Madai ya Wazanzibari 15 na Yasemwavyo kuhusu Muungano na Hatima Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya Wazanzibari 15 na Yasemwavyo kuhusu Muungano na Hatima Yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaimati, Apr 24, 2011.

 1. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sun, 24 Apr 2011
  Salma Said

  WAKATI vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama yakiendelea na mazoezi ya gwaride katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kwaajili ya maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 47 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Wazanzibari 15 wanaojulikana kama G15 wamejitokeza na kuhoji uhalali wa muungano huo kwakuwa hauna mkataba.


  G15 ni kati ya vikundi mbalimbali vinavyojitokeza kuhoji uhalali wa muungano huku vingine vikishia kuishitaki serikali mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar jana, Makamu mwenyekiti wa G 15 Rashid Yusuf Mshenga amesema kuwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar hauna uhalali kwa kuwa Zanzibar hawakupewa mkataba.

  "Muungano huu ni ‘verbal' tu, ni wa kuchanganya mchanga tu wan chi mbili, lakini ukiuliza Mkataba wa muungano haupo. Tunataka muuungano huu upitiwe upya" alisema Mshenga.

  Alisema kuwa upande wa Tanzania bara walipata mkataba wa Muungano uliokuwa umesainiwa, lakini upande wa Zanzibar mkataba huo haukupatikana hali inayotia shaka katika muungano, "Wenzetu bara, Spika wa kwanza Adam Sapi Mkwawa na Pius Msekwa walibaki na nakala ya Mkataba, lakini Zanzibar hakukuwa na Barza la Mapinduzi lililokaa kujadili muungano. Hata Mzee Aboud Jumbe alipoingia madarakani alikiri kuwa hakukuwa na mkataba" alisema Mshenga.

  Alisema kuwa harakati za kundi hilo zilianza tangu mwaka 2005 kwa kuishitaki Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili ionyeshe mkataba wa muungano na ndipo Mwanasheria mkuu wa SMZ alipokiri kuwa hana mkataba huo.

  Alisema kuwa hata mwanasheria mkuu wa Zanzibar wa kwanza Dourado amethibitisha kuwa hakupewa makataba wa Muungano wala Katibu mkuu wa kwanza Baraza la Mapinduzi naye hakuhusishwa kwenye mkataba huo wa muungano, hali inayoonyesha kuwa Muungano huo haukuwa na uhalali.

  Alisema kuwa baada ya kuthibitisha kuwa hakuna mkataba ndipo walipoandika barua Ofisi za Umoja wa Mataifa.

  "Tuliandika barua Umoja wa Mataifa Aprili 2010, lakini kwakuwa hawakutujibu, tumewaandikia nyingine kuwakumbusha. UN wanapaswa kusimama kama waamuzi katika suala hili" alisema. Alisema kuwa mara Umoja wa Mataifa watakapowajibu, watafungulia kesi SMZ ili kutaka muungano ujadiliwe upya.

  Mbali na Umoja wa Mataifa, Machenga alisema kuwa nakala ya barua hiyo pia ameipeleka katika balozi za nchi za Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Nchi huru za Afrika.


  Machenga alishangazwa na Serikali ya Muungano na SMZ kuweka kamati ya kushughulikia kero za Muungano wakati hata Mkataba wa muungano haupo akisema kuwa hiyo ndiyo kero ya kwanza.


  "Kamati ya kushughulikia kero za muungano inaundwa na makada wa CCM, kama Waziri mkuu na viongozi wa SMZ, wote hawawezi kuhoji mambo muhimu".

  Machenga alishauri kuwa ili kupata uhalali wa Muungano, Serikali ya Muungano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waunde timu za kuujadili muungano kasha iitishwe kura ya maoni ili wananchi waamue muungano wanaoutaka.


  Kuhusu uhalali wa kikundi hicho alichosema kuwa kinawawakilisha Wazanzibari wote, Machenga alisema kuwa wanaamini kuwa Wazanzibari wengi wanawaunga mkono kwakuwa hukumu ya kesi iliyothibitisha kutokuwepo kwa mkataba wa muungano imeungwa mkono na Wanzibari wengi.


  Hata hivyo alisema kuwa hawatawahamasiaha Wazanzibari kwa maandamano kupinga muungano akisema kuwa hilo ni suala la kisheria hivyo wataendelea kufuata sheria tu.

  Naye Sheikh Farid Hadi Ahmed aliyechana nakala ya muswada wa marejeo ya Katiba katika kongamano la kuujadili hivi karibuni, alisema kuwa hadi sasa hakuna muungano, ni maigizo tu.

