Machali awaendesha puta wabunge wa CCM Bungeni!

Mbunge wa NCCR MOSES MACHALI amemwaga cheche bungeni, ameamua kuwaambia ukweli kuwa ameamua kubaki bungeni ili awambie ukweli wabunge wa CCM kuwa wanachokifanya bungeni ni kuwakandamiza watz,
amesema kuwa walichosema CDM ndoo ukweli na anawaunga mkono kwa 100% kwa jinsi walivyotoka nje kwani hakutaka kutoka nje ili awapasulie ukweli wabunge waliobaki bungeni,

Pindi MACHALI alipokuwa anaendelea kuongea kuna baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wananong'oma chinichini kitu ambacho kilimfanya
MOSES MACHALI kuwaambia "MTACHONGA SANA JUU YANGU ILA NITASEMA UKWELI SITAKI UNAFIKI"
pia kasema "HIKI MNACHOKIFANYA KWA WANANCHI MTALANIWA NYIE WABUNGE WA CCM"

kiukweli MACHALI ni noma na hapo ndoo nimeamini NCCR wako pamoja na wananchi.
 
Anayeongea sasa hivi ni kimada wa ......................... Ni mwanasheria anaongelea/reference ya uganda hivi uganda kuna demokrasia ya kweli??? Huyu mpumbavu tu anapofushwa na fedha za kishenzi....... Hana point anapigania ugali wake tu na penzi!!
 
Huku kwetu alivyoanza Machali kuwapasha unafiki wao wa kuacha kujadili mswada na kukijadili CDM tukafyekewa umeme. Ama kweli miaka 50 ya maendeleo!
 
naunga mkono hoja...Kususia ni moja ya kupinga kushiriki kwani kushiriki ni kubariki kinachoendelea kwani wanatambua mwisho wa siku itakuwa ni wanaosema ndio sema ndioooo na wanaosema sio sema siooo hiyo ni alfa ulela ulela ila huyo mbunge nimemkubali kimsimamo

tatizo sio kuwachana mkuu... hao hata uwachanaje tayari wana azimio la kupitisha huo uozo... na hii wanajivunia majority yao kwa hiyo hata uongee vip haitabadilisha maazimio yao
 
Bado DHIMA ya CDM kutoka nje iko palepale,kwa namna yoyote ccm ni wengi so kwa vyovyote vile lazima wangeupitisha kabisa,ila kiujumla Machali anajua kujenga hoja
 
Kama kuna mwana jf anaangalia bunge ataona kulikuwa na umuhimu wa wabunge kutosusia mjadala bali wangeupinga kwa hoja kama anavyofanya MH.JOSEPH MACHALI-KASULU MJINI[NCCR_ MAGEUZI]

Hoja za kuupinga zipo dhahiri na zafahamika. Kususia vikao ni njia ya kuonesha kwa dhati kutokubaliana na kupelekwa kimabavu kunakofanywa katika mchakato kama tunavyoshuhudia
 
binafsi nilisikiliza hotuba ya combani, lissu na Makinda!!!
nlichojifunza ni kwamba muswada ulishapita kabla hata ya maoni ya wabunge!! kilichobaki ni wabunge kuuza sura kwenye TV!! Mbunge aliyesikia hotuba ya Makinda na ile ya kombani na ANA BUSARA ZAKE ama asingebaki ukumbini au angebaki bila kuchangia chochote!!
 
amewambia "MTACHONGA SANA JUU YANGU ILA NITAWAAMBIA UKWELI"

nimemkubali huyu jamaa, kasema anawaunga mkono CDM ila aliamua kukaa ili awapasulie ukweli.
 
kwa hali ilivyo mswada umetekwa nyara. hata mtu atoe hoja zipi za kuupinga hatasikilizwa. Naona kinachofanyika pale ni maigizo kwamba wanajadili kumbe uamuzi unajulikana. Machali kauliza kama viongozi wa siasa hawana nafasi katika mchakato mzima wa kutengeneza muswada kwani Rais atakayepelekewa kuupitisha si mwanasiasa? Au yeye siasa zake ni bora sababu ni chama tawala? Lakini pia nini kigezo cha kukusanya maoni ya DAR, DODOMA NA ZANZIBAR? Kasulu hawana maoni. Kwa nini waseme Tanzania ni kubwa hawawezi kufika kila mahali? Mbali ni wapi na karibu ni wapi katika nchi moja? Pamoja na hoja zake kaishia kuzomewa! Huo ndio mjadala!!!
 
huyo mama anayejiita mwanasheria ovyo kabisa....

