Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kimeshinda Tuzo ya Kiwanja Bora Barani Afrika katika Tuzo za World Travel Awards (WTA) 2025.
Tuzo hizo zilitolewa usiku wa Juni 28, 2025 katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
JNIA imewashinda wapinzani wake wakuu wakiwemo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Cape Town (Afrika Kusini), Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta (Kenya), na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha O.R. Tambo (Afrika Kusini), katika kipengele cha "Africa’s Leading Airport 2025"
Tuzo nyingine ni;
Africa’s Leading Balloon Ride Operator – Miracle Experience – Balloon Safaris Tanzania
Africa’s Leading Destination – Tanzania
Africa’s Leading Tourist Board – Tanzania Tourist BoardAfrica’s
Leading Beach Destination – Zanzibar
Africa’s Leading Honeymoon Destination – Kitulo National Park
Africa’s Leading Tourist Attraction – Ngorongoro Conservation Area
Africa’s Leading National Park – Serengeti National Park
Africa’s Leading Big 5 National Park – Serengeti National Park
Africa’s Leading Mountain National Park – Kilimanjaro National Park
Africa’s Leading Cultural National Park – Ruaha National Park
Africa’s Leading Scenic National Park – Nyerere National Park
Africa’s Leading Elephant Paradise National Park – Tarangire National Park
Africa’s Leading Cruise Port – Port of Dar es Salaam
Tanzania’s Leading Tour Operator – Altezza Travel
Africa’s Leading Adventure Tour Operator – Zara Tanzania Adventures
Africa’s Leading Tour Operator – Pollman’s Tours & Safaris
Tuzo hizi hutolewa kila mwaka na World Travel Awards kwa lengo la kutambua taasisi zinazotoa huduma bora na za viwango vya juu katika sekta ya usafiri na utalii duniani, zikiwemo viwanja vya ndege, mashirika ya ndege, hoteli na kampuni nyingine za usafiri.