Wakati wa majaribio ya ardhini mnamo 2017, Injini ya GE9X ilitoa matokeo ya kushangaza ya nguvu ya pauni 134,300 (597.396 kN) na kuweka rekodi mpya ya ulimwengu iliyotambuliwa rasmi na kitabu cha kumbukumbu za Dunia cha Guinness World Record.
Moja ya ndege kubwa zaidi ya abiria duniani, Boeing 777X, inatarajiwa kuanza kutoa huduma mwaka 2026 huku shirika la ndege la Ujerumani, Lufthansa, likiongoza shughuli za uzinduzi.
Ndege hiyo, ambayo ni mradi mkubwa zaidi wa ndege za kibiashara wa Boeing, imesimikwa GE9X, injini kubwa zaidi ya ndege za kibiashara duniani.
Toleo la Boeing 777-9, ambayo inaweza kuchukua zaidi ya abiria 425, inapita urefu wa Boeing 747-8 na Airbus A380 ya ghorofa mbili.
Injini za GE9X, kila moja ikiwa na uzito wa takriban pauni 21,000 (Sawa na tani 9.5) na kipenyo cha inchi 184 kwa ujumla, inaonesha mageuzi ya kazi bora ya teknolojia katika uhandisi wa anga.
Kipenyo cha feni kina urefu wa inchi 134, inchi 6 zaidi ya injini za GE90 zinazotumia ndege ya sasa ya Boeing 777-200 na 777-300.
Wachambuzi wa sekta ya anga wanajadili kuwa, nguvu ya upepo inayozalishwa na injizi za GE9X inaweza kuangusha kirahisi Gari kubwa ikiwa inakatiza nyuma yake.
Injini hizo 02 pacha za B777X zinatoa faida ya nguvu sawa ikilinganishwa na ndege nyingine kubwa za kibiashara zenye injini 04 kama vile Airbus A380 na Boeing B747-8.