Madaktari mkisalimu amri sasa mmekwisha; mtawahukumu wanaokuja nyuma yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari mkisalimu amri sasa mmekwisha; mtawahukumu wanaokuja nyuma yenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 2, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo kadhaa ambayo ningependa kuyatolea maoni kwa namna tofauti kwani tangu siku ile ya Jumatano usiku sijapata muda wa kutulia kuweza kuweka mawazo yangu juu ya yanayotokea. Baada ya kusoma (na kusikiliza kidogo hotuba ya Rais) nimejikuta sina mengi ya kusema ila kwamba madaktari wakikubali tu kurudi kazini wakati 'status quo' bado ipo basi wao wamejimaliza na kwa hakika watakuwa wameshindwa kutengeneza mazingira bora kwa madaktari wetu wanaokuja.

  Kikwete kafanya hili ni la "madaktari hawa"
  Mojawapo ya vitu ambavyo naamini vinaweza kuangaliwa kwa makosa ni kujifikiria madaktari hawa; kwamba madai yao ni madai ya wao peke yao; kwamba madai ya madaktari ni ya watu wa wakati huu au kizazi hiki tu. Kama - labda nitumie herufi kubwa hapa - KAMA madaktari wanaamini wanadai vitu ambavyo ni kwa ajili yao wao wenyewe tu na kwamba wanataka kujifurahisha au kufurahishwa wao tu kama madaktari wa sasa ili nao waonekane wanakula ile keki ya taifa basi NI LAZIMA warudi kazini bila masharti.

  LAKINI - kama kinachowaongoza ni kufikiria mazingira ya sekta ya afya na maslahi ya wahudumu wake wa sasa na wa kizazi kijacho basi kurudi mara moja kazini (kumaliza mgomo) kutakuwa ni kosa kubwa ambalo japo litawahakikishia wao chakula na malazi na kutuliza munkari wa wanasiasa kwa hakika litakuwa ni jambo la kuja tena kushughulikia na vizazi vijavyo vya madaktari.

  Binafsi ninaamini hili siyo suala la madai ya "madaktari hawa" tu bali ni suala la sekta nzima na madaktari wanaokuja nyuma yao. Kwa mbali hili linaonekana kwenye madai ya madaktari "wanafunzi" ambao leo hii tunaweza kuona kutoka mbali kuwa watakuja kuongoza mgomo mwingine. Hivi Ulimboka na wenzake kwani wameanza juzi? Si walianza tangu wakiwa wanafunzi wa udaktari? Wakati kina Ulimboka wakiwa shule na walipokwarizana na watawala wakaahirisha lakini likaja kutokea tena mapema mwaka huu na sasa na kwa hakika bila kulimaliza inavyopaswa hili litatokea tena.

  Uhalali wa mgomo wa madaktari hautokani na sheria
  Mojawapo ya mambo ambayo yanahitaji kufikiria ni kuwa je sheria yaweza kutumika kuwakandamiza watu? Je mara zote sheria inapaswa kutiiwa hata kama inakandamiza jamii au kundi la watu? Wana filosofia na wanaharakati duniani wanatambua kuwa sheria ikiandikwa ili kukandamiza watu basi watu wana haki (inayotokana na ukuu wa dhamira zao) kutoitii sheria hiyo. Madaktari inawezekana kabisa wanagoma bila kufuata sheria lakini itakuwaje kama wamegundfua kwamba sheria iliyopo inawakandamiza? Je waitii tu? Sheria kandamizi na dhalimu haipaswi kutiiwa. Hili ni somo toka Afrika ya Kusini, India, Marekani na nchi nyingine ambapo watu wametambua kuwa watawala hutumia "sheria" kukandamiza watu.

  Serikali ilipitisha sheria ambazo zimekuwa ni kandamizi kwa haki za wafanyakazi. Sheria zimejengwa ili kuwalinda watawala wasisumbuliwe na watawaliwa. NI sawasawa na kundi la ng'ombe kutengeneza sheria za kudhibiti nyangenyange wasitue migongoni mwao. Tumeliona hili hata kwenye suala la maandamano ya kisiasa ambapo sheria zimeundwa ili kuzuia maandamano ya kisiasa (japo wenyewe wanasema kwa ajili ya kulinda amani na utulivu!).

