Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Maafisa wa Forodha wa Indonesia wamemkamata rubani msaidizi wa Shirika la Malaysia Airlines, anayetambulika kwa herufi MS0, katika Uwanja wa Ndege wa Soekarno-Hatta tarehe 29 Julai 2026 kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa Forodha ya uwanja huo, ukaguzi ulibaini takriban kilo 26 za ecstasy, sawa na vidonge 70,114, pamoja na gramu 4 za methamphetamine zilizofichwa ndani ya begi lake.

Mamlaka zimesema ukamataji huo ulitokana na upitiaji na uchunguzi wa X-ray, licha ya mtuhumiwa kupita awali kwenye njia ya haraka ya forodha.

Forodha ya Soekarno-Hatta imetoa pia video ya CCTV ikionesha mchakato wa ukaguzi na ukamatuzi mara baada ya mtuhumiwa kushuka kutoka ndege ya Malaysia Airlines.

Pia ilikamatwa chupa ndogo yenye mkojo ambayo wachunguzi wanaamini ilikusudiwa kutumika kuharibu matokeo ya vipimo vya dawa za kulevya.

Mtuhumiwa amekabidhiwa kwa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai cha Polisi wa Kitaifa wa Indonesia kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria kuhusiana na tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya.
1785826098088.jpg
 
Ndege ya Shirika la All Nippon Airways (ANA) aina ya Boeing 767 ililazimika kusitisha kutua (go-around) mara mbili mapema leo katika Uwanja wa Ndege wa Haneda, Tokyo, baada ya karibu kugongana na ndege ndogo ya CitationJet ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Japan.

Kwa mujibu wa data ya ADS-B, tukio hilo lilitokea wakati ndege ya ANA ikiwa katika hatua za mwisho za kutua.

Ndege ya CitationJet ilivuka mbele ya njia ya kutua, na kusababisha mfumo wa onyo la migongano angani TCAS kutoa tahadhari kwa rubani wa ndege ya 767.

Rubani alifanya maamuzi mara moja kwa kupandisha ndege na kughairi kutua. Ndege hiyo ililazimika kuzunguka na kujaribu kutua tena, lakini ilifanya 'go-around' ya pili kabla ya kutua salama baadae.

Data zinaonyesha ndege hizo mbili zilikaribiana umbali wa maili 0.776 na futi 100 kwa wima.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Japan imesema uchunguzi umeanza ili kubaini jinsi ndege ya CitationJet ilivyovuka njia ya kutua bila ruhusa.

Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
1785827923790.jpg
 
Netflix inatarajiwa kutoa filamu mpya ya dakika 93 iitwayo "Freefall: A Reckoning for Boeing" ambayo inachunguza madai ya kupuuza usalama katika kiwanda cha Boeing cha Charleston, South Carolina.

Filamu hiyo, iliyotayarishwa na Rory Kennedy, inaangazia urithi wa John Barnett, meneja wa ubora wa Boeing kati ya 1985 hadi 2017, ambaye alijipiga risasi na kufariki Machi 2024 wakati wa kesi dhidi ya kampuni hiyo.

Barnett alikuwa ameibua wasiwasi kuhusu utamaduni wa usalama Boeing, ikiwemo mfumo wa oksijeni.

Wafanyakazi wengine wa Boeing nao wamesema walipata vitisho baada ya kuzungumza kuhusu ubora duni, huku baadhi wakisema sehemu za ndege zilikuwa "zimeoza" kabla hazijafungwa.

Dokumentari hiyo pia inaunganisha madai ya Barnett na tukio la Alaska Airlines 1282 mwezi Januari 2024, ambapo mlango wa ndege ya Boeing 737 MAX 9 uliruka angani na barakoa za oksijeni ziliripotiwa kutofanya kazi.

Boeing haijatoa maoni rasmi kuhusu filamu hiyo mpya.
1785831951104.jpg
 
VESTMANNAEYJAR, ICELAND — Mamlaka ya Usafiri ya Iceland imewafungia leseni marubani wawili wa shirika la ndege la Icelandair baada ya kubainika walikiuka taratibu za usalama kwa kushusha ndege ya abiria chini ya kiwango salama cha kimo cha anga.

Matukio hayo yalitokea tarehe 11 Aprili wakati wa safari ya mwisho ya kustaafu kwa rubani mkuu wa ndege hiyo aina ya Boeing 757-200.

