Madai ya Wazanzibari 15 na Yasemwavyo kuhusu Muungano na Hatima Yake

Ukishasema "mtoto akililia wembe mpe" ni kama umeona wewe unajua zaidi kinachoweza kuwadhuru Wazanzibar zaidi yao wenyewe, kama mtoto mdogo asiyejua madhara ya wembe.

Kabla ya Muungano, mbona wembe haukuwakata?

Ukisoma mienendo ya thread za Muungano unaona dhahiri Watanganyika tunalazimisha Muungano.

Hakuna Mzanzibari aliyelazimishwa Muungano, naona hata kwenye Sherehe Wazenj wapenda Muungano wametulia tele kuufurahia Muungano! Kusema eti wanalazimishwa ni kuwadhalilisha Wazanzibari kama vile ni watu wanaopelekwa pelekwa tu!
 
Hamjalalamika kwa sababu ndio mnaofaidi nchi moja kubwa kuikalia nyengine ndogo.

Wazanzibari watachukua kila hatua kuondokana na adha ya "muungano" huu feki.

“[President Nyerere] managed half the work of a python… He swallowed Zanzibar all right but he did not crush its fighting force first. The live animal is a long time digesting, and its kicks are being felt hurtfully, and possibly even fatally, deep inside Tanganyika’s body politic.”

- ‘The Perils of Nyerere’ in The Economist of June 1964

Muungano mlisaini wenyewe, Karume akakubali kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Nyerere akiwa Rais! Mabadiliko ya 11 ya Katiba ya JMT, 1977 ndiyo yaliyoondoa nafasi ya Makamu wa Rais kuwa moja kwa moja Rais wa Zanzibar! Kama Wazanzibari wasingeupenda Muungano wasingekimbilia mahakamani kupinga mabadiliko hayo ya 11! Pia malamiko mengi ya Wazanzibari ni ya "kutaka haki zaidi" kwenye Muungano badala ya kuuvunja! Otherwise, wangeshajitenga zamani!
 
unataka kusema hata mama Fatma Karume ameudanganya umma kwa miaka yote hii anaposema mumewe hayati mzee Karume ndiye aliyesimamia na kuongoza mapinduzi??

huo ndio ukweli, hebu uliza ni watu wangapi walishuhudia Mapinduzi siku ya Jan 11, '64, hata hapo ulipo bila shaka wapo wazenji waliokuwepo kipindi hicho hebu waulize
 
Tunaambiwa Mapinduzi yalifanywa na wananchi hasa vijana hata wakauchoma moto Mjimkongwe je ni kweli yalifanywa na wazanzibar?
 
Vijana wa kizanzbar nyie ndio wengi mpo hapa na inaonyesha kua hamuupend muungano,anzishen makongamano muwahamasishe na wenzenu ili saut zenu zisiikike,tatizo hamtaki kwenda shuleee,wengi wenu atleast mkija bara ndio mnaambulia shule,maana hata mkipga kelele hapa haisaidii,
mimi ni mwalimu na nawafundisha watoto kutoka visiwani,wengi ni dead wood kama si slow learners,so kwanza vijana muwende darasan kisha anzshen harakat za kudai nchi yenu

Hili ni janga kwa Taifa kama si maafa makuu kwa elimu yetu.
Mwalimu hajui hata kutenganisha mwanzo na mwisho wa sentensi. Hajui kuliandika neno kiusahihi, lina upungufu wa herufi. Hajui matumizi ya alama na vituo (punctuation marks).

Ukiwa na mwalimu kilaza hivi, jua utazalisha vilaza mara mbili.
 
hili likitu halina faida bana ni bora uvunjwe tu hauna maana yoyote
 
Ni kweli Muungano hauna faida kwetu Watanganyika ila ukweli ni kuwa hautavunjwa hata mmwage machozi ya damu au kufa Muungano utaendelea kuwepo kwa lazima mpaka pale CCM itakapofika mwisho wa kutawala
 
Sio kila upande unaona mwenzake hafai! Tanzania Bara hakuna vipeprushi vya kususia sherehe na pia hawajawahi kupeleka kesi yoyote mahakamani dhidi ya Muungano kama walivyofanya Wazanzibari!