  Wameshavunja sheria kwa kusimamia maslahi yao; hawawezi kuvunja zaidi!
  Kama maneno ya RAis Kikwete ni ya kweli (nami naamini ni ya kweli) kwamba mgomo huu hauna uhalali kwa mtazamo wa sheria iliyopo basi madaktari tayari wameshavunja sheria. Na kuwa tayari hatua zimeshaanza kuchukuliwa dhidi yao ni uthibitisho kuwa serikali inaamini mgomo huu ni haramu. Sasa kama hili ni kweli hivyo madaktari wakiendelea kugoma wanajidhuru nini zaidi ya vile ambavyo wameshajidhuru? Tayari wako kwenye mgomo "haramu" sasa kuendelea kugoma hakuufani mgomo huo kuwa "haramu zaidi"! Kwa msingi huo kusitisha mgomo na kurudi kazini bila suluhisho la mezani kunasaliti msimamo wao wote.

  Madaktari wasijifikirie wao wenyewe kwani wataogopa
  Madaktari wakiamua kujifikiria wao wenyewe wataogopa; wataogopa kwa sababu kama yameweza kumtokea Ulimboka yanaweza kumtokea mtu mwingine yeyote kati yao. Je itakuwaje kama watapoteza ajira zao (na hili JK kaliashiria)? watoto wao watakula wapi? Je zile nyumba wanazoishi itakuwaje? Sasa hapa ndio kuna tofauti ya wale wenye kuamini wanachosimamia na wale wanaofuata mkumbo. Kama wanaamini wako sahihi kudai maslahi ambayo siyo tu yatanufaisha wao bali pia madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta hiyo huko mbeleni basi msimamo kwao ni: Kuendelea na mgomo.

  Serikali inaweza kumaliza mgomo ndani ya masaa 24 bila kumfukuza daktari hata mmoja
  Kama nilivyosema wakati ule (Machi) nguvu ya kumaliza mgomo huu iko ndani ya serikali siyo madaktari. Serikali ndiyo inatunga sera, sheria na kupanga bajeti ya sekta hiyo. TAyari tunajua sera yao ya afya ni mbovu imaeshindwa na sheria zake zinaonekana zina matatizo na kama ni bajeti ni hafifu mno na tegemezi. Kama haya yote ni kweli basi changamoto iko kwa serikali kukaa chini na kufikiria wafanye nini kukidhi madai ya madaktari? Binafsi nina pendekezo langu lakini nitaangalia suala hili linaenda vipi.

  Madaktari walisharudishwa kazini mara moja baada ya kikombe cha chai Ikulu. Safari hii hakuna cha chai wala juisi ya machungwa; Je watarudi? Baada ya tukio la Ulimboka...?

  Madaktari waongozwe na kumjali mgonjwa
  Jambo hili llina mitazamo tofauti; je madaktari kurudi kwenye mazingira yale yale mabovu, bajeti finyu na mfumo mbaya wa utendaji kazi ambapo wamejikuta wakishindwa kutoa huduma inayostahili kwa wagonjwa kutafanya hali hiyo ibadilike kwa vile "madaktari wamerudi kazini"? Je kurudi katika mazingira yale yale (CT Scans hakuna, vipimo hadi hospitali binafsi, vitendea kazi hakuna au duni) kutaokoa maisha ya wananchi wetu? Je, hata wakati hakuna mgomo wananchi walikuwa salama mikononi mwa madaktari ambao wamechoka, hawana vitendea kazi na ambao wako kwenye mazingira magumu?

