Madaktari: Hakuna anayerudi kazini kesho!

Na kesho madaktari wasipoenda, itabidi yeye awajibike tumechoka kwa kauli za kupuuzi za watawala wa Africa
 
uwe makini waandishi si lazima uwafuate lakini na pia kama mtu mzima anakwenda mahali ambapo unajua kabisa unayekwenda kukutana naye hayupo halafu unakwenda na kutishia ni upunguani.
 

Mchambuzi,
Serikali yetu imejaa wababaishaji wengi, wapo mawaziri wengi wamepewa wizara wakiwa hawana uwezo wa kuongoza, na hicho ndicho kinachokwamisha utendaji wa serikali, hata mh. Pinda mwenyewe hakustahili kupewa hiyo nafasi ya uwaziri mkuu, uteuzi wake ulikuwa ni wa kisiasa zaidi kuliko utendaji, tukirudi kwenye mgomo wa madaktari ukweli viongozi husika hawana wanachojali, wao matibabu yao ni India labda wagome madaktari wa India ndipo watakapofungua macho na masikio, inakuwaje nchi inakabiliwa na mgomo madaktari mh. Raisi na makamu wote wapo safarini?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Dr STEPHEN ULIMBOKA sisi wapenda maendeleo na ustawi wa jamii ya nchi yetu Tanzania tuko nyuma yako na tunaunga mkono msimamo wako na madaktari wenzako.
Usiogope kitendo cha Habithi Waziri mkuu,aliye Mamruki wa Mafisadi wa CCM cha kukuengua,kukutenga na kutaja jina lako na kukupa kibandiko bandia kwamba wewe Dr Stephen Ulimboka ni mjeuri,unakiburi, mkorofi, ni mtu hatari( kashindwa tu kukuita terorist na muuaji) .

MH Pinda ni kama vile umedata???Somo la Leo si ukorofi wa Dr Stephen Ulimboka.

Somo la Leo ni Uzandiki wa Serikali ya CCM kuwekeza Hospitali za Magabaholi huko India na kudumaza Huduma na ustawi za Hospitali ndani ya Tanzania.

Pinda anapindisha somo ili kuvurugana na kupotosha mwelekeo na uhalali wa madai ya Madakatari.
Njama za Pinda haziwezi kushinda kwa sababu kashindwa kabla hata hajaanza.

Dr Ulimboka kumbuka hata Carl Peters yule Jasusi wa Kijerumani alitumia janja hiyohiyo ya DIVIDE AND RULE kutulegeza kama jamii na kutweka Nira ya chuma ili tubebe uchumi wa nchi yake ujerumani.

Leo hii Pinda ana tumia janja ya Carl Peters ili kuwagawa wapenda maendeleo wote Tanzania ikiwa ni pamoja na waheshimiwa Madaktari kwa nia ya kuneemesha na kufaidisha ustawi wa MAFISADI walio viongozi wa CCM na vibaraka wao wote nje na ndani ya nchi.

Waziri mkuu Pinda ni mshenzi (BABARIAN)kama walivyo washenzi wengine wote DUNIANI.

Wewe Dr Ulimboka kama una uwezo binafsi wa kushawishi madakari kugoma bila kutumia FFU virungu na mabomu ya machozi, inaonyesha jinsi ulivyo kiongozi mwenye talanta ya kuzaliwa na siyo ile talanta ya kuvikwa kama GAGULO waliyo nayo viongozi wote wa Serikali ya CCM.

Dr Ulimboka,Viongzi wote wa CCM wanakuoa hatari si kwa sababu wewe kweli ni mtu hatari bali kwa vile tu macho yako yamefumbuka akili yako ni Timamu na zaidi, Unyonge unaotumaliza Watanzania tulio wengi wewe ulisha kutoka siku nyingi zilizo pita na sasa una ari ya kuondoa unyonge wa walio wengi kwakutumia kipaji chako na elimu yako.