Rubani huyo mkuu aliamua kuipitisha ndege hiyo kwa kimo cha chini sana juu ya mji wake wa nyumbani uliopo katika visiwa vya Vestmannaeyjar ili kuaga familia na marafiki, jambo ambalo lilirekodiwa na kusambazwa mtandaoni na wakazi wa eneo hilo.

Uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Miundombinu ukishirikiana na mamlaka za usafiri umebaini kuwa marubani wote wawili walionyesha uzembe mkubwa unaohatarisha usalama wa abiria na watu waliopo ardhini.

Kutokana na uzembe huo, rubani mkuu amepokonywa leseni yake ya kurusha ndege kwa muda wa miezi 24, huku rubani msaidizi akifungiwa kwa miezi 12 baada ya kuwa likizoni kwa muda mrefu kupisha uchunguzi huo.

Uongozi wa shirika la ndege la Icelandair umethibitisha kukamilika kwa uchunguzi wao wa ndani na kusisitiza kuwa usimamizi wa kampuni hiyo haukuwa na taarifa wala haukutoa kibali cha kufanya maonyesho hayo ya hatari angani.

Licha ya kwamba marubani hao wanayo haki ya kukata rufaa kupinga adhabu hiyo, wachambuzi wa mambo ya anga na jamii ya usafiri wa ndege wamelaani kitendo hicho na kukitaja kama ukiukwaji mkubwa wa nidhamu ya kazi.
1785840266173.jpg
 
Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limekuwa mstari wa mbele katika kuishereheshea Kenya kwa kuwasafirisha nyumbani mabingwa chipukizi wa tenisi wa umri wa chini ya miaka 12, baada ya kushinda Mashindano ya Kanda ya Afrika Mashariki ya WT/CAT.

Timu hiyo iliondoka jijini Dar es Salaam kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tarehe 3 Agosti 2026, ikiwa imepeperusha bendera ya taifa baada ya kutwaa ushindi huo.

Timu ya wavulana ilifanikiwa kutetea taji lake la ubingwa kwa kuwashinda wenyeji Tanzania kwenye fainali, huku wasichana wakijinyakulia medali ya shaba.

Wakati wa kuwasili nchini Kenya, mabingwa hao walipokelewa kwa shangwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na viongozi wa michezo, wazazi na mashabiki.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa KQ alisema shirika hilo limejivunia kuwa sehemu ya safari ya mashujaa hao na kuendelea kuunga mkono vipaji vya vijana kupitia usafiri wa anga wa uhakika kanda nzima ya Afrika Ma
1785852126363.jpg
shariki.
 
Ndege ya michezo ya angani aina ya Yakovlev Yak-55M yenye nambari ya usajili N55YA ilipata ajali mbaya na kupinduka juu chini katika Uwanja wa Ndege wa Quonset State Airport uliopo North Kingstown tarehe 10 Agosti 2024.

Ajali hiyo ilitokea baada ya ndege hiyo kupata hitilafu za kimitambo kwenye injini wakati ikipaa, jambo lililomlazimu rubani kurejea uwanjani hapo kwa dharura.

Wakati wa kutua rubani alipoteza udhibiti wa uelekeo na ndege ikatoka nje ya njia ya kuruka kabla ya kugeuka na kupinduka barabarani. Kwa bahati nzuri rubani alinusurika na majeraha madogo tu.

Ripoti ya mwisho ya uchunguzi kutoka Bodi ya Usalama wa Usafiri wa Anga ya Marekani (NTSB) imebainisha kuwa sababu kuu ya ajali hiyo ni ukosefu kamili wa uzoefu wa rubani katika urushaji wa ndege hiyo pamoja na uamuzi wake wa kutua kuelekea upande uliokuwa na upepo wa nyuma "tailwind" uliovuruga udhibiti.

Kwa mujibu wa NTSB siku ya ajali ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwa rubani huyo kupaa na kurusha ndege hiyo ya Yak-55M baada ya kuinunua karibuni, na hakuwa amewahi kufanya mazoezi yoyote ya kupaa au kutua na chombo hicho.

Kumbukumbu za safari zake zilionyesha kuwa alikuwa na masaa 49.4 tu ya urubani katika maisha yake yote.