  Wengine watasema "warudi tu"; sawa lakiniw arudi wakiwa wamebadilisha nini? Hivyo, mgomo huu kufanikiwa kwake ni lazima kuwe ni kubadilika kwa namna wanavyofanya kazi. Kwa mfano, waseme kuwa wanahitaji kuwe na "minimum standard" ya utendaji kazi wa hospiali. Kwamba, hospitali ya serikali ili ifanye kazi ni lazima iwe na vitu hivi na vikiwa vinafanya kazi:

  X-Rays
  Single Use Gloves
  CT Scan/MRI within 100 miles na kwa hospitali za rufaa ni lazima ziwe na CT Scan inayofanya kazi;
  Idadi ya wauguzi na waganga wasaidizi
  n.k

  Serikali ikikubali kama mambo haya basi madaktari wataweza kurudi kazini hata kama maslahi yao binafsi yanaweza yasiboreshwe kwa wakati huu; lakini kutaka tu warudi ilimradi warudi ni kuhukumu wagonjwa kwenye mikono isiyoweza kuokoa maisha yao hata kama akili na nia ipo.

  HIvyo basi... wanavyofikiria kuamua kurudi au kuendelea na mgomo ni muhimu waangalie picha nzima ambayo ni zaidi ya wao!
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,111
  Likes Received: 10,468
  Trophy Points: 280
  Shkamoo Mzee Mwanakijiji.
  Naswaki kwanza halafu narejea fasta hapa.
   
 3. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  Kwa hicho 'kijimtego' cha rais, hakika ndiyo tutaona nini madaktari wanachokisimamia.
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mi sahizi ndo namalizia dinner aina ya kande za mahindi mabichi, kande hizi zimenikumbusha kwetu kijiji cha Madilu kule Njombe.
  Mimi na mama yenu leo katika endesha endesha mkweche wetu tulipita sehemu fulani huko mashambani wenye wanaita YU PIKI tukachuma mahindi mabichi mapichezi,Strawberries na lubabu.
  Haya Ngoja kwanza niusome huu Mzalendo wa Mzee mwenzangu.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Do they take serious what the president says? Arrogance yetu na ubabe hasa kwa wafanyakazi wa ofisi kubwa za umma inaligharimu sana hili Taifa.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanakijiji hayo matatizo hayawezi kumalizwa kwa siku moja; yanahitaji bajeti, yanahitaji sera ya afya kubadilishwa, yanahitaji majadiliano na kuhusisha wadau, nk.

  Hivi tumejiuliza bajeti ya afya ya mwaka huu inayoenda kusomwa bungeni ina nini ndani yake katika ku address matakwa ya madaktari? Kwa nini ndugu zetu madaktari wasingesubiri kuiona na kuisikia budget inasemaje?

  Ndugu Mwanakijiji katika mgomo huu anayeumia ni mwananchi wa kawaida kabisa wa Tanzania yetu hivyo basi Madaktari wakirudi kazini atayekuwa ameshinda ni huyu common mwananchi na siyo serikali. Wakirudi watakuwa hawajashindwa chochote bali watakuwa wameshinda katika kuyaokoa maisha ya watanzania masikini ambao wengi wanakufa kwa malaria mna homa za matumbo. wengi wanakufa kwa minyoo ambayo inapimwa na darubini ya kawaida; wale wanaotaka vipimo complicated huwa tunawasikia wakiwa wamefia ama Uingereza, India ama Afrika kusini au hata Nairobi. Tuwaonee huruma watanzania hawa wanyonge.
   
 7. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  M/kijiji unanishangaza kujifanya hujui kuwa sheria zilitungwa kukandamiza watu, ule usemi wa sheria msumeno hujawahi isikia, na wale mawakili wanaotetea wahalifu si kwa mujibu wa sheria. Si sheria hizi hizi hutumika kumtoa hatiani mhalifu. Tuna mifano mingi ya sheria kandamizi si kwa mgomo huu tu bali kwa watoto wanaobakwa na kulawitiwa, sheria kandamizi kwa wanawake, mauaji ya albino, hili la madaktari wamejipalia wenyewe kujifikiria wao peke yao tupo wengi tunaohitaji maisha bora
   
