Madai ya Wazanzibari 15 na Yasemwavyo kuhusu Muungano na Hatima Yake

Kwa suala la Muungano Watanzania Bara si kweli kuwa wanaupenda ndiyo maana hawajaenda mahakamani ila ni kuwa hawajali. Rais wa Muungano anaonekana wazi ni Rais wa bara japo Nyerere alionekana ni Rais wa Tanzania yote kwa matendo. Watu wa Zanzibar kwa sababu ya kufanana mitizamo ni rahisi kuamua maamuzi yanayofanana tofauti na bara. Wazanzibari ni wachache na unapozungumza suala la nchi yao wanaacha kutazama "Yanga na Simba" wanakusikiliza unachosema. Huku bara mambo ni tofauti kidogo. Huku bara Maaaskofu na Masheshe wakisema "acheni!" ni rahisi watu kusikiliza bila kuweka maswali mengi (kama ilivyokuwa imani katika dunia ya nchi za kiarabu ambayo sasa inaanguka), Zanzibar wanamsikiliza yule anayesema yale wanayoamini tu na si U-Shehe wake.

Si kweli kwamba Wazanzibari hawapendi ushehe wa mtu, ndio maana chokochoko za Muungano huwa zinaanzia misikitini!
 
@lordjustice
kukuelimisha tu ni kwamba kiti cha UN kilipatikana baada ya uhuru wa znz wa dec 10 mwaka 1963.serikali iliyokuwa ikiongozwa na waziri mkuu, mzalendo sh.mohammad shamte.mfalme alikuwepo kiheshima tu na alikuwa si mtendaji.baadae watanganyika wakaja wakaipindua na kuitawala upya znz.kwetu sisi muungano ni jini linalonyonya damu zetu.leo ni siku ya huzuni kuu na hatuna cha kusherehekea.
 
Zanzibar hawakuhofia kurudi kwa Sultani kwa sababu sio wao waliofanya Mapinduzi, ni Nyerere aliyefanya Mapinduzi usiku wa January 11, 1964 kutumia Special Forces na kulazimisha Muungano. Note that!


Mapinduzi yalifanywa na Wazanzibari wenyewe, asikudanganye mtu! Mmeshazoea kumfanya Nyerere kama kitambaa cha kupengea kamasi, as if Wazanzibari hawajawahi kabisa kuvikalia hivyo visiwa, au alikuwa vichwani mwa Wazanzibari kila mara ku-deactivate akili zao! Haya tutajie idadi na majina ya hao unaowaita "Special Forces" waliotumwa na Nyerere tr 11/01/1964!
 
Kuna kila sababu ya kukaaa na kujadili MUUNGANO, na si kudanganyadanganya watu kwa kufanya miafaka na mashirikisho ya kipuuzi ya vyama fulani VIWILI TU, ili kuwasahaulisha watu kwa muda!..hizi ni mbinu za kishetani ambazo tayari wazanzibar washazishitukia, na sasa wameona muafaka ni kusimamia jambo hili kwa matendo ya kushitua kidogo!

Mwisho wa kwepakwepa umefika, Hati za Muungano ziwekwe hadharani, ili ijulikane articles zilikuwa zinasemaje, na je bado zina mashiko kwa karne hii?
Mgonjwa wa Malaria haponi kwa Diclopar!
 
Vijana wa kizanzbar nyie ndio wengi mpo hapa na inaonyesha kua hamuupend muungano,anzishen makongamano muwahamasishe na wenzenu ili saut zenu zisiikike,tatizo hamtaki kwenda shuleee,wengi wenu atleast mkija bara ndio mnaambulia shule,maana hata mkipga kelele hapa haisaidii,
mimi ni mwalimu na nawafundisha watoto kutoka visiwani,wengi ni dead wood kama si slow learners,so kwanza vijana muwende darasan kisha anzshen harakat za kudai nchi yenu
 
Sio kila upande unaona mwenzake hafai! Tanzania Bara hakuna vipeprushi vya kususia sherehe na pia hawajawahi kupeleka kesi yoyote mahakamani dhidi ya Muungano kama walivyofanya Wazanzibari!

Hamjalalamika kwa sababu ndio mnaofaidi nchi moja kubwa kuikalia nyengine ndogo.

Wazanzibari watachukua kila hatua kuondokana na adha ya "muungano" huu feki.

"[President Nyerere] managed half the work of a python… He swallowed Zanzibar all right but he did not crush its fighting force first. The live animal is a long time digesting, and its kicks are being felt hurtfully, and possibly even fatally, deep inside Tanganyika's body politic."

- ‘The Perils of Nyerere' in The Economist of June 1964
 
"mtoto akilia wembe mpe". Ndo akili za viongozi wetu watafuta madaraka wa afrika kuwahadaa na kuwaaminisha watu kuwa "pasipo muungano maendeleo ya zanzibar yatakuwa juu". Hii ni dhana dhahania, na kwa uroho wa madaraka na ubinafsi wa viongozi wa kiafrika, maendeleo ya wazanzibari/watanzania ni kujilimbikizia mali na usitawi wa viongozi/wafalme wa kiafrika. Chuki za kidini, kikanda (zanzibar vs bara), kikabila zimechachushwa na viongozi watakao madaraka kwa kuwaaminisha wananchi watawaliwa kuwa kwa namna hii....maisha yao yatabadilika-kumbe mmmmmmmmmh,ni ndoto za alinache!!!! "kalaga baho" .