Ulishasikia mvamizi akalalamika?
 
Haaa haaaa! Zanzibar iliyokuwa na kiti UN haikuwa ile ya Sultani wandugu? Mapinduzi tr 12/01/1964, Muungano tr 26/04/1964 baada ya kuhofia kurudi kwa Sultani, kwa hiyo ulikuwa ni muda mfupi kwa Zanzibar kufanya hayo yote!

La! Serikali iliyotowa msaada kwa Tanganyika ilikuwa ya Abeid Amani Karume!
 
Si kweli kwamba Wazanzibari hawapendi ushehe wa mtu, ndio maana chokochoko za Muungano huwa zinaanzia misikitini!


Kwako wewe Zanzibar mikutano yote inafanywa msikitini? Una maana kuwa Samweli Sitta alisilimishwa na kuingia msikitini ili kuendesha mkutano wa Katiba?
 
Ulishasikia mvamizi akalalamika?

Baada ya miaka 47 ndio "mnagundua" uvamizi kama yule mzungu "aliyegundua" Mlima Kilimanjaro? Lazima utakuwa ni "uvamizi mzuri," ndio maana "haukugundulika" mapema, hadi itumike "microscope!"
 
Kwako wewe Zanzibar mikutano yote inafanywa msikitini? Una maana kuwa Samweli Sitta alisilimishwa na kuingia msikitini ili kuendesha mkutano wa Katiba?

Ni wapi nilidai kuwa "mikutano yote" inafanyikia misikitini?
 
Hakuna Mzanzibari aliyelazimishwa Muungano, naona hata kwenye Sherehe Wazenj wapenda Muungano wametulia tele kuufurahia Muungano! Kusema eti wanalazimishwa ni kuwadhalilisha Wazanzibari kama vile ni watu wanaopelekwa pelekwa tu!

Nafikiri tusioshauriwa huu Muungano ni wengi kuliko hao unaowasema wewe! Ukweli ni kuwa iwapo hata viongozi wa juu wa Zanzibar wanaposema kuwa hawaridhiki na Muungano huo ni ushahidi tosha huko kupelekeshwa kumewatosha!
 
Kuna kila sababu ya kukaaa na kujadili MUUNGANO, na si kudanganyadanganya watu kwa kufanya miafaka na mashirikisho ya kipuuzi ya vyama fulani VIWILI TU, ili kuwasahaulisha watu kwa muda!..hizi ni mbinu za kishetani ambazo tayari wazanzibar washazishitukia, na sasa wameona muafaka ni kusimamia jambo hili kwa matendo ya kushitua kidogo!

Mwisho wa kwepakwepa umefika, Hati za Muungano ziwekwe hadharani, ili ijulikane articles zilikuwa zinasemaje, na je bado zina mashiko kwa karne hii?
Mgonjwa wa Malaria haponi kwa Diclopar!

Hapa Jimmy, umefunga mjadala kwangu.... hiyo ndio njia pekee....
Tunataka UKWELI
 
Nafikiri tusioshauriwa huu Muungano ni wengi kuliko hao unaowasema wewe! Ukweli ni kuwa iwapo hata viongozi wa juu wa Zanzibar wanaposema kuwa hawaridhiki na Muungano huo ni ushahidi tosha huko kupelekeshwa kumewatosha!

Hao Viongozi wenu ni wanafiki, sio wakweli hata kidogo, wanafanya maamuzi wenyewe kisha baadaye wanakuja kudai kuwa eti walipelekeshwa!
 
Hilo halitasaidia kwani Zanzibar imejaa wanaofaidi na kuutaka "muungano" kutoka Dar na Tanga walioletwa kwa maksudi. ikijuulikana Wazanzibari wengi hawashughulikii

Kwa Wazanzibari wengi, hii ni siku ya huzuni, siku walipopokwa nchi yao waipendayo.

Kwa Wazanzibari wengi, hakuna cha kusherehekea.

Pole kwa kuwa una huzuni siku ya leo. Naomba kujua elimu yako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom