Madaktari mkisalimu amri sasa mmekwisha; mtawahukumu wanaokuja nyuma yenu

hivi polisi na madaktari nani ana mshahara mzuri mazingira bora ya kazi??je polisi wakigoma??..ninyi dr's ubinafsi umewazidi kati ya madia 12, 11 ni madai yenu binafsi ya posho na mishahara... moja tu ndo uboreshaji wa huduma za afya.. hivi mnafikiri uboreshaji wa afya ni wa siku moja?? kwa hiyo mtaendelea kugoma hadi wodi za wazazi,watoto zijengwe ndo mrudi kazini???? hivi ninyi wasome kweli au wanasiasa?????.... KAMA HAMJUI KWA SASA TUMEWASHATOA THAMANI KWANI MNAAJENDA YENU NYUMA KATIKA MGOMO HUU.
 
Madaktari waongozwe na kumjali mgonjwa
Jambo hili llina mitazamo tofauti; je madaktari kurudi kwenye mazingira yale yale mabovu, bajeti finyu na mfumo mbaya wa utendaji kazi ambapo wamejikuta wakishindwa kutoa huduma inayostahili kwa wagonjwa kutafanya hali hiyo ibadilike kwa vile "madaktari wamerudi kazini"? Je kurudi katika mazingira yale yale (CT Scans hakuna, vipimo hadi hospitali binafsi, vitendea kazi hakuna au duni) kutaokoa maisha ya wananchi wetu? Je, hata wakati hakuna mgomo wananchi walikuwa salama mikononi mwa madaktari ambao wamechoka, hawana vitendea kazi na ambao wako kwenye mazingira magumu?

Wengine watasema "warudi tu"; sawa lakiniw arudi wakiwa wamebadilisha nini? Hivyo, mgomo huu kufanikiwa kwake ni lazima kuwe ni kubadilika kwa namna wanavyofanya kazi. Kwa mfano, waseme kuwa wanahitaji kuwe na "minimum standard" ya utendaji kazi wa hospiali. Kwamba, hospitali ya serikali ili ifanye kazi ni lazima iwe na vitu hivi na vikiwa vinafanya kazi:

X-Rays
Single Use Gloves
CT Scan/MRI within 100 miles na kwa hospitali za rufaa ni lazima ziwe na CT Scan inayofanya kazi;
Idadi ya wauguzi na waganga wasaidizi
n.k

Serikali ikikubali kama mambo haya basi madaktari wataweza kurudi kazini hata kama maslahi yao binafsi yanaweza yasiboreshwe kwa wakati huu; lakini kutaka tu warudi ilimradi warudi ni kuhukumu wagonjwa kwenye mikono isiyoweza kuokoa maisha yao hata kama akili na nia ipo.

HIvyo basi... wanavyofikiria kuamua kurudi au kuendelea na mgomo ni muhimu waangalie picha nzima ambayo ni zaidi ya wao!

Nakubaliana na pointi yako hapo juu, cha msingi kwenye huu mgomo anaeteseka sana ni wananchi wa hali duni, na sizungumzii sisi hapa JF maana humu tayari watu wote hali yao ni juu ya mtanzania wa kawaida. Kwa maana kwamba aidha watu humu JF wapo nje ya nchi au wana uwezo wa kuwa na kompyuta au simu ya bei mbaya kuchat. Mwananchi anyetegemea sana huduma ya hospitali ya serikali hana huo uwezo na mgomo huu hivi tunavyoongea tayari wananchi kadhaa wamepoteza maisha yao.

Matakwa ya madaktari ni halali hamna mtu anyepinga suala hapa ni jinsi gani ya kufikia hilo lengo. Kwa kuanzia tuangalie hali ya hospitali zetu zilivyokua nyuma na hapa zilipo je kuna maendeleo yeyote, je serikali inafanya juhudi za makusudi kwa kadri ya uwezo wake kuboresha mazingira ya kazi na huduma kwa ujumla kwenye sekta nzima ya afya?

