Machali awaendesha puta wabunge wa CCM Bungeni!

Machali awaendesha puta wabunge wa CCM Bungeni!

amewambia "mtachonga sana juu yangu ila nitawaambia ukweli"

nimemkubali huyu jamaa, kasema anawaunga mkono cdm ila aliamua kukaa ili awapasulie ukweli.

niungane na mdau aliyesema kuwa baada ya kuwachana, kuonesha kuwa amekerwa angetoka nje ya ukumbi kwani kama ni mtu makini hana haja ya kuendelea kubishana na ccm, kwani hana anachoweza kuwashawishi wezi wale
 
Mtoa mada ulitakiwa ulete na taarifa nzima na sio kidokezo kama hiki kwa sababu wengine tunakuwa class hatuangalii tv
Mkuu pole na kitabu, umekosa uhondo wa Mh. Machali, kawafunika Wabunge wote wa CCM walichangia mswada huo leo. Ila usihofu Darasa ni muhimu ili usijeukawa Dent wa KUDESA na paper.
 
binafsi nilisikiliza hotuba ya combani, lissu na Makinda!!!
nlichojifunza ni kwamba muswada ulishapita kabla hata ya maoni ya wabunge!! kilichobaki ni wabunge kuuza sura kwenye TV!! Mbunge aliyesikia hotuba ya Makinda na ile ya kombani na ANA BUSARA ZAKE ama asingebaki ukumbini au angebaki bila kuchangia chochote!!

Pia chama cha majaji wastafu wamesema kuwa kitendo cha muswada huu kuwekewa tarehe ya kuanza kutumika hata kabala ya kupitishwa na bunge ni dalili za wazi kuwa Serikali hailiheshimu bunge na ina uhakika hata iweje muswada huo utapita na kuwa sheria.
 
Ndugu zangu tangu nilipoanza kusikiliza mjadala huu ni leo tu angalau mbunge mmoja kati ya waliobakia ndani amemwaga point tupu. Hata makinda amekubali maana alikuwa akisikiliza kwa makini sana. Naamini Kijana Machali amefanya kazi ya ziada kuwapa laivu magamba . Nilikuwa najaribu kuangalia yale mazee manene yenye vitambi yakiwa hayaamini point zinazotoka kwa kijana wetu Moses bila shaka kuna somo pale. Kwanza amewasifu CDM kwa msimamo wao na akasema yuko pamoja nao ila alibaki kuwapasha magamba. Amewaomba sana kutokubali mswaada huo. naamini baada ya hapo Makinda na Pinda watakaa kutafakari upya ujumbe wa Shujaa Moses . Well done Machali Mungu aendelee kukupa busara zaidi usijiunge na magamba huko mbeleni . Ujumbe umefika watanzania tumekusikia na naomba vyombo vya habari na Jf tumpe support ili watu wengi wapate ujumbe wake kwa wingi.
 
Hata mimi niemsikia. Jambo aliloanza nalo ni kuwaomba wabunge na watanzania kwa ujumla wajiulize ni kwa nini wabunge wa CDM wanapinga? na n kwa nini wananchi na wanaharakati wanupinga mswada huu? sasa suala la CCM kujiuliza ndilo haliwezekani kwani ni sikio la kufa. Ngoja wamalize kisha sisi tuanze
 
Kama kuna mwana jf anaangalia bunge ataona kulikuwa na umuhimu wa wabunge kutosusia mjadala bali wangeupinga kwa hoja kama anavyofanya MH.JOSEPH MACHALI-KASULU MJINI[NCCR_ MAGEUZI]
Ukishindwa kwa wingi hoja zako si imeshindwa? Hao wanahitaji hivyo hivyo tu.
 
Ndugu zangu tangu nilipoanza kusikiliza mjadala huu ni leo tu angalau mbunge mmoja kati ya waliobakia ndani amemwaga point tupu. Hata makinda amekubali maana alikuwa akisikiliza kwa makini sana. Naamini Kijana Machali amefanya kazi ya ziada kuwapa laivu magamba . Nilikuwa najaribu kuangalia yale mazee manene yenye vitambi yakiwa hayaamini point zinazotoka kwa kijana wetu Moses bila shaka kuna somo pale. Kwanza amewasifu CDM kwa msimamo wao na akasema yuko pamoja nao ila alibaki kuwapasha magamba. Amewaomba sana kutokubali mswaada huo. naamini baada ya hapo Makinda na Pinda watakaa kutafakari upya ujumbe wa Shujaa Moses . Well done Machali Mungu aendelee kukupa busara zaidi usijiunge na magamba huko mbeleni . Ujumbe umefika watanzania tumekusikia na naomba vyombo vya habari na Jf tumpe support ili watu wengi wapate ujumbe wake kwa wingi.

