mzee mwanakijiji nakupongeza kwa makala yako nzuri, nimeisoma kwa kina nakuielewa, kwa wenzetu waliozoea ku copy n ku pest kwao bado ni ngumu kuelewa, ukweli ni kuwa THE LAW IS BLIND! IT CANT SEE AND WORSE ENOUGH IT CANT MAKE ITS OWN DECISION INSTEAD IT DEPENDS ON THE MINDS OF THE ONE WHO OWN IT!
madakatari tumeliona hilo, 2najua kamwe hamna mgomo halali, isipokuwa tu mgomo wa hiari kwa waumini wanpogoma kula na kunywa kumuomba Mungu kuwasamehe, kuwabariki etc.
inapokuja swala la jambo nyeti kama hili la madakatri kugoma watawala wakatumia nguvu kubwa kutafuta majibu rahisi badala yakutafuta mbinu thabiti zakuutatua inaonyesha unyonge wa fikra za watawala, napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa, mbinu zakung'oana meno na kucha kwa koleo zilitumiwa na wakoloni na kwa kuwa mifumo yetu ni muendelezo wa pale wakoloni walipo achia ndiyo waona wanatumia mbinu kama hii.
Rais Kagame jana akihutubia taifa na Mh rais wetu akiwepo alikemea tabia ya viongozi wakiafrika ku google majibu ya matatizo yao badala yakutumia bongo zao. Inashangaza viongozi wanapotulazimisha kuona rangi nyeusi kuwa nyeupe, wantamani kujua ni nani anafadhili mgomo wa madaktari na hawatamani kuona wala kusikia mahitaji halisi ya watumishi wa afya na wananchi kwa upana wake. ukweli ni kuwa hakuna anayefadhili mgomo wa madaktari kwa fedha, mawazo, au aina yoyote ya msaada. Madaktari tunao uwezo wakufikiri na kuamua bila kutumiwa na mtu na zaidi hatuna nia yoyote yakuichafua serikali kwa kuwa hatuwezi kukata tawi tulilokalia.
Ndugu zangu kwa hakika sisi tulio katika fani hii tumeona mengi sana, iadadi ya wagonjwa wanaokufa kwa kukosa vifaa tiba na madawa ya gharama nafuu ni kubwa sana na kibaya zaidi wanapokufa ndugu huishia kulia kidogo nakusahau mpaka atakapokufa mwingine ila kwetu tunaona mambo hayo kila iitwapo leo.
nina kubali kabisa kuwa kiapo cha watumishi wa afya hakiruhusu mtu kugoma ila kina mtaka mtoa huduma ya afya kuweka mbele haki ya uhai wa mgonjwa kwa gharama yoyote ile, na hiki ndicho tunachikifanya, kuiambia serikali ya kuwa tunataka mabadiliko katika sekta ya afya, kwa upana wake.
wanaosema madaktari ni watu wenye ubinafsi na wanaotamani kuishi maisha yakiteule siyo kweli , kinachotusukuma ni kutaka kuona sekta ya afya inapewa kipaumbele kinacho stahili, tuna omba umma wa Watanzania wajue kuwa hatuna nia yakutaka wao wapunguziwe maslahi tupewe sisi la hasha tunaamini kila mtumishi wa umma anapaswa kupewa maslahi yanayolingana na mahitaji yake na kulingana na vigezo vilivyopo na uhalisia wa maisha.
Niwakumbushe tu ya kuwa serikali hii hapo mwaka 1998 ilifanya upembuzi yakinifu kuangalia ni viwango gani vya mishahara kitakacho stahili kulipwa kila mtumishi wa umma kwa vigezo vilivyo ainishwa na ripoti hiyo na mapendekezo yake yapo mezani kwa ofisi ya utumishi, nawasihi kila mmoja pale alipo aitafute aisome aone mwaka 1998 alipaswa lipwa shilingi ngapi kwa ugumu wa maisha ya wakati ule kisha aone kwa sasa atastahili kulipwa kiasi gani.
siyo hilo tu pia kuna miongozo na taratibu za kazi baada ya muda wa kawaida wa kazi, safari za kikazi na kadhalika , ni vyema pia wakazisoma waelewe haki zao,badala yakusikia mambo yanayoelezwa kwa umahiri na mwajiri tu bila kumpa mwajiriwa fursa yakueleza upande wake.
nina wasihii Watanzania wenzangu hasa madakari (MD) assistant Medical officers (AMO) clinical Officers (CO) na watendaji wengine wote wa sekta ya afya tuungane pamoja kudai kuboreshwa kwa sekta ya afya kwa manufaa ya wananchi na watumishi wa afya.
serikali inakotupeleka siko tunakotaka kwenda japo tunaweza kwenda, tukiungana madaktari kwa uchache wetu tuna weza kuuza huduma kwa wananchi kwa gharama kubwa ambazo wananchi wengi hawataweza kuzimudu. mmesikia Mh rais akijivunia kujengwa kwa hosipitali ya moyo, figo, etc, haya yote yamewzekana kwa utayari wetu wakuishauri serikali na wakati huo huo kujitoa kusoma kwa muda mrefu ili huduma hizi ziwafikie watanzania wote na kwa gharama rafiki kwa watu wote.