MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Hii nchi ina vichekesho vya kushangaza na sio kufurahisha!
Kuna kipindi kila mwanasiasa na hasa wa upinzani alikuwa akipanda kwenye jukwaa analalamika kuhusu baa la njaa ambalo walikuwa wanadai liko mbioni kulikumba taifa wengine wakaenda mbali zaidi na kumtaka Rais atangaze hali ya hatari.
Thread nyingi hapa Jamiiforums za kuanzia mwezi wa Desemba-Januari 2017 zilijaa hoja kuhusu baa la njaa nchini na athari zake.
Rais Magufuli aliposema, hakuna baa la njaa na akasisitiza yeye ni kiongozi pekee nchini mwenye uwezo wa kujua kama kuna baa la njaa au la. Kauli yake ilikoleza moto kutoka kwa wanasiasa.
Wanasiasa walipanda majukwaani na kudai Rais Magufuli ni kiongozi ambaye ana kiburi na hana huruma na pia hajui anachokisema kwa sababu wao wanawasiliana moja kwa moja na wananchi.
Wengine wakaanza kuja na takwimu za upungufu wa akiba ya taifa ya chakula wakidai haitoshi kutokana na baa la njaa linalokabili taifa.
Kuna baadhi ya wanasiasa wakaenda mbali zaidi na kudai kilichotokea mwaka 1983-85 nchini Ethiopia kuhusu baa la njaa kinainyemelea Tanzania.
Baadhi ya viongozi wa dini ''walinasa'' kwenye mtego wa wanasiasa na kuanza kuimba wimbo ya wanasiasa wakiomba serikali itambue kuwa kuna baa la njaa nchini.
Leo hii hakuna tena hoja ya baa la njaa wala wananchi kufa na njaa lakini kikubwa zaidi, wanasiasa waliotaka kutuaminisha kuna baa la njaa hatuwasikii wakileta mrejesho wa hoja zao.
Siwezi kushangaa kama nikiwasikia tena wanasiasa wakisema, wananchi wamekosa soko la kuuzia mazao yao baada ya uwepo wa mazao mengi nchini!
Madai ya wanasiasa kuhusu uwepo wa baa la njaa yanatoa picha/angalizo gani kama taifa?
Hii inatuambia kuwa tuna wanasiasa nchini ambao ni wanafiki, wapotoshaji, waongo au hawana uhakika wa kile wanachokisema.
Hii pia inatoa angalizo kwa serikali kuwa makini kwa kila hoja au madai yanayotolewa na wanansiasa.
Kikubwa zaidi, Madai ya wanasiasa hasa wa upinzani yanampa Rais Magufuli ''ruhusa'' ya kutosikiliza kinachodaiwa na wanasiasa.
Baadhi ya Thread/Mada kuhusu baa la njaa nchini zilizoanzishwa mwezi Dec-Jan 2017;
LINK>>>Ukame umetamalaki sasa, nchi inaelekea kwenye baa la njaa
LINK>>>Taarifa za serikali juu ya baa la njaa nchini zinajikanganya
LINK>>>Baa la njaa na ukame: KKKT waonya upungufu wa chakula nchini
LINK>>>Baa la njaa na ukame: Kanisa Katoliki lawataka waumini kufunga na kuomba mvua
LINK>>>Baa la njaa: Bei za vyakula hazikamatiki, watu washindia maembe