Mkuu pamoja na hoja nzuri kabisa lakini badili rangi unayotumia inaumiza macho kusoma kidogo, otherwise you're right.
 
KWELI MACHALI NIMEMKUBA NA NAMUUNGA MKONO HUYU KIJANA MWENZANGU,NIMEKUWA NIKIFUATILIA TANGU SAKATA HILI LILIPOANZA HAPO JANA,MACHALI HAKUTOKA WENZAKE WALIPOTOKA NIKAHISI LABDA MTAZAMO WAKE NI CHANYA YAANI KUUNGA MKONO KUMBE NI MPIGANAJI ALIYEBAKI KUHAKIKISHA ANAPIGILIA MSUMARI MSIMAMO WA WENZAKE WALIOTOKA NJE.

KAMA KUNA MDAU ALIKUWA ANAFUATILIA ATAKUBALIANA NA MIMI KUWA HATA SPIKA ALIPOMPA NAFASI ALIMPA NAFASI HIYO AKIWA NA MATUMAINI KUWA JAMAA ATAWASUTA WENZAKE MAANA ALIMKARIBISHA KWA BASHASHA NA SMILE YA KULAZIMISHA KUMBE NI SHUJAA SIYETAKA KUBEZWA.

NILIPENDA ALIPOWAAMBIA ''MIZEE YA CCM'' KUWA NAMNUKUU '' mtachonga sana juu yangu ila nawasilisha mawazo yangu,ya wananchi wangu,chama na watanzania kwa ujumla''.

HIVI CCM MBONA WANAIPELEKA HARAKA HII ISSUE!!MI NAONA CHAMA KIMEJAA WAZEE WENGI KIASI KWAMBA WAMEFIKIA ''POINT OF NO RETURN'' KWENYE KUFIKIRIA NA KUHESHIMU AMANI YA WATZ WAPIGA KURA WAO!! WANAJALI KULA TU NA KUSHIBA BILA KUSAHAU MIPASHO!! MI NAOMBA KAMA WANAWEZA UPANDE MWINGINE WA BUNGE HASA NYUMA IWE INAKAA BENDI YA TOT IWE INACHAGIZA. SHAME ON THEM( CCM)!!
 
tatizo sio kuwachana mkuu... hao hata uwachanaje tayari wana azimio la kupitisha huo uozo... na hii wanajivunia majority yao kwa hiyo hata uongee vip haitabadilisha maazimio yao

Nonsense Majority mwategemea nchi itakuwa salamaa kweli hivi CCM wana kuwa na wasiwasi gani kama wao wanaongoza nchi kwa muda wote huo leo hii kukubali kile wananchi wanakitaka wao wanaoni ni adhama fulani hivi inawavua nguo au ?? wao hawakuwa wakisoma alama za nyakati? Au JK alikubali haraka akijua kuwa wataupitisha kimtindo mtindo ??

My Take;
wabunge wa CCM hebu kuweni wasikivu kwanza msipende kusema CHADEMA na VYAMA vingine vya upinzani ni wakorofi yaweze kana hata nyie CCM ndio wakorifi kupita maelezo kwani nyie ndio mumeshika Dolla sasa mwaogopa nini kukubali huo muswaada wa katiba kuendana na matakwa ya watanzania?

CCM hapo nyie hamuoni kuwa twatengeneza janga lingine kwanini tusiepushe janga na kuwasikiliza wananchi hilo kundi dogo la wapinzani msitake kulifanya ati wao hawajui kitu kumbukeni kidogo huwa ndio bora sana kuliko kingi yawezekana wingi wenu ukawa na maamuzi mabaya kuliko ya wachache mkaja jutia baadae.

Au ndani yenu CCM kunashinikizo hili lipite la mswaada ili mtu furani au kundi fulani lije kuwajibishwa huko mbeleni au mwalichukulia hili jambo kiutashi wa kichama zaidi?
 