Pia hakuwa na uzoefu wowote uliorekodiwa wa kuendesha ndege zenye mfumo wa gurudumu la nyuma "Tailwheel" au maarufu kama "Aviator" ambazo zinajulikana kuwa na changamoto kubwa na zinahitaji mbinu maalum wakati wa kutua.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa rubani huyo alikuwa akifanya safari hiyo bila kuwa na leseni rasmi wala vyeti halali vya urubani vinavyomruhusu kisheria kurusha ndege hiyo.
1785866679646.jpg
 
Ndege ya shirika la Kenya Airways, yenye safari nambari KQ784, imepata ajali ya kupasuka gurudumu wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town nchini Afrika Kusini.

Tukio hilo limetokea leo Jumanne, Agosti 4, 2026, ambapo abiria na wafanyakazi wote wa ndege hiyo waliteremshwa salama na hakuna majeraha yaliyoripotiwa.

Kufuatia tukio hilo, uwanja wa ndege wa Cape Town ulilazimika kufunga njia kuu ya kurukia na kutua ndege kwa sababu ndege hiyo ilikuwa bado ipo kwenye eneo la tukio ikifanyiwa matengenezo.

Hali hiyo imesababisha ndege zote zilizokuwa zikiwasili kuelekezwa kwenye viwanja mbadala, huku safari za kimataifa za kuondoka zikiwa zimesitishwa kwa muda, ingawa safari za ndani ya nchi bado zinaendelea.

Shirika la Kenya Airways limetangaza kufuta safari ya kurudi ya KQ785 kutoka Cape Town kwenda Nairobi ili kuruhusu mafundi kukamilisha ukaguzi na matengenezo ya ndege hiyo.

Kampuni hiyo imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwahakikishia abiria walioathirika kuwa timu yao ya huduma kwa wateja inawasiliana nao ili kuwapa usaidizi na mipango mbadala ya usafiri.
1785866745005.jpg
 
TAARIFA YA RATIBA YA MIKUTANO YA HADHARA YA MAKAMU MWENYEKITI BARA MH. JOHN HECHE NDANI YA MKOA WA MARA

1. Tarehe : 6/8/2026- SIRARI.

2. ⁠Tarehe: 7/8/2026 -SHIRATI

3. ⁠Tarehe: 8/8/2026- MUSOMA MJINI.

#KATIBAMPYA#FREETUNDULISSU
1785934142303.jpg
 
Shirika la ndege la Uganda Airlines limezindua rasmi safari mpya za ndege kutoka Entebbe kwenda Kigali nchini Rwanda na Accra nchini Ghana, zilizopangwa kuanza rasmi mnamo Novemba 2026.

Safari za kwenda Kigali zitakuwa za kila siku kwa kutumia ndege za Bombardier CRJ-900, wakati safari za Accra zitakuwa mara nne kwa wiki kwa kutumia ndege ya Boeing 737-800.

Upanuzi huu unalenga kukuza biashara, utalii, na kuongeza ushindani wa usafiri wa anga kati ya ukanda wa Afrika Mashariki na Magharibi.

Hatua hiyo inakuja kufuatia mpango wa shirika hilo kununua ndege mpya nane (08) kutoka kampuni ya Boeing ili kuongeza ufanisi wa huduma zake.
1785934204839.jpg
 
Mamlaka nchini Ujerumani zimeanzisha uchunguzi wa ugaidi kufuatia ugunduzi wa ndegenyuki "drone" iliyobeba vilipuzi kando ya ndege ya mizigo ya Ukraine katika Uwanja wa Ndege wa Leipzig/Halle usiku wa jumanne.

Kifaa hicho, maarufu pia kama 'kamikaze drone' kilichotambuliwa na mfanyakazi wa uwanja wa ndege, kilishindwa kulipuka kutokana na hitilafu ya kiufundi na hakikusababisha madhara, huku kukiwa na uhusiano wa kimkakati wa uwanja huo kama kitovu cha misaada ya kijeshi ya NATO kwenda Ukraine.

Maafisa wa Ukraine wameashiria kuhusika kwa Urusi kufuatia tukio hilo, ambalo linakuja huku kukiwa na maonyo ya kijasusi kuhusu kampeni za mashambulizi mseto ya Urusi dhidi ya Ulaya.

Uwanja wa Ndege wa Leipzig/Halle umekuwa ukilengwa, huku ndegenyuki hiyo yenye kilipuzi ikionyesha hatari zinazoendelea kwa miundombinu ya usafirishaji.
1785943256528.jpg
 
Back
Top Bottom