Safi sana mkuu nsimba, hawa wenye ndoto za 'kuukata' nje ya muungano bila kuwa na mikakati ya kuendelea wanaishi ktk dhana dhania.
Gharama za kiutawala kwanza ni kubwa ktk mfumo huu achilia mbali mijitu yenye uchu wa mali za umma.
 
"mtoto akilia wembe mpe".
Ukishasema "mtoto akililia wembe mpe" ni kama umeona wewe unajua zaidi kinachoweza kuwadhuru Wazanzibar zaidi yao wenyewe, kama mtoto mdogo asiyejua madhara ya wembe.

Kabla ya Muungano, mbona wembe haukuwakata?

Ukisoma mienendo ya thread za Muungano unaona dhahiri Watanganyika tunalazimisha Muungano.
 
Muungano gani huu?? Rais wawili wa TANZANIA na wa ZANZIBAR yuko wapi wa TANGANYIKA? Serikali ya mapinduzi ya ZANJI!!, iko wapi serikali ya TANGANYIKA? Kuwe na articles za wazi kwa nini hakuna rais wa kuwawakilisha Watanganyika? Kama rais wa muungano ni mmoja hakuna haja ya kuwa na rais mwingine wa pili (Zanji). Tunafungamana kwa maslahi ya watu wawili ambao hata hivyo walishatangulia mbele ya haki. Muungano ujadiliwe upya.
 
Wanaotaka ufe sio viongozi peke yao, bali Wazanzibari wengi hawautaki hivi ulivyo ambapo inaonyesha dhahir kuwa nchi moja kubwa imeikalia nyengine ndogo.

Hizo gharama ambazo Dr. Lwaitama anazizungumzia zinamhusu nini? Kwani kabla ya huu unaoitwa "muungano", kila nchi ikijiendesha vipi?

Kabla ya Muungano, Zanzibar ilikuwa na kiti chake UN na katika agencies zake kadhaa. Pia ilikuwa na kiti huko Jumuiya ya Madola na itifaki zote za kiserikali.

Huu si muungano kabisa, unadumu kwa kutumia nguvu za dola tu.
Waungwana naomba mnijuze hao raia/wananchi wa Zanzibar asili yaoi.e.mababu zao walitokea wapi?!
 
Haaa haaaa! Zanzibar iliyokuwa na kiti UN haikuwa ile ya Sultani wandugu? Mapinduzi tr 12/01/1964, Muungano tr 26/04/1964 baada ya kuhofia kurudi kwa Sultani, kwa hiyo ulikuwa ni muda mfupi kwa Zanzibar kufanya hayo yote!


Zanzibar ilipata UHURU tarehe 10/12/63 na sio tarehe 12/01/1964.

Huo ni upotoshaji mkubwa wa Historia ya Zanzibar My Lordship.
 
Waungwana naomba mnijuze hao raia/wananchi wa Zanzibar asili yaoi.e.mababu zao walitokea wapi?!

Hapa mada sio asili lakini kama unataka kujua, Zanzibar ni kisiwa na kina watu wa asili mbali mbali ikiwa ni pamoja na Tanganyika.

Kwani Tanganyika unadhani haina asili?
 
Zanzibar hawakuhofia kurudi kwa Sultani kwa sababu sio wao waliofanya Mapinduzi, ni Nyerere aliyefanya Mapinduzi usiku wa January 11, 1964 kutumia Special Forces na kulazimisha Muungano. Note that!
unataka kusema hata mama Fatma Karume ameudanganya umma kwa miaka yote hii anaposema mumewe hayati mzee Karume ndiye aliyesimamia na kuongoza mapinduzi??
 
Vijana wa kizanzbar nyie ndio wengi mpo hapa na inaonyesha kua hamuupend muungano,anzishen makongamano muwahamasishe na wenzenu ili saut zenu zisiikike,tatizo hamtaki kwenda shuleee,wengi wenu atleast mkija bara ndio mnaambulia shule,maana hata mkipga kelele hapa haisaidii,
mimi ni mwalimu na nawafundisha watoto kutoka visiwani,wengi ni dead wood kama si slow learners,so kwanza vijana muwende darasan kisha anzshen harakat za kudai nchi yenu
mimi ni mtanganyik-lakini pia muungano naona imefika wakati sasa ufike kikomo
 
Kuvunja Nchi? ndoto ya wajinga, mbona kila mtu angetamani? kama ingekuwa inawezekana kirahisi si Pemba ilishaomba? na mikoa mingine nayo ikitaka? tusidanganyane, hakuna anaeonewa au wote watafute jambo la kulalamikia? semeni lingine.
Muungano haurudi nyuma, daima.
 
mimi ni mtanganyik-lakini pia muungano naona imefika wakati sasa ufike kikomo

kwa hili tupo pamoja,yaani mimi siioni mantiki ya muungano,sinufaiki nao,sisomi zanzbar,sifany kaz huko,sifany biashara huko,wala hakuna bod ya mikopo huko,so wajitenge huenda wanachokiamin kitatimia,kua watamove foward
 
Kuvunja Nchi? ndoto ya wajinga, mbona kila mtu angetamani? kama ingekuwa inawezekana kirahisi si Pemba ilishaomba? na mikoa mingine nayo ikitaka? tusidanganyane, hakuna anaeonewa au wote watafute jambo la kulalamikia? semeni lingine.
Muungano haurudi nyuma, daima.
zipo nchi zilizowahi kuungana na zishavunja muungano wao-kwa hio sisi tutakuwa si wa kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom