Mada maalum: Tuijadili Tanganyika

Viongozi wachuuzi na wapenda pesa, hawana cha kupoteza na kitu kinaitwa Tanganyika au muungano

Wanauhakika wa kuhama nchi pindi inapobidi, kwa hiyo huwezi kuwaeleza wakaelewa kama wanaharibu mahali

Wao kwao, Tanganyika au muungano si kipaombele chao, bali ni wapi zilipo pesa wapige?

Tunatokaje hapo?

Ni wanyonge waliochoka kabisa kulipishwa kodi na hawaoni zinafanya nini zaidi ya kuwaletea maumivu tena

Kunyang'anywa hata kile kidogo walichonacho

Nachukulia mfano,

Machinga huwa ni mtu anayetumia jasho na damu kupata ridhiki lake, lakini amewekewa mgambo wa kumsaka, na akimpata anamnyang'anya mali zake anabaki masikini na asijue atapata vipi tena, na wakati huo huo anawatoto, maana yake, yeye na kizazi chake chote, hakiwezi kuondokana na umasikini

Watu kama hawa, bila kujali imani zao, tuungane, tuyachukue haya mateso tunayopitia, tuunganishe nguvu, tumlilie Mungu ili atupe njia sahihi za kudili na ukandamizwaji huu

Na ama Tumwambie Mungu aanze kuwanyofoa mmoja baada ya mwingine ambao wamekuwa wanyonyoji wa nchi hii
 
Watu kama hawa, bila kujali imani zao, tuungane, tuyachukue haya mateso tunayopitia, tuunganishe nguvu, tumlilie Mungu ili atupe njia sahihi za kudili na ukandamizwaji huu
 
Ukiona watanganyika hawatakiwi kumiliki ardhi Zanzibar lakini wao wanamiliki Tanganyika, uongozi vivyo hivyo. Nyerere alitukosea watanganyika,hatupaswi kuendelea na kosa hili tukatae kabisa
 
Tanganyika Kwa Sasa Tanganyika inatawaliwa na mkoloni CHURA KIZIWI
 
Tupiganie sana Katiba Mpya ambayo itaipa Tanganyika nafasi yake na Uhuru wake.
 
 
Kwahiyo naamini kwa wakati ule,maamuzi waliyofanya akina comrade Nyerere na comrade Karume yalikuwa maamuzi sahihi kutokana na mahitaji ya wakati ule
Fair enough!
Sasa kizazi baada ya uhuru tunaona hawa wazee walifanya makosa,lakini hatupaswi kuwalaumu bali tunapaswa kutafuta njia ya kutatua mapungufu ambayo yamejitokeza
-Njia ya kutatua matatizo ni mbovu. Kwamba kuna 'kero' za Wazanzibar, wasikilizwe na kutekelezewa
-Njia ilikuwepo kupitia serikali 3 na mambo 7 ambayo Tanganyika ingewasaidia Wazanzibar. Yes, ingewasaidia kwasababu hakuna kitu hata kimoja Tanganyika inaweza kusema imepata katika Muungano
-Njia inayotumiwa na viongozi kudai kuna serikali ya Muungano inajadiliana na ya Mapinduzi ni Utapeli.
Ndani ya SMT wapo Wazanzibar, hao ndio wanakwenda kujadili jambo na SMZ.
-Njia zinazotumika za kuwafanya Wazanzibar raia special wa Tanzania ni mbaya.
 
Moja wapo ni huu wa kwetu,waazilishi waliamua kuwa na aina hiyo ya Muungano,kwamba kila upande utakuwa na Raisi wake na bendera yake
Pande zipo ngapi?
Kwahiyo mimi na wewe tumeyakuta hayo,kama haturidhiki basi tutafute namna ya kupaza sauti na kurudisha Tanganyika yenu
Hivi unataka sauti zipi tena! kwamba huoni au hujasikia!
Kama wakubwa hawaoni haja ya kufanya hivyo na waona la kheri ni kuendelea kutatua changamoto kama wanavyofanya siku zote,basi tukae kwa kutulia
Changamoto zipi zimetatuliwa?
 

Tanganyika ina matatizo mengi makubwa ya kutengezwa., ambayo ni lazima tuyatatue ili Tanganyika isife na ipate maendeleo ya vitu na watu.

Maja ya matatizo hayo ni MUUNGANO. Huu Muungano kama ulivyo umekua UKIIKABA KOONI Tanganyika ili ife.

Aina ya Muungano inayokubalika ni wa;
1. Serikali moja, AU
2. Serikali tatu.

Vingevyo muungano uvunjwe.
 
Shida Ina anza vizee vyenyewe vilivyoipigania Tanganyika haviipendi Tanganyika!Mzee kama Wasira hata upigigie mbuzi gitaa haelewi kitu plus maccm mengi tu! Tanganyika inapendwa na kupiganiwa na Kizazi kipya ambacho hata hakijazaliwa kipindi hicho!Maccm yako mengi bungeni kama yangekua na uchungu na Tanganyika Kwa nini yasipeleke hoja wajadili hatma ya Tanganyika???Mimi ndio maana wazee wa Tanganyika hata akinipa ushauri natamani nimpe dole la kati tu qmmk!!!
 
Tanganyika izinduliwe tu maana ipo tayari. Kila kilichopo ni cha Tanganyika, lakini kinaitwa Tanzania ili Zanzibar wapate access.
 
Chadema chakavu mookua mtaacha. Kwa Sasa akili zenu Bado ni za kitoto hivyo vinyuzi vyenu vilivyojaa ukomedi vinapotezewa tu na wenye akili......ishieni kujibizana wenyewe na kufirahi Huku mkiwa hamna furaha basi siku iende.

Nje ya mada; nasikia mwamba mgao wa tone tone anapelekewa kulekule selo, ni kweli hii?!!!!
 
Mi huwa nahisi Karume alimtrick Julius, Mwalimu alipigwa zile janja janja za sungura,
 
Tunatakiwa kuidai Tanganyika waziwazi bila Kuona haya, tukaidai hadi UN na mahakama za kimaraifa haiwezekani mgeni aje afuje Mali zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…