MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Usiwe na wasiwasi. Hutokea.

Mnywishe kijiko kimoja cha chakula cha kahawa nyeusi, ile kama ya vijiwe vya gahwa, na asali kijiko kimoja baada ya gahwa. Ataongea baada ya wiki kama chiriku. Usianze tu kumwambia anyamaze.

Kutwa X 3
Asante Faizafoxy so nimnyweshe kwa wiki nzima?
 
Usiwe na wasiwasi. Hutokea.

Mnywishe kijiko kimoja cha chakula cha kahawa nyeusi, ile kama ya vijiwe vya gahwa, na asali kijiko kimoja baada ya gahwa. Ataongea baada ya wiki kama chiriku. Usianze tu kumwambia anyamaze.

Kutwa X 3

Nina jambo kama hilo, insababishwa na nini? So unategeeza hyo gahwa kabisa?
 
1. je alikulia katika mazingira gani?. je, wazazi walikua bize sana na wakamwachia mtoto akuzwe na house girl ambae sii mwongeaji sana na watoto? (mi nimeshuhudia wazazi wakiwa bizy na kazi hadi mtoto anachelewa kuongea).

2. kama ni wakristo... kambatizeni mtoto huyo.. kama mlisha mbatiza... BASI FANYENI MAOMBI NA MUWE NA IMANI... KWA MAANA IMANI YENU NDIO ITAMPONYA HUYO MTOTO.

3. Faidi isiyo rasmi ya mtoto kuto ongea mapema ni kua mtoto hua GREAT THINKER sana... kwamaana akili yake imekua katika internal discussions na sio via mouth. so he will be one of the greatest thinkers. Albert Einstein started to speak when he was 3 years old
fanya uchunguzi mdogo tuu.. utagundua kua watoto wengi waliochelewa kuanza kuongea ndio hua wanakua ma-think tanks. and visionary thinkers. futurists, forward thinkers etc.

4. zaidi ya yote hayo mufanye maombi... kwa maana kuna uwezekano mkuwa sana huyo mtoto huenda amefungwa kuongea na na nguvu za giza.. kama ndio hivyo ... mombi ndio njie effective na ndio ya pekee kutoa hilo tatizo...
 
Mkuu usiwe na wasiwasi ataongea tu muda ukifika--huyo hana tatizo lolote la kiufundi--ni tatizo la kimaumbile tu. Watoto wa kiume huchelewa sana kuongea. Mtoto wangu alianza kuongea akiwa na umri wa miaka 3.5. Mpaka sasa anakaribia miaka 4 lakini bado anaongea kwa kusuasua.

Kipindi hajaweza kuongea, akiwa na tatizo humshika mtu mkono na kumpeleka kwenye friji kisha kuonyesha anachotaka--maji, soda, juice, etc. Niliogopa nikadhani mwananangu ana tatizo lakini kila nikiangalia matendo namuona yupo intelligent sana.

Mtoto wako ataongea tu usiwe na wasiwasi. kuna mtu nilikutana naye akasema watoto wake wote huchelewa sana kuongea--huongea wakiwa na umri wa miaka 5. ni suala la kawaida. brain development differs from child to child. your child will speak eventually.
 
Jihadhali na TV kwa mtoto kuanzia anapozaliwa adi miaka 2. TV zinasababisha mtoto kuchelewa kuongea zinamchanganya asiweze kusikiliza sauti za watu waliomzunguka.

Mtoto hujifunza kuongea kupitia maongezi yanayojiludialudia ndani ya familia au jamii inayomzunguka.
 
Wasiwasi kama mzazi ni lazima uwepo. Lakini kwa uzoefu wangu watoto wa kiume huwa wanachelewa sana kuongea. Mtoto wangu wa kiume aliongea na miaka 3, na nina mjukuu wangu ana miaka 2 na nusu naye hivyo hivyo.

Kama Madaktari wamesema hana tatizo basi endelea kumpeleka shule ajichanganye na watoto wenzie, ataongea tu.
 