Dr Stephen Ulimboka usibabaike hapo ulipowashika usianchie kabisaaa, umewameshikwa pabaya sana, sasa wanahaha kama fungo kashikwa haja mbili.

Viongozi wa serikali ya CCMwana Njama za Kuhujumu na Kudhurumu Utu wa kila Mtanzania.
Njama zao CCM zimefika ukingoni, kushindwa ni lazima.

Madaktari wamekutana na waandishi wa habari muda si mrefu na kutoa kauli ya kukaidi amri ya Waziri Mkuu juu ya wao kurejea makazini kesho.



Dr. Stephen Ulimboka, mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari akitoa tamko lao...
 
Acha Dharau.

 

Upo sahihi. Lakini miaka yote nilikuwa najisemea mwenyewe kwamba tatizo pale labda pia linachangiwa na uwepo wa mawaziri wasiojua masuala ya public health management. Mponda ni mtaalam wa hilo, lakini hakuna kitu. Miaka ya nyuma wamejaribiwa mawaziri wenye background ya utibabu, haikufanya kazi, wakawekwa wanasiasa kama mama Zhakia Meghji na wengineo, nayo haikusaidia. hii ina maana kuna tatizo kubwa zaidi - la kimuundo, sera, siasa na ufisadi.
 



FF hata wewe umekata tamaa? I didn't expect this from you...hakuna tunaloweza? Oooh, yes we can do something! Are you seating in public office believing that we can't do anything positive for our good nation? Is this the spirit? Kama wewe umejikatia tamaa huwa unatoa maamuzi gani kama mtumishi?

Ma "advisor" kama waarabu? Kwani makatibu wakuu ni nani kama sio advisors? Au tubadilishe title tu zao? Halafu hao the-so-called advisors watapata support na watawezeshwa kushauri inavyopaswa na wakasikilizwa? Au wataundiwa zengwe na kutupwa nje? Give me a break, FF, I strongly believe we can do something, siyo kukaa tu na kusema hatuwezi kufanya jambo lolote.

Leo umeongea na nimeona jinsi ulivyo. Mtupu na umekata tamaa. Eti hatuwezi jambo lolote! Si kweli. tunaweza kuleta maendeleo katika nchi yetu. No wonder watu wamejikatia tamaa kama wewe wanakula kila mtu kivyake kwa urefu wa kamba yake.
 


Wanaoweza wanaanzisha kampuni na hospitali zao binafsi..siyo kulalamika mishahara

Pesa ziko nyingi tu kwenye bank, madaktari waliochoka na serikali watengeneza hospitali ya mfano waajiri madaktari na wawalipe mshahara wanaotaka wao..

Halafu itatia akili kwani wataweka mshahara competative salary ili watu wache wafanye kazi serikalini, otherwise hakuna wanachowezza zaidi kulalamika, kuandamana, na kulaumu sifa kubwa ya wabongo..
 

Kamanda umewesema vyema, true diagnosis, na true prognosis ya mgonjwa, tatizo na wewe umetoa prescription ya kisiasa!!!! lakini ni better kuliko ile ya fundi skurubu pinda kufanya doctors kama wanafunzi wa vyuo...

KUhusu bajeti, and the budgetting process, my brother that is when i realised that we dont have the minister for health, his deputy au PS au hata CMO, walichakachua bajeti, wakatumia baadhi ya watu wa kamati ya bunge, wakawahonga, wakafuni kombe, kibaya zaidi madaktari wanajua kilichotokea, vijana wa sikika wakaleta waliyoyaona... but in a jungle state, memos were circulated, shoddy justifications were set and boom the budget passed, TUNAJUA KILICHOFANYIKA

From that day, i learnt kwamba Wizara ya Afya imeingia gundu/najisi kabisa..... and what we see is just a tip of an inceberg

