Madai ya kuondoa CCTV Camera: Wahusika mpaka sasa wameshindwa kutoa ufafanuzi wala kukanusha

Kwa ufupi kamera hizi kazi yake ni kuchukua taarifa tu kisha taarifa hupelekwa kwenye kifaa maalumu kwaajili ya kutunzia taarifa,pia huunganishwa kwenye screen maalumu kwaajili ya kuonyesha live perfomance za mijongeao ya mahali.
Mimi nawaona wajinga waliotoa kamera,njia waliyotumia kupoteza ushahidi ni ya kitoto sana.
Mimi nimewahi kuwa CCTV & CONTROL ROOM OPERATOR nina experience kidogo ya mambo haya.
Kwakuwa akili yao ni ndogo na Mbowe kadokeza kuhusu zile CAMERA basi kitakachofuata kwao ni aidha kupinga kwamba hapakuwahi kuwa CCTV CAMERA mahali pale wakati wa tukio , , mbinu yao ya pili katika kujitetea ni kuziweka kamera mpya usiku chini ya ulinzi mkali wa watu wasiojulikana.
Ningeanika hapa njia nzuri ya kuficha ushahidi wa CCTV CAMERA ila hawa watu wanaweza wakaitumia siku nyingine kwenye tukio jingine.
 
Ni wazi wamekosa utetezi au wanahofia kuibua mjadala zaidi kama sio kuhofia maswali ya waandishi.

Hili jambo linahitaji majibu kutoka kwa wahusika tofauti na hapo huu utakuwa ni ushahidi tosha wa kimazingira kuwa kuna jambo haliko sawa.

Ingekuwa ni utaratibu wa kawaida bila shaka wangeshajitokeza hadharani na kutupa mifano ya maeneo mengine ambayo utaratibu kama huo ufanyika au hata kutaja sehemu ambayo camera hizo zimekuwa zikipelekwa na pengine kutoa vielelezo vya makabidhiano au matengenezo,n.k .

Kama wanafunga camera mpya basi tunatarajia wangetoa document za manunuzi au document zinazonyesha kuwa hizo camera zinapaswa kubadilishwa pamoja na nyaraka za camera mpya zilizofungwa maana sidhani kama nyumba za viongozi zinaweza kuachwa bila camera za usalama kwa maana ya kuondoa zilizopo wakati za ku-replace hazijapatikana.

Vile vile inawezekana ziliondolewa kwa nia njema tu ya kufanya uchunguzi au kuhifadhi au kulinda ushahidi ila kwa mtazamo wangu walichokosea ni kufanya hivyo bila kushirikisha upande wa pili maana teyari kuna hali ya kutoaminiana.

Binafsi nilitarajia kama camera hizi zilinasa chchote basi umma ungedokezwa mapema kuwa camera hizi zilinasa tukio lile na kwamba wanatarajia zitasasaidia uchunguzi na leo hii sidhani kama mh.Mbowe angehoji jambo hili.

Lakini pia kama camera zilinasa sura za wahusika ni vzuri sura hizo zikawekwa hadharani ili wananchi wakazifahamu na kusaidia upelelezi.

Anyway,labda wanaandaa majibu hivyo tuwe wavumilivu.


Unataka watoe ufafanuzi gani? ilikuwepo iliondolewa ili zile picha za video zisionekane popote. what do you want?
 
"Wahusika wameziondoa". Inajitosheleza.
Nijuavyo mie kulikuwa hakuna haja ya kuziondoa, cctv camera system inaweza kuhifadhi recorded datas kwenye camera husika na kwenye machine yake DVR au NVR. Kuwa na system hiyo ni pamoja na kurahisisha kazi kwa wapelelez (polisi).
Kuhangaika na dereva wakati kila kitu kimerekodiwa na wana uwezo wa kuiaccess ni kuruhusu watu watilie shaka kwa kujiuliza why, why this etc.Ushahidi wa derva na wengineo ni kujaziajaia tu .
CCTV Camera system is a very true and strong tool of providing evidence.
 
Kumbe sikuhizi hata polisi wakikusanya ushahidi wanatakiwa kumwomba Tundu Lisu au CDM.
Kwa wenzetu , kama picha zilinaswa watuhumiwa sura zao zingewekwa kwenye magazeti na runinga ili wananchi wasaidie kuwapata, naonaga marekani wao mpaka video wanaweka wazi kwa wananchi Tz inaogopa nn
 
Mbona kuna habari kuwa watu ndani ya tisi washatajana na hata Akaeli na wenzake washawajua ila kuwataja hadharani bado inakuwa ngumu kwa sababu za kisheria!
 
Nilitegemea kwa maneno yale ya Mbowe kwenye press conference awe ameshaitwa kuhojiwa mapema,Ina maana zile zilikuwa ni facts tupu imebidi wajipange
 
Back
Top Bottom