  Akizungumza nyumbani kwake Darajani mjini Zanzibar, Sheikh Ahmed alishauri kuwepo na kura ya maoni ili kutafuta uhalali wa muungano.

  "Muungano umeshakufa, tangu walipokufa Karume na Mwalimu Nyerere, hakuna tena muungano. Cha kufanya sasa ipigwe kura ya maoni ili tuone kama wananchi wanautaka muungano"

  Alisema kuwa muungano uliopo sasa haukuwa na uhalali kwakuwa wananchi hawakushirikishwa,
  "Karume na Nyerere walikuja na kuwekea saini bila hata kuwashirikisha wananchi.hakuna aliyeweza kuhoji wakati ule kwakuw ailikuwa ni ubabe tu" alisema.

  Aliufananisha muungano huo na muungano wan chi za Ulaya akisema kuwa Muungano unatakiwa uvutie siyo ulazimishwe,
  "Kitu chochote kizuri kinavutia watu kuja. Angalia Jumuiya ya Ulaya, nchi nyingi zinaomba uanachama, lakini huu muungano wetu wa kulazimisha. Kama kweli kulikuwa na umuhimu wa kuungana, mbona tusiungane na Uganda na Kenya? Kwanini Zanzibar tu? alihoji Sheikh Ahmed
   
 2. H

  Hamisi M Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napata mkanganyiko, ikiwa kuna uhalali wa muungano kwanini mkataba unabaki kuwa siri na hauwekwi wazi kwa wanachi.
  Kwanini? Viongozi wa ngazi za juu ndio wanaoupigiadebe muungano wakati masuala waliyokubaliana waasisi wa muungano hawayaweki hadharani.
  Kwa nini kila mwaka ktk sherehe z muungano tunaishia kuangalia gwaride na halaiki ya watoto wa masikini wakizawadia traksut na kofia na kurudia simulizi za historia ya muungano badala ya kujadili chachangamoto za muungano pamoja na kutafuta suluhisho la matatizo na kero za muungano?
   
 3. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu Wakubwa wanajua kuwa hakuna kero za Muungano bali Muungano wenyewe ndio kero na kwa maslahi yao, wameahidi kuulinda kwa hali yoyote ile.
   
 4. H

  Hamisi M Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakuwa wamemua kuulinda kwa maslahi yao binafsi wakumbuke kuwa utatuzi wa kero na takataka za huu muungano feki ndio ndio njia ya busara na sahihi zaidi.
  Wasisubiri yalomkuta ZIN AL ABINE na wenzake.
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Vipeperushi vimetengenezwa na kugawiwa kwa wingi Zanzibar vikihimiza wananchi wasihudhurie sherehe za muungano leo kwa sababu Muungano hauna tija yoyote kwa Wazanzibari.
  Hata hivyo serikali bado inawaomba wananchi wahudhurie sherehe hizo kwa ahadi kuwa kero za Muungano zitatatuliwa zote kwa mujibu wa sheria.

  Source: Radio WAPO kipindi cha PATAPATA
   
 6. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Ni kwanini kila upande wa Muungano unaona mwenzake hafai?
   
 7. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo halitasaidia kwani Zanzibar imejaa wanaofaidi na kuutaka "muungano" kutoka Dar na Tanga walioletwa kwa maksudi. ikijuulikana Wazanzibari wengi hawashughulikii

  Kwa Wazanzibari wengi, hii ni siku ya huzuni, siku walipopokwa nchi yao waipendayo.

  Kwa Wazanzibari wengi, hakuna cha kusherehekea.
   
 8. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi cha Kipima Joto cha ITV ijumaa iliyopita, Dkt.Lwaitama muhadhiri wa UDSM alitoa wito kuwa wengi wanaotaka muungano ufe ni viongozi wa juu ambao wengi wana tamaa ya madaraka huku wananchi wa kawaida wenyewe wakiupenda ila wanaaminishwa muungano ni mbaya. Na akasema pia gharama za kuvunja muungano ni kubwa sana kwsbb kila nchi itahitaji kuwa na jeshi la kulinda mipaka,kuanzisha paspoti,ofisi za kibalozi na pia kutokana na historia yake ni rahisi kujikuta katika mizozano ya marakwa mara na ni kama ilivyokuwa kwa Ethiopia na Eritrea kwa hiyo ni vema tofauti zikajadiliwa wazi kuliko kuficha ficha mambo ambako kunaleta manung'uniko
   
 9. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Wanaotaka ufe sio viongozi peke yao, bali Wazanzibari wengi hawautaki hivi ulivyo ambapo inaonyesha dhahir kuwa nchi moja kubwa imeikalia nyengine ndogo.

