Machozi Yamenitoka Nikimark Midterm

Machozi Yamenitoka Nikimark Midterm

Madhara ya BRN kwa wanafunzi wanafaulu lakini hawajui kuandika only in Tanzania maajabu haya
 
Aheri ya ww wanajua hata kuandk majna yao na hawajataga hata m1. Mie nmekata tamaa kabisa jumlisha wakuu wa shule hawana mikakati yoyote, lazma uchuje. Mpaka naojiona mwenyehatia.
 
Tatizo ni mwl wao hauko makini kufundisha bali kulaumu tu
 
Tatizo wanajifanyia yakwao na BRN yao hiyo. Wanaleta u-quantity badala ya u-quality.
 
Kwa Kweli Kama Hali Ndio Hii Mwakani Naacha Kazi Ya Ualimu.Watoto Hawawezi Kuandika Kiingereza Kabisa.Wamefauluje Kuja Sekondari,nimefundisha Topic Na Kurudia Mara Nyingi,wapo Waliopata A na b na c pia.kuna kundi kubwa la waliofeli hadi mtu anapata 12,18,4,yani Nimelia Kwa Kuona Mtu Badala Ya Kuandika Legs Anaandika Leges,process-presse,before-bifore,stone-ston,monkey-mankey,fire-firs,kwa Kweli Kwa Namna Hii Sijui Wanafauluje Watu Kama Hawa.Waalimu Wenzangu Nitumie Njia Gani Mana Kuandika Hawajui Na Mimi Sylubus Haina Sehemu Ya Kufundisha Watu Kusoma Na Kuandika.Nimetumia Kila Njia Ila Madogo Baadhi Hawaelewi Kitu.


Acha Ujinga na kulia lia hapa, watu kama ninyi ndiyo mzigo kwenye hii Jamii yetu na mnaoifanya hii nchi ishindwe kwenda mbele!
Sasa kama wewe kweli ni Mwalimu na umeona kwamba Watoto wana matatizo ni kwa nini usijitolee kuwafundisha? Sasa ulitake nani awafundishe?
Unafahamu hata maana ya kuwa Mwalimu?
Mimi wakati nasoma kulikuwa na Walimu waliokuwa wanabakia shuleni mpaka saa kumi mbili jioni na watoto waliokuwa na matatizo na kuwasadia mpaka walikuwa wanaelewa na hakuna siku walikuwa wanalia lia kama wewe unavyofanya hapa!

Na Je ukiletewa watoto wa Mitaani ambao hawajawahi hata kuona mlango wa darasa ulipo utafanyaje? Unafikiri nchi itaendelea kwa kulia lia hivyo kama mtoto mdogo?

Ndiyo maana rais Mkapa aliwaita wa-Pumbavu na ma-Lofa kwa maana hamna akili wala uzalendo hata kidogo si ajabu wewe mwenyewe umefika hapo ulipo kwa sababu kuna watu huko nyuma walijitolea kukusadia kwa namna moja au nyingine sasa kama kila mtu angesema kama ulivyosema wewe si leo hii ungekuwa kwenu Machame unachuna mbuzi!
 
elimu imechanganywa na siasa kaka..usitegemee kupata compitence students..timiza wajib wako tu mkuuuu
 
Bro Ninatumia Mda Wa Ziada Sana Na Hadi Weekend.Ila Hawajui Kuandika.Bro Kuleta Uzi Huu Hapa Ni Ili Nipate Mawazo Zaidi Mana Nimetumia Njia Zote Nilizofundisho Diploma Na Katika Degree Ya Elimu.
 
elimu imechanganywa na siasa kaka..usitegemee kupata compitence students..timiza wajib wako tu mkuuuu

Ni Kweli Mana Nimejitoa Hadi Mda Wa Ziada.Nimetumia Njia Nyingi.Nikiangalia Katika Masomo Mengine Wanafunzi Hawa Wanafanya Vibaya
 
Lowasa ukiingia ondoa mdudu aitwae BRN bora watu wote wafeli kwa kukosa vigezo kuliko kufaulisha watu watao aibisha nchi yetu
 
Unataka kutuambia, umeshindwa kazi? Wacha kudeka mkuu.

Sijashindwa Kazi Mkuu,nalima Vizuri Na Napanda Mbegu Bora Bali Nalalamika Mavuno Duni Mkuu.Naomba Ushauri Wa Njia Za Ziada
 
Nitajitolea Kwa Kila Hali Na Mali Kuwasaidia Vijana Wangu.Ila Sitaweza Kuwafundisha Kusoma Na Kuandika.Kwa Kuwasaidia Ntawapa Ruhusa Waende Shule Ya Msingi Wakajifunze Kusoma Na Kuandika Kiingereza Darasa La3 Na La4 Huko.
 
Hiyo ni taaluma yako na nadhani umebobea kwelikweli. Hupaswi kulia, kusikitika wala kukata tamaa. Kuwa mbunifu, fanya darasa liwe lenye kufurahisha zaidi. Kile wanakipenda kigeuze kuwa elimu. Tunawategemea nyie alafu nanyi mnalalamika tena mwishowe hatutaona faida ya uwepo wenu tena.
 
Back
Top Bottom