Mada maalum: Kuelekea tarehe 01/06/2019 | Nini mbadala wa mifuko ya plastiki?

Nina shamba limepakana na mnada huko Singida kila tar sita huwa na mnada,wakiondoka naachiwa plastiki nyingi kuliko hizo zilizopigwa marufuku hadi zinakera watu wa mazingira tutembeleeni na sisi wa vijijini
Sasa wanazuia mifuko ya plastic, ilihali kuna bidhaa nyingi ambazo vifungashio vyake ni plasric, swali ni je, zikishatumika kwani hazitaacha plastic kibao zikizagaa mtaani?
 
Na ukizingatia tunaelekea kwenye uchaguzi wa mitaa kisha uchaguzi Mkuu mwakani kubadilisha gia hewani ili kupata kiki inawezaekana,mfano mzuri kwenye tinted na vikokoto
Na utasikia maandamano yakiitishwa ili kupongeza juhudi za mheshimiwa katika kujali wanyonge wasioweza kuhimili gharama za vifungashio vipya!!!
 
Nina shamba limepakana na mnada huko Singida kila tar sita huwa na mnada,wakiondoka naachiwa plastiki nyingi kuliko hizo zilizopigwa marufuku hadi zinakera watu wa mazingira tutembeleeni na sisi wa vijijini
Wamekusikia
 
Majani ya migomba inatumika vizuri tu kwa kuhifadhia vyakula
Migomba ni michache kwa ukubwa wa nchi.İnabidi maeneo yote yaafayo kilino cha migomba wapande migomba kwa wingi sana kwa industry ya mifuko.kigoma, mara, moro arusha wsboreshe kilimo cha migomba kama mby kagera, moro na kilimanjaro.
 
Zamani kulikuwa na mifuko ya karatasi, uswahilini ilikuwa ikitengezezwa kutumia mifuko ya saruji.....
 
Habari JF.
Kama mjuavyo tarehe 01/06/19 ndiyo mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki humu nchini.
Je ni upi mbadala wa mifuko hii ili kutoleta adha kwa wafanyabiashara na wateja ktk maeneo mbalimbali?
Je serikali yetu tukufu na sikivu imejipanga vipi kutatua changamoto zitokanazo na marufuku hii?
Karibuni.
Mifuko ya plastiki haihusiani na serikali sikivu wala tukufu, lazima itokomezwe imetutesa sana tangu enzi za mkuu wa mkoa Dar mzee Makamba anaingia Shoprite kuikamata! Tutabeba nyama hata ndani ya majani ya migomba, tulibeba chips enzi hizo ndani ya magazeti mazingira yalikuwa safi. Watanzania tutaanza kutabasamu baada tu ya miezi mitatu itakapoanza kutoweka majalalani.
Ninapendekezo la ziada kwa serikali, pampasi, ponpon na vinavyotumiwa kuafungia watoto navyo vipigwe marufuku kwani akinamama wanatupa hovyo mitaani.
 
Migomba ni michache kwa ukubwa wa nchi.İnabidi maeneo yote yaafayo kilino cha migomba wapande migomba kwa wingi sana kwa industry ya mifuko.kigoma, mara, moro arusha wsboreshe kilimo cha migomba kama mby kagera, moro na kilimanjaro.
Hata Mimi nadhani migomba haitokidhi mahitaji
 
Mifuko ya plastiki haihusiani na serikali sikivu wala tukufu, lazima itokomezwe imetutesa sana tangu enzi za mkuu wa mkoa Dar mzee Makamba anaingia Shoprite kuikamata! Tutabeba nyama hata ndani ya majani ya migomba, tulibeba chips enzi hizo ndani ya magazeti mazingira yalikuwa safi. Watanzania tutaanza kutabasamu baada tu ya miezi mitatu itakapoanza kutoweka majalalani.
Ninapendekezo la ziada kwa serikali, pampasi, ponpon na vinavyotumiwa kuafungia watoto navyo vipigwe marufuku kwani akinamama wanatupa hovyo mitaani.
Tatizo nini mbadala ktk kipindi hiki cha mpito
 
Mimi nitatumia pakacha langu kwa ajili ya shopping.
Kwa wale watu wa pwani wanajua Pakacha ni kitu gani!!
 
Back
Top Bottom