  Hizo gharama ambazo Dr. Lwaitama anazizungumzia zinamhusu nini? Kwani kabla ya huu unaoitwa "muungano", kila nchi ikijiendesha vipi?

  Kabla ya Muungano, Zanzibar ilikuwa na kiti chake UN na katika agencies zake kadhaa. Pia ilikuwa na kiti huko Jumuiya ya Madola na itifaki zote za kiserikali.

  Huu si muungano kabisa, unadumu kwa kutumia nguvu za dola tu.
   
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sio kila upande unaona mwenzake hafai! Tanzania Bara hakuna vipeprushi vya kususia sherehe na pia hawajawahi kupeleka kesi yoyote mahakamani dhidi ya Muungano kama walivyofanya Wazanzibari!
   
 11. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  ni kweli mkuu,natazama star tv wana kipindi live cha muungano,kuna jamaa kapiga sim toka zenji anaeleza muungano ulivyochakachuliwa na hata ukitazama vyema picha za utiaji saini zinazo oneshwa ktk tv utagundua kuna uchakachuaji mkubwa.yaonesha km maridhiano hayakufikiwa kama tunavyosoma ktk vitabu vya historia
   
 12. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haaa haaaa! Zanzibar iliyokuwa na kiti UN haikuwa ile ya Sultani wandugu? Mapinduzi tr 12/01/1964, Muungano tr 26/04/1964 baada ya kuhofia kurudi kwa Sultani, kwa hiyo ulikuwa ni muda mfupi kwa Zanzibar kufanya hayo yote!
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Picha imefanyaje?
   
 14. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ila msishangae watu wakijaa! Sirikali yetu inajua jinsi ya kukusanya mamluki ktk shuguli zao
   
 15. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Miaka 47 ndio wanadai hawataki kusherehekea Muungano! Kaaaazi kweli kweli!
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nasema hiviiii,na wauvunjeeee,leo hii ukiniuliza nafidikaje na zanzibar katika maisha yangu ya kawaida ntakwambia sifaidiki na lolote
   
 17. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "mtoto akilia wembe mpe". Ndo akili za viongozi wetu watafuta madaraka wa afrika kuwahadaa na kuwaaminisha watu kuwa "pasipo muungano maendeleo ya zanzibar yatakuwa juu". Hii ni dhana dhahania, na kwa uroho wa madaraka na ubinafsi wa viongozi wa kiafrika, maendeleo ya wazanzibari/watanzania ni kujilimbikizia mali na usitawi wa viongozi/wafalme wa kiafrika. Chuki za kidini, kikanda (zanzibar vs bara), kikabila zimechachushwa na viongozi watakao madaraka kwa kuwaaminisha wananchi watawaliwa kuwa kwa namna hii....maisha yao yatabadilika-kumbe mmmmmmmmmh,ni ndoto za alinache!!!! "kalaga baho" .
   
 18. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa suala la Muungano Watanzania Bara si kweli kuwa wanaupenda ndiyo maana hawajaenda mahakamani ila ni kuwa hawajali. Rais wa Muungano anaonekana wazi ni Rais wa bara japo Nyerere alionekana ni Rais wa Tanzania yote kwa matendo. Watu wa Zanzibar kwa sababu ya kufanana mitizamo ni rahisi kuamua maamuzi yanayofanana tofauti na bara. Wazanzibari ni wachache na unapozungumza suala la nchi yao wanaacha kutazama "Yanga na Simba" wanakusikiliza unachosema. Huku bara mambo ni tofauti kidogo. Huku bara Maaaskofu na Masheshe wakisema "acheni!" ni rahisi watu kusikiliza bila kuweka maswali mengi (kama ilivyokuwa imani katika dunia ya nchi za kiarabu ambayo sasa inaanguka), Zanzibar wanamsikiliza yule anayesema yale wanayoamini tu na si U-Shehe wake.
   
 19. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Zanzibar hawakuhofia kurudi kwa Sultani kwa sababu sio wao waliofanya Mapinduzi, ni Nyerere aliyefanya Mapinduzi usiku wa January 11, 1964 kutumia Special Forces na kulazimisha Muungano. Note that!
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hawana ujanja hao! watabebwa na malori na kupewa buku 2 na kofia tu....walau leo wasahau bagarashia watinge cap za chama cha Magamba....
   
Loading...