Jiulize swali moja.... WHO SUFFERS IN ALL THIS???? Mpiga kura aliyenyimwa elimu, nafasi, haki na usawa... huu ni mtaji, but this time wataalam wa afya watafanya waliyoweza wasomi wa ukerewe, kwenda nyumbani kuelimisha, kila mmoja kwenye jimbo lake ka kusema kweli nini kilitokea, kutibu bure, kushawishi wanachi juu ya maradhi yawasumbuayo, kusema ukweli bei ya dawa wanayotumia na gharama inayokua accounted mwisho wa siku kwenye vitabu vya serikali

there are three years remainig and that gives medical personnel time to document ukweli wa sekta, tena kwa nafasi na wakati, free na hakuna atakayestop this one

PINDA KWA HILI AMEPINDA, NA AMEPINDISHA FACTS, ILI TU KUPINDISHA HAKI NA HII INAPINDISHA SOCIAL JUSTICE PRINCIPLES
 

FF... tuna advisers kwenye kila nyanja, tumewageuza wabeba briefcase za akina "tall-Membe", tena unajua tunawapataje??? tunacheki swahiba we dont care about knowledge, na hata kama ana knowledge, we dont listen to him/her, tunasikiliza washkaji, tunasoma gazeti la uwazi na kisha tunajichimbia kwa waganga kusoma nyota, mbalamwezi na sayari!!!!

tukishindwa kabisa, tunamwachia Mungu
 

Well Said. As we head towards 2015, CCM inajijenga mazingira mengi sana ya self - destruction. Kuna mambo mengi sana ambayo itakuwa magumu to reverse. Pengine mtu kama pinda hatajali kwani atakuwa amestaafu na hana kashfa yoyote ya ajabu, kwahiyo atakula pension yake vizuri tu kama mstaafu na mkulima. Otherwise hili suala angelisimamia kwa umakini zaidi.
 
FF acha urongo! Kikwete ni mbadhirifu wa Mali za nchi, Mwizi, Hana vision! Hata kodi hawezi kusanya! Uchumi umekuwa mgogoro! Serikali lege lege na imejaa ushikaji kila kitu ni midhaha tu
 

Dada, Jk kajitengenezea mwenyewe huo mfumo wa kejeli dharau nk. wansema ukiua kwa upanga, basi utakufa kwa upanga... aliwakumbatia hao kejeli family kupanga wengine vinyesi, sasa ile karma inaplay role yake

mwambie (najua una access) afumbe macho, aume meno na afanye kweli.... VUNJA BARAZA, TANGAZA KAZI ZA WAKURUGENZI WA IDARA NYETI NA AANZE UPYA, TUTAMUWEKA KWENYE VITABU MILELE
 
ff acha urongo! Kikwete ni mbadhirifu wa mali za nchi, mwizi, hana vision! Hata kodi hawezi kusanya! Uchumi umekuwa mgogoro! Serikali lege lege na imejaa ushikaji kila kitu ni midhaha tu

kamanda, serikali inakusanya kweli kodi za wafanyakazi, lakini sio wafnyabiashara, kwani wao huwasilisha direct kwa wakuu kwenye maboksi na visalfeti... Yupo mmoja kigambo ana ardhi kuliko ikulu, anahonga balaa
 
kamanda, serikali inakusanya kweli kodi za wafanyakazi, lakini sio wafnyabiashara, kwani wao huwasilisha direct kwa wakuu kwenye maboksi na visalfeti... Yupo mmoja kigambo ana ardhi kuliko ikulu, anahonga balaa

Aiseeee!!
 
Hapa kuna hatari na ya wagonjwa wote kuwa wanapimwa na kuambiwa hawaumwi
 
Hizo pumba tu. Ukweli unashindwa kuusema, nioneshe kimoja ambacho walifanya wa kabla yake yeye hakukifanya zaidi yao.

kukaa na cameroon,huku akiwa amemwambia kama anataka misaada lazima..... Malizia mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…