Mada: Unazangumziaje suala la wazazi waliowatekeza watoto wao kuwatafuta kipindi watoto wao wakishafanikiwa?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Moja kati ya maswali watu wengi huwa tunajiuliza siku zote huyu mzee au huyu mama alikuwa wapi miaka yote hiyo leo ndo anaibuka akitaka atambulike rasmi yeye ndo mzazi halali au biological father au mama.

Haya yote nimeyaleta kwenu tuweze kujadili baada ya kusikia mada hii ikijadiliwa redio moja kuhusiana na swala la wazazi wengi kujitokeza kudai watoto wao kipindi watoto wameshafanikiwa ktk maisha moja katika mijadala hio nilisikia wachangiaji wakizungumza.

1. Kuna mtoto bila kutaja jina mmoja yeye alidai kwa mara ya kwanza alivyojiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baba yake ambaye alipotezana naye muda mrefu aliposikia yupo pale alimtafuta na kumuelezea hali halisi.

2. Mwingine yeye yupo Benki Kuu jina hakutaja ila alimfahamu mama yake akiwa na miaka 31 ambapo alimtafuta kwa juhudi kubwa wafahamiane lakini huyu kijana alidai yeye miaka yote ya utotoni alilelewa na bibi yake, mama hakumfahamu.

3. Mwingine yeye bila kutaja jina lake yupo Uhamiaji; yeye baba yake mzazi alikuwa mstaafu serikalini wa miaka mingi ndo juzi juzi kamtafuta mwanaye.

Lakini, je tatizo liko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kukimbia majukumu ...

Mzee kama huyo ni wa kumsalimia tu mara moja moja...
Maana itakuwa anafata kitu kwako na sio utu.. .

Mama tu ndiye angalau wa kuhurumiwa.. ... ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inakeraa sna mm binafsi ni mhanga mzee alimpa mama ujauzito akiwa kidato cha pili mama alikua sio mwanafunzi enzi hizo.mzeee kaendelea na masomo wakapotezana maana miaka hiyo mawasiliano ilikua shida.so nmekuja kumjua baba nko kidato cha pili 2006 nikiwa na 17 yrs nilifurahi shida ilikuja kwenye huduma za kielimu mzee hakuonesha ushirikiano maana kipindi hicho alikua ni mwl geita na mm nlikua nalelewa upande wa mama mwanz.mzee nkimpigia simu napokua nmekwama mzee anabadili no ya simu so mm na mm tukasema isiwe kesi acha tupambane na hali zetu.nashukuru mungu shule nlisoma kwa shida sana mama hakuwa na uwezo nikamaliza kidato cha sita na division 3 gs nlipata f hivyo nikakosa sifa za kwenda chuo kikuu nkawaza niaply diploma napo nkaangalia hali ya bi mkubwa asingeafford maana alipunguzwa kazi kiwandani.ikabidi niingie kitaaaa kuhusle mpaka sasa nahusle.kimbembe sasa mzeee sasa haishi kunitafuta na kulalamika kua inakuaje mwanae nmemsusa hata simu tu.
 
Huu uzi umenikumbusha yule kijana aliyefaulu vizuri form four mwaka jana au juzi. Baba yake aliwatelekeza tangu akiwa mdogo akaja kuibuka baada ya kijana kutangazwa kafaulu vizuri tena aliibuka kwenye sherehe ya kijana kupongezwa bila hata aibu daah

Msanii domo baba yake alimtelekeza halafu mzee alikua na pesa balaa ila hakuwajali,kaona mafanikio ndio kaibuka na kulazimisha apewe matunzo
 
Yeye kama hakutimiza wajibu wake kwangu kama mzazi mimi sitashindwa kutimiza wajibu wangu kwake kama mtoto. Malipo duniani akhera mahesabu.
 
Back
Top Bottom