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  28 toa 14 hadi 16 hizo ni ngapi mzee, si itaangukia kwenye siku hizohizo nilizozitaja mimi? wiki mbili ina siku kumi na nne. kuhesabu tunaanza kuhesabu siku ya kwanza ndio ile anayoanza kubleed. day one ni ile anayoanza kubleed hesabu hadi kumi na tatu hadi kumi na nne, is what i am talking about. ila for safety, sisi tunajua kuanzia siku ya kumi hadi siku ya kumi na saba hivi ni danger zone. sasa wewe unaelewa nini mkuuu. her cycle ni 28 exactly. thank God.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  People don't read your minds but what you present to them. In your case, "baada ya bleed" gives an impression that you were talking of days "after bleeding ceases" and not "from the onset of bleeding". But now everything is clear, particularly to me. As others have said, to avoid sex at ovulation is a big mistake and you are going to sexually destroy your wife. You urgently need to look for the right methods of making safe sex or try VASECTOMY as I said before.
   
Loading...