Je bajeti ya afya ikoje kulinganisha na sekta nyingine hapa nchini?

Swala la vitendea kazi vibovu lipo kwenye sekta zote hapa nchini kuanzia elimu, afya, ulinzi, mahakama kila mahali labda tu kwa viongozi wa juu na hata huku utendaji wake bado haufai wote tunalijua hilo.

Ni lazima tuangalie mambo kwa upana zaidi na uwezo tulionao, serikali yetu kuweka vifaa vya kisasa hospitali zote kuu za nchi kwa sasa sidhani kama inaweza, na hata hivyo hatuna wataalam wa kutosha kuendesha hiyo mitambo yote kama unavyo suggest hapo juu. Tanzania bado tuna rate ndogo sana hata kwa standard ya afrika kati ya dokta na idadi ya watu.

Nilitoa ushauri hapo mwanzo kuwa suala la posho kwa watumishi wote wa umma liwe nje ya serikali kuu na kiundwe chombo kushughulikia hilo kwa watumishi wote wa umma. Pili suala la malipo, sisi wengine kwenye ajira zetu unaposaini mkataba unajua kiasi na kukubali malipo hayo na hatuna huo uwezo wa kugoma. Kwani madokta walipoanza kazi walikuwa hawajui mshahara wao uko chini na vitendea kazi duni kama watz wengine kibao? au wameshtukia hilo sasa maana hata polisi, mahakimu, walimu, mamesenja, na sisi wengine wote watz tunajua tangu mwanzo kuwa mishahara na mazingira ya kazi hapa kwetu kwa kweli si mizuri hilo si jipya.

Narudia tena nawasihi madaktari warudi kazini kuokoa maisha ya watanzania wenzetu ambao hawana uwezo wa kutibiwa hospitali binafsi wala nje ya nchi hao ndio victim namba moja ya huu mgogoro, kumbukeni hilo.
 
tusubiri tuone tamko lao baada ya kikao chao hiyo kesho!lijalo kubwa kuliko liishalo!
 
Mgomo wa madaktari unakuwa mgumu zaidi kwa kuwa MTANZANIA wa kawaida hauelewi. Anadhani madaktari wanamgomea yeye. Rais na watu wake hawawezi kukosa huduma ya matibabu. Madaktari pia hawawezi kukosa huduma ya matibabu kama tulivyoona kwa Dr Ulimboka.
Hakuna mgomo nchi hii utakaofanikiwa bila MTANZANIA wa kawaida kuuelewa, kuukubali na kuunga mkono.
 
Warudi tu kazini. Lakini wait! Si watanzania wataendelea kufa kwa kukosa huduma? What is the point ya mgomo. Wananchi kwaninni kwa pamoja tusimwambie mkuu kuwa hiyo approach ya vitisho ni mauaji kwa raia. Wanaharakati wamesma sana lakini ghafla wamwekuwa drifted awy na swala la kutekwa na kuteswa kwa dk. Ulimboka. Let them come back to the primary source na kumweleza mkuu aangalie upya anavyowatenda raia wake wanyonge ambao hata kusoma tu tabu lakini walikubali kushikwa mkono kuelekezwa ilipo picha ya mkuu il wampigie kura. Hao ndo wanakufa wachache ajanja wataka-survive wameshachoshwa na propaganda!
 
Mgomo wa madaktari unakuwa mgumu zaidi kwa kuwa MTANZANIA wa kawaida hauelewi. Anadhani madaktari wanamgomea yeye. Rais na watu wake hawawezi kukosa huduma ya matibabu. Madaktari pia hawawezi kukosa huduma ya matibabu kama tulivyoona kwa Dr Ulimboka.
Hakuna mgomo nchi hii utakaofanikiwa bila MTANZANIA wa kawaida kuuelewa, kuukubali na kuunga mkono.

