Kama wameshindwa kusimamia tukapata sanamu linaloendana na uhalisia wataweza kusimamia mambo kwa maendeleo ya nchi?

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Hata madaktari na wanasayansi wanapofanya majaribio na utafiti wao kama ni tiba huwajaribu wanyama wakipona basi tiba hiyo hupewa wanadamu.

Kama dawa au upasuaji haukufanikiwa kwa kitu halisi basi binadamu hawezi kufanyiawa au kupewa dawa hiyo.

Sasa CCM wameshindwa kutengeneza sanamu tu ambalo sio halisi je unafikiria wataweza kufanya jambo halisi la maendeleo kwa wananchi?

Kama li sanamu tuu limewashinda, watamaliza uhaba wa sukari, umeme, ajira?

Hawa ma ccm yanatawala kwa nguvu bila ridhaa ya watu na hawajui nini cha kufanya hawana dira. Ndio mana juzi kuna kibwetele mmoja ameropoka eti serikali isilaumiwe watu kukosa maendeleo kwa kuwa sio wajibu wa serikali kuwaletea watu maendeleo.

Huyu anayesema hivi alikuwa waziri na aliapa kuitii katiba inayosema jukumu kuu la serikali itakuwa ni kuleta ustawi kwa wananchi.
 
Wamezingua! Wametengeneza sanamu ya Nyerere ambalo sura sio ya Nyerere halafu wanapiga chapuo kutuaminisha! Nani asiyejua sura ya Nyerere!
 
Wamezingua! Wametengeneza sanamu ya Nyerere ambalo sura sio ya Nyerere alafu wanapiga chapuo kutuaminisha! Nani asiyejua sura ya Nyerere!
Haya ma ccm ni mabingwa wa upotoshaji na urongo.

Tanganyika ilijipatia uhuru wake mwaka 1961 haya majambazi yakapora uhuru wa Tanganyika na watu wake na kuipa nchi isiyojulikana ya Tanzania bara.

Ukiyaangalia usoni yakivaa suti utafikiria yamesoma kumbe ni ma mbumbumbu tuu yalizidiwa akili na ka nchi kadogo kaliko kataa kuua serikali yake na kukataa kutawaliwa na wageni.
 
Back
Top Bottom