Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Kipande cha roketi ya Falcon 9 kimegonga uso wa Mwezi, lakini inaweza kuchukua muda kabla ya watafiti kuweza kutathmini kikamilifu matokeo na athari za mgongano huo
-
Wanasayansi wanaweza kujifunza nini baada ya sehemu ya roketi hiyo kugonga Mwezi?
-
Pangusa kushoto kufahamu zaidi
-
-
-
#bbcswahili #spaceX #falcon9 #angazambali #sayansiyaanga
1786079404175.jpg
1786079400983.jpg
 
HII NDEGE INDIGO AVIATION IKO ZANZIBAR WATU WANAFANISHA NA HII YA DAR HII NDIO ILIFANYA KAZI SANA DAR ZANZIBAR PEMBA NA SEHEMU NYINGINE NITAWALETEA STORY YAKE
1786114592381.jpg
 
Ndege ya shirika la Air India iliyokuwa ikitokea Phuket kuelekea Delhi ilikumbana na mtikisiko mkubwa wa ghafla angani uliodumu kwa dakika nne hadi tano na kusababisha majeraha kwa watu 17 baada ya ndege hiyo kushuka ghafla kwa urefu wa futi 300.

Waziri wa Usafiri wa Anga wa India, K Rammohan Naidu, alithibitisha kuwa tukio hilo lilitokea kwenye ndege aina ya Airbus A320neo ikiwa safarini na abiria 137 na wafanyakazi 08 wa ndege.

Chanzo cha mtikisiko huo kimebainika kuwa ni aina ya mtikisiko wa hewa safi ambao hauwezi kugundulika kwa urahisi na rada za hali ya hewa za ndege hiyo.

Kutokana na nguvu ya mtikisiko huo, abiria na wafanyakazi ambao hawakuwa wamefunga mikanda walirushwa hadi kwenye dari la ndege na kusababisha uharibifu wa baadhi ya vifuniko vya juu vya kuhifadhia mizigo.

Jumla ya abiria 13 na wafanyakazi 4 walijeruhiwa vibaya, ambapo baadhi ya wafanyakazi wa ndege na abiria walipata majeraha makubwa ya uti wa mgongo na shingo lakininqahidumu waliendelea kuwahudumia abiria hadi ndege ilipotua salama mjini Delhi.

Baada ya kutua, majeruhi walikimbizwa hospitalini kwa matibabu huku mamlaka ya usafiri wa anga ikisitisha safari za ndege hiyo na kuanza uchunguzi rasmi kwa kutumia vifaa vya kurekodi sauti na data za safari hiyo ili kubaini undani wa tukio hilo.
1786130116871.jpg
 
Back
Top Bottom