Ndicho ambacho mlikuwa hamjui mgomo ulivyoanza dharura zote zilikuwa zinaonwa na ile ya dr ulimboka pia ilikuwa ni dharura pia na ndio maana alipata huduma kama ambavyo wengine walikuwa wakipata huduma ya dharura ila baada ya lile tukio na kujaribu kumuua kushindikana na kufichuka madr ndio walipata hasira na nadhani hata hizi dharura sasa zinaendelea kusuasua zaidi...hivyo ndugu ulipotoka
 
mzee mwanakijiji nakupongeza kwa makala yako nzuri, nimeisoma kwa kina nakuielewa, kwa wenzetu waliozoea ku copy n ku pest kwao bado ni ngumu kuelewa, ukweli ni kuwa THE LAW IS BLIND! IT CANT SEE AND WORSE ENOUGH IT CANT MAKE ITS OWN DECISION INSTEAD IT DEPENDS ON THE MINDS OF THE ONE WHO OWN IT!

madakatari tumeliona hilo, 2najua kamwe hamna mgomo halali, isipokuwa tu mgomo wa hiari kwa waumini wanpogoma kula na kunywa kumuomba Mungu kuwasamehe, kuwabariki etc.

inapokuja swala la jambo nyeti kama hili la madakatri kugoma watawala wakatumia nguvu kubwa kutafuta majibu rahisi badala yakutafuta mbinu thabiti zakuutatua inaonyesha unyonge wa fikra za watawala, napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa, mbinu zakung'oana meno na kucha kwa koleo zilitumiwa na wakoloni na kwa kuwa mifumo yetu ni muendelezo wa pale wakoloni walipo achia ndiyo waona wanatumia mbinu kama hii.

Rais Kagame jana akihutubia taifa na Mh rais wetu akiwepo alikemea tabia ya viongozi wakiafrika ku google majibu ya matatizo yao badala yakutumia bongo zao. Inashangaza viongozi wanapotulazimisha kuona rangi nyeusi kuwa nyeupe, wantamani kujua ni nani anafadhili mgomo wa madaktari na hawatamani kuona wala kusikia mahitaji halisi ya watumishi wa afya na wananchi kwa upana wake. ukweli ni kuwa hakuna anayefadhili mgomo wa madaktari kwa fedha, mawazo, au aina yoyote ya msaada. Madaktari tunao uwezo wakufikiri na kuamua bila kutumiwa na mtu na zaidi hatuna nia yoyote yakuichafua serikali kwa kuwa hatuwezi kukata tawi tulilokalia.

Ndugu zangu kwa hakika sisi tulio katika fani hii tumeona mengi sana, iadadi ya wagonjwa wanaokufa kwa kukosa vifaa tiba na madawa ya gharama nafuu ni kubwa sana na kibaya zaidi wanapokufa ndugu huishia kulia kidogo nakusahau mpaka atakapokufa mwingine ila kwetu tunaona mambo hayo kila iitwapo leo.

nina kubali kabisa kuwa kiapo cha watumishi wa afya hakiruhusu mtu kugoma ila kina mtaka mtoa huduma ya afya kuweka mbele haki ya uhai wa mgonjwa kwa gharama yoyote ile, na hiki ndicho tunachikifanya, kuiambia serikali ya kuwa tunataka mabadiliko katika sekta ya afya, kwa upana wake.

wanaosema madaktari ni watu wenye ubinafsi na wanaotamani kuishi maisha yakiteule siyo kweli , kinachotusukuma ni kutaka kuona sekta ya afya inapewa kipaumbele kinacho stahili, tuna omba umma wa Watanzania wajue kuwa hatuna nia yakutaka wao wapunguziwe maslahi tupewe sisi la hasha tunaamini kila mtumishi wa umma anapaswa kupewa maslahi yanayolingana na mahitaji yake na kulingana na vigezo vilivyopo na uhalisia wa maisha.