Uchangiaji wa namna hii hapa JF umezidi kuota mizizi,

Kama mtazingatia kwamba si wote kwa wakati huu wana uwezo wa kuiona tbc1 basi mngekuwa mnajitahidi kuelezea japo kwa ufupi fulani kasema hiki na kile, lakini hii ya kusema kawachana live, kawaambia ukweli, sasa wasiotazama tv sasahivi wanaelewa nini? jitahidini basi kutujuza nani kasema nini ili walau tujue kinachoendelea, wengine tumebanwa na wakoloni hatuna nafasi ya ku-access tbc kwa muda huu.

Though tunashukuru kwa kutuhamasisha kufuatilia thread hii!
 
Amemsafisha kubenea na kibanda juu ya tuhuma za mh.zito kuwa magazeti yao yamekuwa yakimuandama kumbe kweli mosses aliyatamka yale yaliyoripotiwa na magazeti hayo.

Ktk hali ya kawaida maoni ya lisu kama msemaji wa upinzani yamejitosheleza na ndio maana ccm wapambe na cuf wameshindwa kujipambanua ktk mjadala huu na kuwa busy kuwalaumu chadema na maoni yao.

Ktk hili naungana na mwana mapinduzi mwenzangu william malecela hata kama yeye ana fursa nene za kiuchumi ila kimsimamo hapa tupo pamoja.

Mosses machary hongera kwa kujipambanua na kutumia haki yako ila nimebaini kafulila na mkosamali wamekuzidi kete ktk agenda hii ya katiba yetu, tafuta njia mbadala wa kujipambanua hapo.
 
Anayeongea sasa hivi ni kimada wa ......................... Ni mwanasheria anaongelea/reference ya uganda hivi uganda kuna demokrasia ya kweli??? Huyu mpumbavu tu anapofushwa na fedha za kishenzi....... Hana point anapigania ugali wake tu na penzi!!

lazima awatetee mabwana zake licha ya kutoa kitumbua lazima aseme hayo, huoni hata sura yake imekaa kinyege nyege tu. Eti naye ni mwanasheria na mwanaharakati aliyebobea, ushuzh wako wewe kadada ka ccm (UMMY).
 
Mosses Machali amewakilisha maoni ya Watanzania wengi, tukopamoja, ingekuwa busara baada ya kumaliza kuchangia angetoka nje.
 
Kama kuna mwana jf anaangalia bunge ataona kulikuwa na umuhimu wa wabunge kutosusia mjadala bali wangeupinga kwa hoja kama anavyofanya MH.JOSEPH MACHALI-KASULU MJINI[NCCR_ MAGEUZI]

utapinga kwa hoja hata kama zitakuwa nzito kiasi gani mwisho wa siku ni sauti za ndiyo zitakazoamua kukubalika kwa mswaada au la. Machali anatakiwa kufahamu kwamba, hoja zake ni upuuzi mtupu kwa CCM unless CCM waseme tumemsikia MACHALI heshima yake inaweza kurudi.

Kwa sasa kachafuka na yeye ni sehemu ya maamuzi ya CCM, anakuja kutuhadaa kwa kutangaza laana ambazo hazitawarudisha nyuma CCM kwani wameshamua kuukubali msuada
 
huyo mama anayejiita mwanasheria ovyo kabisa....
Halafu huyu mama ni muongo anasema hata katiba ya Kenya ilipatikana kwa njia kama hii wanayotaka kuitumia Tanzania,si kweli mchakato wa katiba Kenya ulianzia mbali kwanza Bomas,halafu wakateuliwa wajumbe wa kamati ya wataalamu ambao waliwakilisha maoni bungeni na kwa wanachi ili yajadiliwe halafu ndio ikaja kupigwa kura ya maoni ya kukataa au kukubali,sasa hapa hayo masaburi ya katiba kayaandika nani na nina kapendekeza hiyo kamati iliyoandika hayo masaburi?upuuzi mtupu CCM mnatupeleka pabaya na bado hamjifunzi na hamsikii sijui ni ujinga au ndio kujipendekeza kwenye chama,subirini dawa yenu ipo jikoni tutaonana 2015 tumewaona ,tumewasikia
 
Mosses Machali amewakilisha maoni ya Watanzania wengi, tukopamoja, ingekuwa busara baada ya kumaliza kuchangia angetoka nje.

hawezi kutoka nje kwani yeye ni sehemu ya maamuzi ya CCM kupitisha muswada. Anachokifanya anatuhadaa kwa kujifanya yuko na sisi watatnzania wakati ukweli siyo.

Ikumbukwe tu kuwa hakuna atakachosema kitawarudisha nyuma CCM
 
Hongera mh. Machali ukweli wananchi tunaona na tunafuatilia kwa makini sana.ukweli ni kwamba wabunge wengi hasa wa cmm nashangaa wanashindwa kujikita kwenye tatizo badalake wanakalia vijembe.big up
 
Back
Top Bottom