Na kama damu ya watanzania itamwagika watu wawili ambao wanatakiwa wakamatwe mara moja ni Spika Anna Makinda na Waziri Mkuu Pinda. Wawili hawa wamekuwa wanakazania muswada usomwe bila ya kupata maoni ya wananchi. Cha ajabu Spika anapuuza hata hata maagizo ya bunge wakati muswada huu unaondolewa (March).

Pinda na Makinda walikuwa na uwezo kabisa wa kuzuia haya lakini wametumia nafasi yao kubaka demokrasia. Hawafai.
Jamaa keshajua na kuona utamu wa kuogea sabuni za kunukia sasa, utamwambia nini!
 
ni kweli huo muswada ni kama umeshapita,inatakiwa mpaka tarehe 1.12.2011 kuwe na tume.

binafsi nilisikiliza hotuba ya combani, lissu na Makinda!!!
nlichojifunza ni kwamba muswada ulishapita kabla hata ya maoni ya wabunge!! kilichobaki ni wabunge kuuza sura kwenye TV!! Mbunge aliyesikia hotuba ya Makinda na ile ya kombani na ANA BUSARA ZAKE ama asingebaki ukumbini au angebaki bila kuchangia chochote!!
 
niungane na mdau aliyesema kuwa baada ya kuwachana, kuonesha kuwa amekerwa angetoka nje ya ukumbi kwani kama ni mtu makini hana haja ya kuendelea kubishana na ccm, kwani hana anachoweza kuwashawishi wezi wale
Si kwamba ni Wezi tu bali akili zao zimeshagandiana Ujinga. Hawezi kuwabadili wale kwani akilizao zimeshafikia "monopoles" ya kuelewa
 
Kama kuna mwana jf anaangalia bunge ataona kulikuwa na umuhimu wa wabunge kutosusia mjadala bali wangeupinga kwa hoja kama anavyofanya MH.JOSEPH MACHALI-KASULU MJINI[NCCR_ MAGEUZI]

Halafu mwisho wa siku?.....wanafiki waseme ndio....ndioooooîìöþ...! Wasioafiki waseme sio....wanafiki wameshinda mswada umepita! daa, kudadaa!
 
amewambia "MTACHONGA SANA JUU YANGU ILA NITAWAAMBIA UKWELI"

nimemkubali huyu jamaa, kasema anawaunga mkono CDM ila aliamua kukaa ili awapasulie ukweli.
kwahiyo baada ya kupasua ukweli kesho ataungana na wenzake kutoka au? Na session ya jioni je, atahudhuria? tusubiri tujionee wanasiasa wetu
 
kwa hali ilivyo mswada umetekwa nyara. hata mtu atoe hoja zipi za kuupinga hatasikilizwa. Naona kinachofanyika pale ni maigizo kwamba wanajadili kumbe uamuzi unajulikana. Machali kauliza kama viongozi wa siasa hawana nafasi katika mchakato mzima wa kutengeneza muswada kwani Rais atakayepelekewa kuupitisha si mwanasiasa? Au yeye siasa zake ni bora sababu ni chama tawala? Lakini pia nini kigezo cha kukusanya maoni ya DAR, DODOMA NA ZANZIBAR? Kasulu hawana maoni. Kwa nini waseme Tanzania ni kubwa hawawezi kufika kila mahali? Mbali ni wapi na karibu ni wapi katika nchi moja? Pamoja na hoja zake kaishia kuzomewa! Huo ndio mjadala!!!

ccm ni wapuuzi sana wamechukua maoni ya zanzibar,dar na dodoma kwani wameambiwa katiba ni sawa reseach hadi waamue kuchukua sample population and sample size?
 
Yah,kaongea vizuri ila namshauri naye atoke coz jioni watampiga madongo mengi na asipovumilia atampiga m2 ngumi ,si tunajua magamba yanavyojua umbea na majungu kuliko kujenga hoja?
 
Watanzania tutumie muda huu kuomba na kufunga kila mtu kwa imani yake ili haki itendeke kwenye huu mchakato mzima wa kuelekea kupata katiba mpya
Na sio kuwa watizamaji tu.

Maombi ya umoja Mungu huwa anajibu kwa haraka,and it is never too late kwa Mungu,hivyo anza kufanya dua,maombi kwa imani yako sasa hivi.
 
Back
Top Bottom