Niwakumbushe tu ya kuwa serikali hii hapo mwaka 1998 ilifanya upembuzi yakinifu kuangalia ni viwango gani vya mishahara kitakacho stahili kulipwa kila mtumishi wa umma kwa vigezo vilivyo ainishwa na ripoti hiyo na mapendekezo yake yapo mezani kwa ofisi ya utumishi, nawasihi kila mmoja pale alipo aitafute aisome aone mwaka 1998 alipaswa lipwa shilingi ngapi kwa ugumu wa maisha ya wakati ule kisha aone kwa sasa atastahili kulipwa kiasi gani.

siyo hilo tu pia kuna miongozo na taratibu za kazi baada ya muda wa kawaida wa kazi, safari za kikazi na kadhalika , ni vyema pia wakazisoma waelewe haki zao,badala yakusikia mambo yanayoelezwa kwa umahiri na mwajiri tu bila kumpa mwajiriwa fursa yakueleza upande wake.

nina wasihii Watanzania wenzangu hasa madakari (MD) assistant Medical officers (AMO) clinical Officers (CO) na watendaji wengine wote wa sekta ya afya tuungane pamoja kudai kuboreshwa kwa sekta ya afya kwa manufaa ya wananchi na watumishi wa afya.

serikali inakotupeleka siko tunakotaka kwenda japo tunaweza kwenda, tukiungana madaktari kwa uchache wetu tuna weza kuuza huduma kwa wananchi kwa gharama kubwa ambazo wananchi wengi hawataweza kuzimudu. mmesikia Mh rais akijivunia kujengwa kwa hosipitali ya moyo, figo, etc, haya yote yamewzekana kwa utayari wetu wakuishauri serikali na wakati huo huo kujitoa kusoma kwa muda mrefu ili huduma hizi ziwafikie watanzania wote na kwa gharama rafiki kwa watu wote.
 
Any body can easily be a cop in Tanzania.
After all, you need to fail most of your classes in O level in order to qualify to be a cop.
As far as you don't arrest real criminals! Your job is safe.

Who can not be a Police in Tanzania?

Ndugu Madilu wa Madilu. Nadhani unachotaka kutuambia ni kwmba wewe tu ndiyo huwezi kuwa cop. Hata Marekani inchukuwa wakimbizi na kuwafanya ucops isipokuwa wewe tu. Mwajiri anaouwezo wa kumuonea mwajiriwa na Mwaliriwa anouwezo wa kumuonea Mwajiri na hili ni hasa kwa wafanyakazi wa serikali. Cha msingi toa utatuzi unaoeleweka na siyo kukashifu utaalamu wa wenzio. Madaktari wamegoma mara ngapi na hamna suluhisho? unadhani kugoma ni just kuweka zana chini na kupita wodini kuwasanifu wagonjwa? Unadhani kuweka zana chini kuna tofauti gani na kumwona mgonjwa na kumwachia nurse while unaenda kwenye maduka yako ya dawa, hosipital binafsi kwa part time wala muajiri hakuangalii ni muda gani unaenda kwenye shughuli hizo.

Mimi ninachoweza kusema ni kwamba mgomo wa madaktari hautakuwa na mafanikio yoyote kwa madaktari kama wengi wanavyofikiria. Walivyogoma awali wakarudi kazini ilikuwa ndiyo wameshaloba step. Hivyo kwa sasa nawaasa warudi tu kazini wajipange upya. Watafute new strategies zinazoendana na specific goals la sivyo wakuwa wanatumia siasa kupambana na wanasiasa. Na cha Msingi watafute mzee mwenye busara awatangulie maana ukweli sisi vijana busara kidogo sana na utashi ndiyo kabisaa hatuna
 
Mkuu Mwanakijiji hayo matatizo hayawezi kumalizwa kwa siku moja; yanahitaji bajeti, yanahitaji sera ya afya kubadilishwa, yanahitaji majadiliano na kuhusisha wadau, nk.