 8. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Wakirudi wamekwisha
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji.
  Kupanga ni kuchagua pitia vizuri hayo madai ya Madaktari wetu yapo madai 12 kwenye hayo madai 12 dai 1 moja tu ndio wanataka waboreshewe mazingira ya kazi yao lakini madai 11 yaliyobaki ni maslahi yao binafsi...nadhani hapa hakuna cha kusalimu amri muajiri wao ambaye ni serikali hana uwezo wa kulipa mshahara huo, kupanga ni kuchaguwa wameambiwa kama wanaona mshahara ni mdogo ruksa kutafuta sehemu nzuri yenye maslahi mazuri wanalipa vizuri sehemu ingine.
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kumaliza mgomo ni sawa na mbwa aliemfukuza mwizi baada ya kutishiwa akageuka na kufyata mkia.
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Kudai huduma bora eti ni kujipalia mkaa? Ovyoo!@mnyampaa
   
 12. m

  msapwat Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  binafsi naamini mh.rais anaouwezo wa kutatua tatizo ila yupo katika harakati za utatuzi.au mnasemaje?
   
 13. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani wameingia ndani sana kutoka kama ulivyosema impact ya kurudi bila suluhisho la kudumu itakuwa kubwa na mbali ya yote the damage has already been done, watu wengi wamepoteza maisha na wanaendelea kupoteza maisha for this to go in vain. Tunachohitaji ni suluhisho la kudumu si bla bla na vitisho
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Serikali imewaeleza mgomo haukubaliki ,serikali kama muajiri mwengine yeyote yule anawalipa wafanyakazi wake kutokana na uwezo alionao serikali kwa waliyoyadai madaktari haina uwezo huo ,sasa hawa jamaa sielewi nikimaanisha madaktari ni kazi yao ipi isiyohitaji posho ??? Maana hiyo posho ni kwa kila stepu hata kutoka nyumbani kuelekea kazini basi atahitaji posho ,mmeona wapi ?

  Serikali imeweka wazi kutoka kwenye hotuba ya Mheshimiwa Raisi kuwa asie weza kufanya kazi kwa makubaliano na mishara iliyopo awe huru kuacha kazi na si vinginevyo hakuna haja ya malumbano malumbano ya nini na serikali imesema haina uwezo na hakuna kulazimishana. waache kazi na wakatafute kule watakapolipwa mshahara wanaoupanga wao madaktari , Jamani mshahara ni makubaliano ya awali kati ya muajiri na muajiriwa ,ila baada ya kuajiriwa unadai makubwa ni muajiri gani atakubali hayo ?
   
 15. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  A=excelent
  b=very good
  c=good
  d=average
  e=satisfactory
  s=weak (dhaifu)=jk
  f=poor
   
 16. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Serikali ya Kikwete inajaribu kutumia nguvu nyingi mno kuonyesha umma wa WaTanzania kwamba suala la mgomo wa madaktari kiini chake ni kudai kulipwa mishahara mikubwa na marupu rupu mengine ya mamilioni ya shilingi.
  Kila mara Rais akipata mwana wa kuongelea suala hili amekuwa akisisitiza juu ya madai haya ya mishahara mikubwa ambayo serikali haiwezi kumudu na makusudi kabisa kuacha kutaja Ukosefu wa Vitendea kazi,Uovyo wa mazingira ya kufanyia kazi na urasimu.

  Rais Kikwete na waziri wake mkuu Pinda wamekuwa hawaelezi kabisa ukweli juu ya asili halisi ya mgomo wa madakatari. Kama Suala la vitendea kazi,mazingira mabovu ya hospitali zetu yasiyo faa kwa mgonjwa na dakatari, bajeti finyu, wizi ulio kubuhu na ubadhirifu wa mafungu ya tiba, wagonjwa kurundikana katika wodi,bajeti finyu isiyotoshereza na ukiritimba wa wizara ya afya na serikali kwa ujumla.

  Kukwepa kutoongelea kiini cha mgomo wa madaktari mpaka sasa kimeweza kumpa uwezo wa kuendelea kuwarubuni wananchi wengi kwamba Madaktari ni watu wenye ubinafsi wasio jali kazi yao na watu wanao weka mbele fedha na maslahi kuliko wagonjwa na wananchi wa Tanzania.

