Revolutionary
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 456
- 86
Moja kati ya Vigezo vikuu vya Miradi ya maendeleo ya Jamii ni ushirikishwaji wa wadau husika. Kushirikishwa kwa wadau kuna faida nyingi ikiwemo, kuleta mchango mkubwa kimawazo kutokana na experience yao kubwa katika eneo hili. Pili ushirikishwaji wa wadau huleta urahisi katika utekelezaji wa mradi husika kwa sababu unajenga ownership, wadau wanajisikia kwamba mradi ni wao tofauti kama hawatahusishwa kabisa.
Mradi wa Machinga complex ni mradi mzuri sana, lakini hali ni ya kusikitisha sasa kwani wamachinga wenyewe wamejiondokea zao wako soko lao la zamani la Karume wanaendeleza mchakato.
Waziri husika suala limemshinda, Rais kuona hivyo anaagiza wadau watafutwe mkutano ufanyike kujua tatizo ni nini? Mtazamo wangu ni kwamba angewashirikisha wadau kabla ya kujenga, haya ya leo yasingetokea. wangeweza kupata mwafaka wa nini kifanyike, leo hii mambo yangekua mazuri.
Kwa sasa nadhani kurudi wamachinga pale mjengoni ni ngumu.
Namshauri Rais na waziri husika ku-execute plan B, ambayo ni kuitisha mkutano na wafanyabiashara wakubwa na potential investors wa kitanzania na wataalamu wa fedha na uchumi ili kuona ushauri wa kiufundi na wanawezaji wa kukodishwa kufanya biashara hapo na nani yuko interested, awasilishe pendekezo lake. hakika najua watu watachangamkia fursa hii na wafanyabiashara watapatikana kufanya biashara kubwakubwa kama supermarkets, butiques, shops nk. Baada ya hapo mjengo ubadilishwe jina, maisha yaendelee kuliko kungojea na kuanza kumtafuta mchawi nani sasa wakati serikali inakosa pesa (implicitly and explicitly) kwa kudororesha economic asset ya mjengo huu.
Wakae vikao na wamachinga kutafuta suluhu mpya shirikishi kuona nini kifanyike! kama ni kujenga mjengo mwingine sehemu itakayokubalikana na wote au la!
Au mwaonaje wadau?
Akhsanteni!