Hivi tumejiuliza bajeti ya afya ya mwaka huu inayoenda kusomwa bungeni ina nini ndani yake katika ku address matakwa ya madaktari? Kwa nini ndugu zetu madaktari wasingesubiri kuiona na kuisikia budget inasemaje?

Ndugu Mwanakijiji katika mgomo huu anayeumia ni mwananchi wa kawaida kabisa wa Tanzania yetu hivyo basi Madaktari wakirudi kazini atayekuwa ameshinda ni huyu common mwananchi na siyo serikali. Wakirudi watakuwa hawajashindwa chochote bali watakuwa wameshinda katika kuyaokoa maisha ya watanzania masikini ambao wengi wanakufa kwa malaria mna homa za matumbo. wengi wanakufa kwa minyoo ambayo inapimwa na darubini ya kawaida; wale wanaotaka vipimo complicated huwa tunawasikia wakiwa wamefia ama Uingereza, India ama Afrika kusini au hata Nairobi. Tuwaonee huruma watanzania hawa wanyonge.

Mkuu bajeti ya kuwezesha madai ya daktari ipo ya kutosha tu. Kama Serikali itaamua kututoa misamaha ya kodi ambayo ni zaidi ya Shilingi 1.04 Trillioni kwa mwaka, kuhakikisha utajiri mkubwa wa mali asili nchini mwetu (Dhahabu, Uranium, Almasi, Tanzanite, Gas) unatumika kwa maslahi ya nchi yetu, kukomesha kabisa ufisadi wa mabilioni ya pesa miaka nenda miaka rudi kwa kuwashughulikia ipasavyo mafisadi kwa kutumia sheria za nchi basi ile kauli ya DHAIFU kwamba "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" itakuwa kweli. Ila tukiendelea kuamini ngojera za Serikali hii DHAIFU "kwamba nchi yetu ni maskini" "Serikali haina uwezo" basi hata miaka 50 mingine ijayo nhi yetu itazidi kuwa na hali mbaya kiuchumi na wajanja wachache ndani ya Serikali wakiendelea kuifaidi cake ya Taifa huku asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi maisha ya yaliyojaa ufukara wa kutisha.
 
Ni kweli MKJJ. Tatizo la serikali ya JK ni wachonganishi. Wanachonganisha wananchi na Dr's. Sasa hivi mimi nawahurumia sana Drs kwani wananchi wamewatukana na kuwadharau kwa hizi propaganda za kisiasa. Swali langu hivi huu uhasama wa wananchi/serikali na Dr's utakuja kuisha lini? Je Drs wanajisikiaje watu wanapowatukana na wakati huohuo ndiyo watakao kuja "Dr, nakufa, nakufa". Mi nilionelea wananchi tungeungana na Dr's ktk kuwasaidia hili, kwani ninavyojua in long run serikali wanataka sector ya afya upande wa serikali iwe zoofu na upande wa private uimarike ili capitalist wapate faida kubwa. Na hili wananchi leo hatuwezi kuliona. Lakini kama hali ikiachwa hivihivi basi mjue Dr akimaliza anaenda nje ya nchi au anakwenda private, na serikalini zitaendelea huduma mbovu na wasio kuwa na hela (masikini wanaowatukana Dr's) watakufa. Wananchi muache ujinga wa kuwatukana Dr's. Kauli yenu kwa pamoja semeni "Dr's tunawaomba mrudi kazini" that is all. Na siyo kujifanya kuwatunishia misuli kama vile na nyinyi ni Dr's.
 