  Kwa bahati nzuri kwake Kikwete wananchi wengi wa kawaida bado wanaamini chochote kisemwacho redioni kiandikwacho magazetini na kile waonyeshwacho katika luninga. Kwa mtaji huo bado kuna kundi kubwa la watu ambao hawaelewi vema madai halisi ya madkari zaidi ya yale yanayotolew na viongozi wa serikali kwa makusudi ya kudanganya.

  Wako wanao elewa wazi kiini cha mgomo wa madaktari lakini kwa sababu udhaifu wa serikali uliopelekea kusababisha mgomo wa madaktari ndiyo unao wapa neema, utukufu, heshima, mamlaka na mabilioni ya fedha mifukoni mwao hawako tayari kuukubali ukweli.
  Kiini cha mgomo wa madaktari kwao ni kiini cha Utajiri,heshima na utukufu wao wanaomba usiku na mchana kiini hicho kiendeee kuwepo. Kwa wenzetu hawa kuna faida ya kimaslahi kwao endapo mgogoro huu ukiendelea kutopata ufumbuzi. Kundi hili la watu lina jua wazi kwamba Ufumbuzi wa mgogoro wa madaktari utawanyima chanzo kikubwa cha mapato yasiyo na jasho kwao na kwa familia zao.

  Hata hivyo kwa namna yeyote ile serikali ya CCM ni lazima isalimu amri na kuleta mabadiriko ya kweli, kwa sababu muda kusema uongo umelikwisha siku nyingi wanishi katikamuda wa kuazima. Mfumo wetu wa afya nchini hautoi mwana wowote kwa serikali kucheza na suala hili. Serikali ya CCM imezoea kujibaraguza huku ikitoa vitisho vya hapa na pale mpaka suala lililopo mezani kwake litakapo sahaulika na kila mtu, hapo ndipo ile kauli ya NI UPEPO HUO UTAPITA HUTOLEWA. Hata hivyo suala la mgomo wa Madaktari linahusu maisha ya watu wote kwa ujumla wao bila kujari itikadi zao na imani zao.Jinsi muda unavyopita ndivyo jinsi suala hili litazidi kujisokotea katika mtirirko wa maisha ya kila siku ya kila mtu na kujidhihirisha wazi undani wake na hatimaye kwenda na system nzima.

  NO LONGER AT EASE
   
 17. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serekali ilishatamka kwamba mazungumzo na madaktari bado yanaendelea. Kati ya madai kumi na mbili matano yalishatekelezwa. Kwa nini madaktari hawa wasiwe na subira? Shinikizo hili la kuendelea kugoma linatoka wapi? Hivi tujiulize, kwa mfano polisi wetu nao wakiamua kugoma kwa sababu hawana vitendea kazi vya kutosha itakuwa sawa? Sote tunajua jinsi jeshi letu la polisi linavyopata tabu kiutendaji achilia mbali viwango vya chini vya mishahara yao. Madaktari wanachokosa ni uzalaendo na kamwe maswala yao hayatatatuliwa kwa migomo. Mimi nitaendelea kwenda kwenye hospitali za private nisije katwa mguu wakati kichwa kinauma!
   
 18. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kazi mbaya ukiwa nayo
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Any body can easily be a cop in Tanzania.
  After all, you need to fail most of your classes in O level in order to qualify to be a cop.
  As far as you don't arrest real criminals! Your job is safe.

  Who can not be a Police in Tanzania?

   
 20. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Mie naona MMK ima wakati unamsikiliza rais tayari ulikuwa unalala au ulikuwa na msongo wa mawazo. Rais kasema hakuna haja ya mgomo,kwani serikali ni mwajili tu, sasa kama wewe mwajiliwa unaona anachokupatia mwajili wako hakikidhi mahitaji yako basi unamaamuzi ya kuacha kazi. kama kweli serikali imekili kuwa haiwezi basi waache kazi. kawambia wasisubiri kufukuzwa ndani ya 24hrs. mie nadhani kiswahili hicho siyo kigumu kueleweka.wao waachie ngazi then serikali iajili upya.
   
Loading...