Madaktari mkisalimu amri sasa mmekwisha; mtawahukumu wanaokuja nyuma yenu

Mzee Mwanakijiji,

Unahaha na ufataani, wamekwisha rudi kazini fitna na majungu yako hayajafanya kazi.

Kwa maandiko yako inaonesha ulikuwa unaona raha wale wagonjwa wanavyoendelea kuteseka.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji,

Unahaha na ufataani, wamekwisha rudi kazini fitna na majungu yako hayajafanya kazi.

Kwa maandiko yako inaonesha ulikuwa unaona raha wale wagonjwa wanavyoendelea kuteseka.
Tatizo ma dr wangeweka na kokamaa kwenye kuboresha huduma za afya na madai yao yangejikita huko kweli watanzania wangewaa elewa. ndio maana serikali ikatumia madai yao 11 kuwamaliza, na wao wamebaki na dai moja tu ambalo ndio mwanakijiji anaona ndio nguzo pekee iliobaki.
 
"wanaokuja nyuma yenu" ni Kiswahili kibovu. "wanaokuja" ni "present tense".

Tathmini ujipange kuandika vizuri.
 
Any body can easily be a cop in Tanzania.
After all, you need to fail most of your classes in O level in order to qualify to be a cop.
As far as you don't arrest real criminals! Your job is safe.

Who can not be a Police in Tanzania?

We Jamaa unafikiria sana! Yaani kwa kifupi wewe ni mkali
 
Mzee Mwanakijiji!Kwanza Heshima yako mkuu wangu.
Mimi nadhani huu siyo muda wa kuchochea pande yoyote kati ya madaktari au Serikali maana kati yao hakuna anaye athirika bali ni mwananchi mimi nisiye na hatia.Kuendelea kuvimbishiana kifua na Serikali hakutawasaidia lolote hasa ukizingatia kuwa mkuu wa nchi ameshatoa msimamo wa serikali juu ya hili.
Ningependa tuwe kimya au kuwasihi madaktari warudi kazini wakati majadiliano yao yakiwa bado yanaendelea kama Rais alivyosema.Jamani kuandika tunaandika tu lakini hatujui impact inayoweza kutokana na maandiko yetu.Vifo vikiongezeka madaktari watajiongezea adui wa tatu ambaye ni mwananchi wanayeishi naye mtaani na pakifikia hapo sijui mtandika kitu gani tena humu jamvini.
Kwa hili Mzee Mwanakijiji sikuungi mkono hoja hata kidogo unless uwe una hidden agenda yako.
 
Serikali imewaeleza mgomo haukubaliki ,serikali kama muajiri mwengine yeyote yule anawalipa wafanyakazi wake kutokana na uwezo alionao serikali kwa waliyoyadai madaktari haina uwezo huo ,sasa hawa jamaa sielewi nikimaanisha madaktari ni kazi yao ipi isiyohitaji posho ??? Maana hiyo posho ni kwa kila stepu hata kutoka nyumbani kuelekea kazini basi atahitaji posho ,mmeona wapi ?

Serikali imeweka wazi kutoka kwenye hotuba ya Mheshimiwa Raisi kuwa asie weza kufanya kazi kwa makubaliano na mishara iliyopo awe huru kuacha kazi na si vinginevyo hakuna haja ya malumbano malumbano ya nini na serikali imesema haina uwezo na hakuna kulazimishana. waache kazi na wakatafute kule watakapolipwa mshahara wanaoupanga wao madaktari , Jamani mshahara ni makubaliano ya awali kati ya muajiri na muajiriwa ,ila baada ya kuajiriwa unadai makubwa ni muajiri gani atakubali hayo ?



Ni kweli kabisa unalosema mkuu,lakini hiyo ya wabunge inatoka wapi? Kinacholeta matfaruku hapa ni ule uwezekano wa wengine kupata na wengine kukosa katika serikali moja.
 
MTOA MADA IF SO UNATAKA TUINGIE LIBYA sema mzee tutakusaport but baada ya mda mchache kutakuwa hakuna mjanja, kwani sisi tunao lala nje ya majumba yetu kila siku kwa ajili ya maisha yenu na mali zenu hatuna haki, je hatuna elimu kama mnavyodai, na kama hauamini kama tuna shule za kufa mtu let do a research. NASHAURI selikali inajali watumishi wake wote maana wanategemeana, kukiwa na vita askari ni bora kuliko mtu yeyote, ukiwa huji kusoma mwalimu wa a,e,i,o,u ni muhimu sana kwa wakati huo kuliko soldier, ukiwa umekwama na usafiri konda ni muhimu sana kuliko mtu yeyote so tuvumliane wakuu. ikifika 2015 mtaamua mtu gani wa kumpa huu mtaa wa tanzania
 