Madaktari wameamua Kurudi kazini haya wale mlokua mkipenda wagome haya tupeni maoni yenu
 
Mzee Mwanakijiji na wanaforum wenzangu
Binafsi nimeshangazwa na majibu ya raisi juu ya huu mgogoro na akionyesha wazi kuwa serikali yake haikuwahi kufikiria kuutatua hata mara moja.amekuwa bingwa wa kukokotoa takwimu za miaka ambazo kama umri uongezekavyo nazo pia huongezeka kutokana namabadiliko ya bei za bidhaa nagharama za kimaisha

Serikali fanisi ingekaa na wataalamu wetu hawa hata kama sio kuwaongezea kwa percent waliyotaka japo wangejipigapiga na kusema wanaweza kuongeza hadi mahala fulani..na zile posho pia wakatoa offer yao kwa mtindo wa kugawanyisha fungu dogo litakaloongezwa
Vifaa vya kazi hasa vya kiuchunguzi kama CT Scan,X-Ray,Ultra Sound,Gloves nk vingekuwa ni kipaumbele katika kila Hospitali na vituo vya afya vya serikali.yaani iwe ni sharti la muhimu kutimia ili mahali hapo paitwe Hospitali

wauguzi pia wangetazamwa kwa jicho la pili ili daktari aweze kufanya kazi kifanisi
Kukimbilia kununua mashangingi ya 280 million na maBMW ya ikulu hakutusaidii kamwe.pesa ipo ikipangiliwa vizuri haya yote yanawezekana na si kwa madaktari tu bali hata walimu,askari na kada nyingine

wananchi nao wanajisahau na kulaumu bure hawajui kuwa yakiboreshwa hayo na wao watakuwa na nafuu na mazuri ya kutibiwa na kupona kiusahihi na kiuharaka na sio kuwaonea wivu wanaowatibia

Ongeza mshahar,ongeza posho,nunua vifaa,boresha wauguzi,badili mfumo mbovu wa MSD katika kutoa vifaa na madawa

Na mwisho wizara ya afya isiwaingilie wahisani wanapotoa misaada kwa kutaka wapewe direct funds kwani zinaishia matumboni mwao,waache wahisani wafadhili miradi,wajenge vituo wao wasubiri kukabidhiwa ikiwa haijachakachuliwa
 
Mzee Mwanakijiji.
Kupanga ni kuchagua pitia vizuri hayo madai ya Madaktari wetu yapo madai 12 kwenye hayo madai 12 dai 1 moja tu ndio wanataka waboreshewe mazingira ya kazi yao lakini madai 11 yaliyobaki ni maslahi yao binafsi...nadhani hapa hakuna cha kusalimu amri muajiri wao ambaye ni serikali hana uwezo wa kulipa mshahara huo, kupanga ni kuchaguwa wameambiwa kama wanaona mshahara ni mdogo ruksa kutafuta sehemu nzuri yenye maslahi mazuri wanalipa vizuri sehemu ingine.

Nimekuwa nikisema siku zote kwamba sina heshima kwa mtu yeyote anayetumia kuaminiwa na kuheshimiwa kwake kupotosha watu, tena kwa makusudi. Mwanakijiji ni kati ya hao wanao-abuse heshima hii. Kwa vile wewe uko nje na huoni maafa yanayotokea kwa wananchi wetu maskini basi unadhani hili ni jambo la kichekesho ambalo linawza kuingizwa siasa za vyama.

Mwanakijiji ni mtu mwenye phobia ya hali ya juu sana dhidi ya Kikwete, lakini elewa kwamba hapa anayeumia si Kikwete, ni wananchi maskini ambao kodi zao ndizo zimekuwanzikiwasomesha na kuwalisha wasaliti hawa. Mwanakijiji anajua kwamba hakuna uchumi wa nchi changa unaoweza ku-accommodate malipo outrageous kama haya ya hawa wasaliti. Kama tunayoambiwa kwamba kuna mkono wa watu ili nchi isitawalike ni kweli, basi naamini Mwanakijiji ni miongoni mwa wapanga mpango huo, alongside wale wenzao wa Chadema ambao wanajifanya kutetea maslahi huku wakiacha mtaji wao na mshine zao za kura zikiteketea.

Ndiyo hao waliochanga kumtibu Ulimboka wakisahau maskini wasio na uwezo wala ndugu wa kulipia matibabu yao. Mwanakijiji ni bad news na ufike wakati apuuzwe kwa tabia yake ya kupinga kila kitu na kupotosha watu. By the way, naendelea kupongeza mkong'oto wa Ulimboka maana anajua sasa maana ya kuugua!
 
Huyu mjomba kama ameshindwa kuishirikisha akili na kutafuta wataalamu wa mambo ya utawala si akae tu pembeni kwa kujilindia heshima.****** alizani magogoni watu wanacheza ngoma kule dah........Sio kwamba ni kweli inji haina pesa ila tatizo haina mpangilio mzuri wa matumizi ya keki ya taifa....Halafu hizi mbwembwe zake za kuwaambia kama hamtaki kazi acheni hii kauli tunamuonya asije akaona kama anaongea na wapumbavu wenzake huko ajue anaongea na watu makini na wanaozijua haki na thamanizao kitaifa sio kienyeji enyeji tu eti kama hutaki acha kazi pumbaafu,hata siku moja haliwezi kuwa kosa kwa kudai stahiki zako pale unapoona unastahili bila kuogopa hizo sheria zao kandamizi. Kimsingi kurudi madactari kazini bila kuonyesha kusikiliza na hata kuonyesha kuzipa nafasi hata zile kero zinazozalisha tatizo ni nini sasa hii kama sio kufanya masihara na wanainji wako ? Anyway tunajua wewe ni freemason na yaweza kua unanufaika na damu hizi za watu wanaopoteza maisha lakini hadi leo bado tu hazijatosha? Ma doctor kwa pamoja umoja wenu ndio siraha yenu hakuna kurudi nyuma na kama kuwafukuza wawafukuze ninyi nyote kama wanaubavu huo.Get well soon Dr.Ulimboka.
 
Na serekali mkisalimu amri sasa mmekwisha; mtawahukumu wanaokuja nyuma yenu!

Tena utakuwa ni usaliti wa hali ya juu kwa walipa kodi wa nchi hii ambao ndiyo wanaoiendesha serikali na kuhudumia maisha ya wasaliti hawa, ambao wao wenyewe kwa kujua hawana uwezo, wamemsalimisha mwenzao Ulimboka kwa wajuzi wa mambo ili wao wabaki kukamua majipu, kufanya tohara na kutoa kimba wanafunzi.
 
I dont get it!! Why do people keep saying "watu wengi wameshapoteza maisha"? Kwani kabla ya mgomo wa madaktari walikuwa hawapotezi maisha due to lack of hospital resources? Sifurahii huu mgomo wa madaktari hata kidogo lakini hebu tusisahau kuwa ni kweli serikali yetu at some point haijali hospitali zetu. Ni hospitali ngapi huko vijijini ambazo hazina umeme au hazijawahi kuwa na umeme? Hospitali moja ya huko Shinyanga vijijini (kama sikosei) imekatiwa umeme kwa miezi saba sasa na wagonjwa wote wanaoenda kutibiwa usiku wakiwemo kina mama wajawazito lazima watoe shs 1,200 kwa ajili ya mafuta ya taa ya kuweka kwenye chemli za hospitali, dont u think that's insane? Sidhani kama serikali inashindwa kuweka umeme, x-ray na ultra sound machines kwenye kila hospitali, inaweza, sasa kwa nini haiweki? Watawezaje kuboresha hospitali za vijijini kama za mjini zinawashinda? Imagine, you have studied for 5years as a Medical doctor, 4 more years as a specialist only to come and see patients that you are suppose to save dying right infront you because of lack of resources while the government spend thousands of cash kwenye sherehe za miaka hamsini ya Uhuru!!! Theatre ya Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi imefungwa tangu 2010 kwa sababu haikuwa na kiwango cha kutosha, sawa nakubali lakini kwa nini mpaka leo haijafunguliwa?? Kitu kikiharibika tena kitu cha muhimu hivyo si unakitengeneza ili kifikie kiwango unachotaka? Sasa kwa nini mpaka leo imefungwa? Serikali inatakiwa kujua jinsi ya ku-prioritize mambo yake, na nadhani in this case Hospitals should be given the first priority because whether there is mgomo or not, watu bado wataendelea kupoteza maisha, especially in rural areas!!
 
