WFP: Njaa itaongezeka baada ya ufadhili kupungua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetahadharisha kuwa kupunguzwa kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu na serikali mbalimbali duniani, kutakuwa na athari chungunzima.

Shirika hilo limeweka bayana kuwa, kupunguzwa kwa ufadhili huo kutalilazimisha shirika hilo kupunguza pia kwa kiasi kikubwa mgao wa chakula kwa watu wenye uhitaji mkubwa.
WFP imeeleza kuwa, kila punguzo la asilimia 1% ya ufadhili linatishia kuwasukuma watu 400,000 kwenye baa la njaa.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu yake mjini Rome limesema punguzo la asilimia 60 ya ufadhili mwaka huu ndio lilikuwa kubwa zaidi katika historia ya miaka 60 ya shirika hilo, na ndio mara ya kwanza kwa shirika hilo kupunguziwa ufadhili licha ya mahitaji kuongezeka.
Kutokana na hilo,

WFP imelazimika kupunguza mgao kwa karibu nusu katika mataifa kama vile Afghanistan, Syria, Somalia na Haiti. Katika taarifa, WFP imetahadharisha kuwa watu milioni 24 huenda wakakumbwa na baa la njaa mwaka ujao.
 
Back
Top Bottom