Madaktari kama kweli wangekua wanajali maisha ya watanzania katika ile orodha yao wasingeweka madai 11 ya kwao na moja ndio hilo unaongelea hapa. Kiukweli hoja yao ingekua na mshiko kama wangesimama na hoja kama MMM aliivyoitabainisha hapa na watanzania tungewaelewa

According to them, wanasema Rais angetakiwa kusikiliza pande zote mbili, na kamwe madai yaliyosomwa na Mheshimiwa hayakuwa yao. Tangu wameanza mgomo huu wa mara ya pili hawajahi kukaa na serikali kuongea nao, hivyo nadhani ingekuwa vizuri kama yeye kama kiongozi wa nchi ambayo sekta ngumu na very delicate kama hii imekumbwa na matatizo kama haya angewaita na kuzungumza nao kabla hajasema hotuba ambayo imechangiwa na waliokuwa chini yake.
 
Mkuu bajeti ya kuwezesha madai ya daktari ipo ya kutosha tu. Kama Serikali itaamua kututoa misamaha ya kodi ambayo ni zaidi ya Shilingi 1.04 Trillioni kwa mwaka, kuhakikisha utajiri mkubwa wa mali asili nchini mwetu (Dhahabu, Uranium, Almasi, Tanzanite, Gas) unatumika kwa maslahi ya nchi yetu, kukomesha kabisa ufisadi wa mabilioni ya pesa miaka nenda miaka rudi kwa kuwashughulikia ipasavyo mafisadi kwa kutumia sheria za nchi basi ile kauli ya DHAIFU kwamba "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" itakuwa kweli. Ila tukiendelea kuamini ngojera za Serikali hii DHAIFU "kwamba nchi yetu ni maskini" "Serikali haina uwezo" basi hata miaka 50 mingine ijayo nhi yetu itazidi kuwa na hali mbaya kiuchumi na wajanja wachache ndani ya Serikali wakiendelea kuifaidi cake ya Taifa huku asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi maisha ya yaliyojaa ufukara wa kutisha.

Hii naikubali sana, ni rahisi kufahamika na mtu atakayeipinga au kushindwa kuifahamu hoja hii fupi akapimwe akili.
 
maana kauli ya jk ni sawa na kuwaambia wapiga kura {WAGONJWA}Kuwa “anayeona haridhishwi na huduma mbovu za hospitali za serikali basi aende hospitali binafsi huko kwenye huduma bora na madaktari wenye furaha na ari!!!!
shame on u mr dhaifu.
 
Mkuu bajeti ya kuwezesha madai ya daktari ipo ya kutosha tu. Kama Serikali itaamua kututoa misamaha ya kodi ambayo ni zaidi ya Shilingi 1.04 Trillioni kwa mwaka, kuhakikisha utajiri mkubwa wa mali asili nchini mwetu (Dhahabu, Uranium, Almasi, Tanzanite, Gas) unatumika kwa maslahi ya nchi yetu, kukomesha kabisa ufisadi wa mabilioni ya pesa miaka nenda miaka rudi kwa kuwashughulikia ipasavyo mafisadi kwa kutumia sheria za nchi basi ile kauli ya DHAIFU kwamba "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" itakuwa kweli. Ila tukiendelea kuamini ngojera za Serikali hii DHAIFU "kwamba nchi yetu ni maskini" "Serikali haina uwezo" basi hata miaka 50 mingine ijayo nhi yetu itazidi kuwa na hali mbaya kiuchumi na wajanja wachache ndani ya Serikali wakiendelea kuifaidi cake ya Taifa huku asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi maisha ya yaliyojaa ufukara wa kutisha.
Nasikia bajeti ya Tanzania na Rwanda zinzfanana hilo ni tatizo jamani
 
mzee mwanakijiji nakupongeza kwa makala yako nzuri, nimeisoma kwa kina nakuielewa, kwa wenzetu waliozoea ku copy n ku pest kwao bado ni ngumu kuelewa, ukweli ni kuwa THE LAW IS BLIND! IT CANT SEE AND WORSE ENOUGH IT CANT MAKE ITS OWN DECISION INSTEAD IT DEPENDS ON THE MINDS OF THE ONE WHO OWN IT!

madakatari tumeliona hilo, 2najua kamwe hamna mgomo halali, isipokuwa tu mgomo wa hiari kwa waumini wanpogoma kula na kunywa kumuomba Mungu kuwasamehe, kuwabariki etc.

inapokuja swala la jambo nyeti kama hili la madakatri kugoma watawala wakatumia nguvu kubwa kutafuta majibu rahisi badala yakutafuta mbinu thabiti zakuutatua inaonyesha unyonge wa fikra za watawala, napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa, mbinu zakung'oana meno na kucha kwa koleo zilitumiwa na wakoloni na kwa kuwa mifumo yetu ni muendelezo wa pale wakoloni walipo achia ndiyo waona wanatumia mbinu kama hii.