I dont get it!! Why do people keep saying "watu wengi wameshapoteza maisha"? Kwani kabla ya mgomo wa madaktari walikuwa hawapotezi maisha due to lack of hospital resources? Sifurahii huu mgomo wa madaktari hata kidogo lakini hebu tusisahau kuwa ni kweli serikali yetu at some point haijali hospitali zetu. Ni hospitali ngapi huko vijijini ambazo hazina umeme au hazijawahi kuwa na umeme? Hospitali moja ya huko Shinyanga vijijini (kama sikosei) imekatiwa umeme kwa miezi saba sasa na wagonjwa wote wanaoenda kutibiwa usiku wakiwemo kina mama wajawazito lazima watoe shs 1,200 kwa ajili ya mafuta ya taa ya kuweka kwenye chemli za hospitali, dont u think that's insane? Sidhani kama serikali inashindwa kuweka umeme, x-ray na ultra sound machines kwenye kila hospitali, inaweza, sasa kwa nini haiweki? Watawezaje kuboresha hospitali za vijijini kama za mjini zinawashinda? Imagine, you have studied for 5years as a Medical doctor, 4 more years as a specialist only to come and see patients that you are suppose to save dying right infront you because of lack of resources while the government spend thousands of cash kwenye sherehe za miaka hamsini ya Uhuru!!! Theatre ya Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi imefungwa tangu 2010 kwa sababu haikuwa na kiwango cha kutosha, sawa nakubali lakini kwa nini mpaka leo haijafunguliwa?? Kitu kikiharibika tena kitu cha muhimu hivyo si unakitengeneza ili kifikie kiwango unachotaka? Sasa kwa nini mpaka leo imefungwa? Serikali inatakiwa kujua jinsi ya ku-prioritize mambo yake, na nadhani in this case Hospitals should be given the first priority because whether there is mgomo or not, watu bado wataendelea kupoteza maisha, especially in rural areas!!
Madaktari kama kweli wangekua wanajali maisha ya watanzania katika ile orodha yao wasingeweka madai 11 ya kwao na moja ndio hilo unaongelea hapa. Kiukweli hoja yao ingekua na mshiko kama wangesimama na hoja kama MMM aliivyoitabainisha hapa na watanzania tungewaelewa

Wengine watasema "warudi tu"; sawa lakiniw arudi wakiwa wamebadilisha nini? Hivyo, mgomo huu kufanikiwa kwake ni lazima kuwe ni kubadilika kwa namna wanavyofanya kazi. Kwa mfano, waseme kuwa wanahitaji kuwe na "minimum standard" ya utendaji kazi wa hospiali. Kwamba, hospitali ya serikali ili ifanye kazi ni lazima iwe na vitu hivi na vikiwa vinafanya kazi:

X-Rays
Single Use Gloves
CT Scan/MRI within 100 miles na kwa hospitali za rufaa ni lazima ziwe na CT Scan inayofanya kazi;
Idadi ya wauguzi na waganga wasaidizi
n.k

Serikali ikikubali kama mambo haya basi madaktari wataweza kurudi kazini hata kama maslahi yao binafsi yanaweza yasiboreshwe kwa wakati huu; lakini kutaka tu warudi ilimradi warudi ni kuhukumu wagonjwa kwenye mikono isiyoweza kuokoa maisha yao hata kama akili na nia ipo.

HIvyo basi... wanavyofikiria kuamua kurudi au kuendelea na mgomo ni muhimu waangalie picha nzima ambayo ni zaidi ya wao!
 
Back
Top Bottom