Machimbo ya laptop

Machimbo ya laptop

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,235
Reaction score
1,867
Habari wakuu?
Kama kichwa cha habari hapo juu. Huwa mara nyingi tunaona tu mitandaoni machimbo ya nguo na viatu hapo kariakoo. Na bei zake rafiki. Kama kuna watu wanafahamu machimbo ya LAPTOP na bei zake tafadhali tujuzane.
ahsante sana
 
Nasubiria na mimi, ngoja ni save nna huu uzi kwa matumizi ya baadae
 
Biashara nyingi za Jumla ni uwe unachukua vitu vingi.

Kama unanunua mwenyewe online hata eBay unapata ukitumia keyword "lot of" mfano kama hizi

Kwa hapa Tanzania kuna Chris lukosi bunju, sema jamaa minada yake haipo kistaarabu, nyomi lake linataka uvumilivu. Mcheki FB angalia na WhatsApp zake

View: https://www.facebook.com/reel/1410820900673808/?app=fbl
Sometimes huwa anauza vitu vikiwa kule kule Uingereza sema jamaa ana tamaa MTU akifika dau kubwa anaweza akauza mzigo wako, kama hilo nyomi la watu kwa maelfu halikusumbui laptop za kuokoteza Hana mpinzani huyu. Nishaona MTU anachukua Hadi gen ya 8 KWa chini ya laki 2.
 
Tupene machimbo aisee! Nilicheki interview ya Ubepari PC, alisema alipoanza biashara akiwa chuoni, alikuwa anauza laptops alizokuwa akizitunza hosteli. Aliziuza kwa faida ya laki moja na hilo lilifanya wafanyabiashara wengine wachukie kuona anaua sana bei. Kwa makadirio, hizo laptop wakati anaanza zilikuwa za bei ya laki 3 hadi 5 na Wauzaji wengine walikuwa wanaweka faida ya laki 2, ambayo ni sawa na faida ya 40% au zaidi. Kwa hiyo, ukikuta dukani laptop inauzwa laki 8, unaweza ku assume kwamba muuzaji kainunua 500k hadi 570k.
 
Biashara nyingi za Jumla ni uwe unachukua vitu vingi.

Kama unanunua mwenyewe online hata eBay unapata ukitumia keyword "lot of" mfano kama hizi

Kwa hapa Tanzania kuna Chris lukosi bunju, sema jamaa minada yake haipo kistaarabu, nyomi lake linataka uvumilivu. Mcheki FB angalia na WhatsApp zake

View: https://www.facebook.com/reel/1410820900673808/?app=fbl
Sometimes huwa anauza vitu vikiwa kule kule Uingereza sema jamaa ana tamaa MTU akifika dau kubwa anaweza akauza mzigo wako, kama hilo nyomi la watu kwa maelfu halikusumbui laptop za kuokoteza Hana mpinzani huyu. Nishaona MTU anachukua Hadi gen ya 8 KWa chini ya laki 2.

Hivi jamaa vitu vyake ni genuine kweli?
 
Back
Top Bottom