Rais Kagame jana akihutubia taifa na Mh rais wetu akiwepo alikemea tabia ya viongozi wakiafrika ku google majibu ya matatizo yao badala yakutumia bongo zao. Inashangaza viongozi wanapotulazimisha kuona rangi nyeusi kuwa nyeupe, wantamani kujua ni nani anafadhili mgomo wa madaktari na hawatamani kuona wala kusikia mahitaji halisi ya watumishi wa afya na wananchi kwa upana wake. ukweli ni kuwa hakuna anayefadhili mgomo wa madaktari kwa fedha, mawazo, au aina yoyote ya msaada. Madaktari tunao uwezo wakufikiri na kuamua bila kutumiwa na mtu na zaidi hatuna nia yoyote yakuichafua serikali kwa kuwa hatuwezi kukata tawi tulilokalia.

Ndugu zangu kwa hakika sisi tulio katika fani hii tumeona mengi sana, iadadi ya wagonjwa wanaokufa kwa kukosa vifaa tiba na madawa ya gharama nafuu ni kubwa sana na kibaya zaidi wanapokufa ndugu huishia kulia kidogo nakusahau mpaka atakapokufa mwingine ila kwetu tunaona mambo hayo kila iitwapo leo.

nina kubali kabisa kuwa kiapo cha watumishi wa afya hakiruhusu mtu kugoma ila kina mtaka mtoa huduma ya afya kuweka mbele haki ya uhai wa mgonjwa kwa gharama yoyote ile, na hiki ndicho tunachikifanya, kuiambia serikali ya kuwa tunataka mabadiliko katika sekta ya afya, kwa upana wake.

wanaosema madaktari ni watu wenye ubinafsi na wanaotamani kuishi maisha yakiteule siyo kweli , kinachotusukuma ni kutaka kuona sekta ya afya inapewa kipaumbele kinacho stahili, tuna omba umma wa Watanzania wajue kuwa hatuna nia yakutaka wao wapunguziwe maslahi tupewe sisi la hasha tunaamini kila mtumishi wa umma anapaswa kupewa maslahi yanayolingana na mahitaji yake na kulingana na vigezo vilivyopo na uhalisia wa maisha.

Niwakumbushe tu ya kuwa serikali hii hapo mwaka 1998 ilifanya upembuzi yakinifu kuangalia ni viwango gani vya mishahara kitakacho stahili kulipwa kila mtumishi wa umma kwa vigezo vilivyo ainishwa na ripoti hiyo na mapendekezo yake yapo mezani kwa ofisi ya utumishi, nawasihi kila mmoja pale alipo aitafute aisome aone mwaka 1998 alipaswa lipwa shilingi ngapi kwa ugumu wa maisha ya wakati ule kisha aone kwa sasa atastahili kulipwa kiasi gani.

siyo hilo tu pia kuna miongozo na taratibu za kazi baada ya muda wa kawaida wa kazi, safari za kikazi na kadhalika , ni vyema pia wakazisoma waelewe haki zao,badala yakusikia mambo yanayoelezwa kwa umahiri na mwajiri tu bila kumpa mwajiriwa fursa yakueleza upande wake.

nina wasihii Watanzania wenzangu hasa madakari (MD) assistant Medical officers (AMO) clinical Officers (CO) na watendaji wengine wote wa sekta ya afya tuungane pamoja kudai kuboreshwa kwa sekta ya afya kwa manufaa ya wananchi na watumishi wa afya.

serikali inakotupeleka siko tunakotaka kwenda japo tunaweza kwenda, tukiungana madaktari kwa uchache wetu tuna weza kuuza huduma kwa wananchi kwa gharama kubwa ambazo wananchi wengi hawataweza kuzimudu. mmesikia Mh rais akijivunia kujengwa kwa hosipitali ya moyo, figo, etc, haya yote yamewzekana kwa utayari wetu wakuishauri serikali na wakati huo huo kujitoa kusoma kwa muda mrefu ili huduma hizi ziwafikie watanzania wote na kwa gharama rafiki kwa watu wote.

Umenena vizuri sana. Pichanayoipata hapa Serikali haikupewa maelezo vizuriau tuseme imepotoshwa! Bado serikali kama ina nia ya kweli ya kumaliza mgomo huu inaweza na si kuishi kwa hisia kuwa kuna chama fulani eti kina mkono nyuma yake. Ebu waboreshe huduma za afya, vitendea kazi, miundombinu, maslahi na dawa kama mgomo utakuwepo.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom