Machinga waanza kunyanyaswa rasmi hawatakiwi huu si wakati wa wanyonge

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,901
Hili ni Eneo la Shule ya Sekondari Mabati Mjini Njombe ambako Meza za Wafanyabiashara wadogo (#Machinga) zimetupwa na Mgambo wa Halmashauri ya Mji huku wafanyabiashara hao wakitakiwa kuondoka pembezoni mwa Barabara na wahamie katika Soko la Dodoma.
Maskini baba aliwambia kufanya biashara popote pale jamani.

Haya mengine ni ya kutazama vyema jamani Mgambo tena wanarudi? jamani Rafiki wawamachinga Dah!!!! Leo Jpm angekuwepo Huki sijui mkuu wa MKOA mkuu wa wilaya MKURUGENZI wa halmashauri ANGEKUWA na hali gani aisee.

Kama uliona watu wanalia wanatandika nguo zao ili tu gari iliyobeba mwili wa Magufuli ipite juu ya nguo zao. Kitendo kile kilikuwa na maana ya pekee. Hiki ndicho hasa kilichokuwa #kikiwaliza msibani watanzania walijua siku za mateso #zinakaribia na sasa mateso ndiyo hayo.

#PUMZIKA kwa amani Magufuli wetu dah. Nimeandika hii msg nimehisi kutokwa na MACHOZI. Unavunjiwa banda lako ambalo ulikuwa umeweka nguvu zako huko kwa ajili ya watoto na maisha yaendelee.

KWELI ULE USEMI PAKA AKITOKA PANYA HUTAWALA NIMEAMINI SASA..

FB_IMG_1619014483386.jpg
 
Machinga hawa wanatakiwa wawe sehemu sahihi kulingana na level yao , unakuta mtu analipa frem laki Saba , mbele yake kuna machinga analipa 50000 , af anachekelea na kujiita mpambanaji... ..Fukuza kabisa hao watu waende sehemu sahihi ya umachinga
 
Lazima tuwe na ustaarabu, tupo karne ya 21 na dunia inaenda kasi. Si kila eneo ni la kila aina ya biashara. Naamini hao waliowaondoa hapo si wajinga. Sikiliza pande zote mbili kisha uje na conclusion yako, la sivyo awamu hii inayoonekana kuwa ya kistaarabu hayo machozi yako utajaza SIMTank.

Hao machinga jiwe aliwazoesha kuishi kisukuma. % kubwa ya wasukuma huku tuna ustaarabu wa zama za mawe.
 
Mbona umeweka picha hiyo hiyo moja mara nyingi hivyo? Naungana na serikali maana Jiwe aliwadanganya sana hawa Machinga, tunataka miji iwe safi bwana! Watu wanapanga bidhaa zao mpaka mwenye maduka ya wenzao bwana, hapana hatuwezi kwenda hivyo!
 
Machinga kufanya biashara popote haikuwa solution ya muda mrefu bali ilikuwa opinion ya mtu mmoja na hakuna mtu anaishi milele ila systems zinaishi milele.

Nadhani department husika zitatafuta solution ya muda mrefu ili kutatua hiyo changamoto once and for all.

Suggestion yangu ni serikali itenge budget ya kujenga miondombinu bora kwenye maeneo maalum na hawa machinga wakafanye biashara zao huko.

Hiyo ndio best solution.
 
Back
Top Bottom