Alipata mtindio wa ubongo? vip uchungu ulikaa mda mrefu kwa mama? wahi hospital akafanyiwe evaluayion na speech therapy if possible
 
Usiwe na wasiwasi. Hutokea.

Mnywishe kijiko kimoja cha chakula cha kahawa nyeusi, ile kama ya vijiwe vya gahwa, na asali kijiko kimoja baada ya gahwa. Ataongea baada ya wiki kama chiriku. Usianze tu kumwambia anyamaze.

Kutwa X 3
Celebrity no 1 wa JF,sasa hii inasaidia vipi? tunaomba maelezo ya ziada
 
Celebrity no 1 wa JF,sasa hii inasaidia vipi? tunaomba maelezo ya ziada

Hiyo niliona wazee wakiitumia endapo mtoto amechelewa kuongea, nasi tumerithi huo ujanja na tunafanya hivyo kwa watoto na inasaidia kufanya mtoto aongee. "Inasaidia vipi?",

kwa ufupi, asali inajulikana manufaa yake kwenye tiba za kisasa na za asili sina haja ya kuielezea kwa kirefu, kahawa nayo ni "stimulant" ya enzi na enzi na huwafanya watu waongee sana, ndio maana maneno na habari nyingi za dunia hupatikana katika vijiwe vya gahwa.
 
tall gal,
Alichekiwa chini ya ulimi? Tongue tie?...Kama amechunguzwa na hata tatizo kwenye viungo vyake vya kuongea na kusikia, then tatizo linaweza kua kwenye ubongo....e.g Autism spectrum disorder-ugonjwa huu ni complex mpaka daktari akueleze.....otherwise anaweza kubenefit na speech therapy.
 
Nenda hospital wamcheki kwenye koo lake..kuna uwezekano mkubwa akawa na nyama zimeota kwenye koo hivyo zinamfanya aone usumbufu kuongea....hiyo kitu ilimtokea mtoto wa rafiki yangu,mpk miaka mitatu alikuwa haongei vizuri, walipompeleka hospital wakagundua hivyo.....na moja ya dalili ni kama huyo mwanao, akitaka kitu basi atakuonyesha bila ya kutamka
 
Dalili za "nyama kooni" adenoids ambazo ni ugonjwa common kwa watoto, ni ; snoring/kukoroma usiku na kuhema kwa shida-mouth breathing.(Mtoto anakua anahema na mdomo-mdomo unakua wazi muda mwingi.)...pia yanaweza athiri lafudi na sauti yake..
 
Kweli mmetufungua wengi..wangu anamwaka 1.4 basi mi nimekazana sema baba...sema mama...mwenyewe nahamu kweli ya kusikia akiongea...kumbe bado na nikawaida tu..
Asanteni kwa kutuelimisha
 
Jaribu pia kimchunguza anasikia? anakijua jina lake? anaweza ku-respond instructions ndogondogo? Hii husaidia kujua kama hana tatizo lolote la ukuaji. Halafu kama unamashaka mpeleke kwa Daktari wa watoto (pediatrician). Sio kila Daktari anafahamu kuhusu ukuaji wa mtoto.

Jingine kwenu familia/ ukoo wenu kuna wenye vigugumizi?? Nimeona watoto wenye asili ya vigugumizi walivyochelewa kuongea
 
Naombeni msaada wana jf.

Mtoto ana miaka mitano sasa hawezi kutamka maneno, hawezi kutafuna chakula.Nimejaribu kumfundisha lakini hafuati kile nachomfundisha au naweza sema hana utulivu wakati wa kumfundisha. Nimejaribu kumpeleka kwa madaktari bingwa wa watoto nao wameshindwa kubaini tatizo zaidi wanasema kiakili yupo fit.

Sasa basi naombeni mawazo ushauri wenu nifanyeje juu ya mtoto huyu kwani nami natamani aongee kama watoto wengine wa umri wake. Na kama unamjua daktari ambae anaweza kumsaidia mtoto huyu naomba msaada wenu. Kina mzizimkavu na wengine nasubiri mawazo yenu.
 
Back
Top Bottom