Machali awaendesha puta wabunge wa CCM Bungeni!

Kama kuna mwana jf anaangalia bunge ataona kulikuwa na umuhimu wa wabunge kutosusia mjadala bali wangeupinga kwa hoja kama anavyofanya MH.JOSEPH MACHALI-KASULU MJINI[NCCR_ MAGEUZI]
 
Nilitamani kumsikiliza kijana huyu ila bahati mbaya majukumu yamenibana sikuweza kuwa na TV karibu.Tuabarisheni jamaa kachangia lipi jingine la muhimu.
 
aisee jamaa kawachana chana vibaya magamba. leo spika kakubari taarifa jana alikataa kila kitu. sijui kimada wa nani anaongea saa hizi ptuuuu
 
Mb Machali ameichana chana mswada wa katiba kwa upana, amesema... kama mswada utapitishwa basi damu ya watanzania itakuwa juu ya wabunge wa ccm wote kwani maoni ya watanzania wote walitaka mswada usomwe kwa mara ya kwanza.

amesema hakutaka kutoka ili aweze kuwaeleza wabunge wa ccm kwa uwazi pasipo kuwaficha tatizo walilo nalo wana ccm.

kazi ipo kweli kweli
 
wambie wabongo wanatembea na majina kiushabiki.jamaa ametumia akili si masub... Km hao wngn walisusa
 
Nimemsikia, lakini mtoa hoja ulipaswa kuelezea zaidi kinachoendelea
ili hata wale wasiotazama televisheni saa hizi wajue kinachoendelea
kuliko kuleta habari nusu nusu...
 
kasisitiza suala la kuusoma mswaada kwa mara ya kwanza
vilevile kasema wananchi bado wanahitaji kutoa maoni maana maoni yaliychukuliwa ni ya watu wa dodoma, dsm na zanzibar tu wakati nchi hii ina mikoa kibao
 
Kama kuna mwana jf anaangalia bunge ataona kulikuwa na umuhimu wa wabunge kutosusia mjadala bali wangeupinga kwa hoja kama anavyofanya MH.JOSEPH MACHALI-KASULU MJINI[NCCR_ MAGEUZI]

tatizo sio kuwachana mkuu... hao hata uwachanaje tayari wana azimio la kupitisha huo uozo... na hii wanajivunia majority yao kwa hiyo hata uongee vip haitabadilisha maazimio yao
 
Mb Machali ameichana chana mswada wa katiba kwa upana, amesema... kama mswada utapitishwa basi damu ya watanzania itakuwa juu ya wabunge wa ccm wote kwani maoni ya watanzania wote walitaka mswada usomwe kwa mara ya kwanza.

amesema hakutaka kutoka ili aweze kuwaeleza wabunge wa ccm kwa uwazi pasipo kuwaficha tatizo walilo nalo wana ccm.

kazi ipo kweli kweli

Sio wa ccm tu, hata wa cuf wanahusika...
 
Jamaa Machali nimemkubaliii......katoa point nzuri sana,amenifurahisha na kunifanya niendelee kuangalia. Ila huyu Ummy anavyowaponda wanasheria wenzake zinamtosha kweli??????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Eti wakasome tena sheria hahahaaaaa kaaaaz ipoooo
 
Na kama damu ya watanzania itamwagika watu wawili ambao wanatakiwa wakamatwe mara moja ni Spika Anna Makinda na Waziri Mkuu Pinda. Wawili hawa wamekuwa wanakazania muswada usomwe bila ya kupata maoni ya wananchi. Cha ajabu Spika anapuuza hata hata maagizo ya bunge wakati muswada huu unaondolewa (March).

Pinda na Makinda walikuwa na uwezo kabisa wa kuzuia haya lakini wametumia nafasi yao kubaka demokrasia. Hawafai.
 
Big up Machali...nimekuckiliza kipindi unaongea umewapa kubwa hao magamba,nimefurah ulivyosema kuwa hukuamua kutoka ili wakati ukifika uwape vidonge vyao...hakika watalaaniwa na wananchi.
 
Kususia ni moja ya kupinga kushiriki kwani kushiriki ni kubariki kinachoendelea kwani wanatambua mwisho wa siku itakuwa ni wanaosema ndio sema ndioooo na wanaosema sio sema siooo hiyo ni alfa ulela ulela ila huyo mbunge nimemkubali kimsimamo
 
kasema Raisi ni mwenyekiti wa CCM na mwanasiasa kwa nini na wenyeviti wa vyama vingine hawahusishwi? Na waziri Kombani alisema wanasiasa wasiwepo kwenye mchakato mbona Raisi ni mwanasiasa? Na akawa anawaambia mtachonga sana nawasikia huko ila ntaongea ukweli ((inaelekea kuna wabunge walikuwa wanamsema)
 
Kuna njia nyingi za kukataa jambo
1.kukaa kimya bila kuchangia
2.kuchangia kwa kukataa moja kwa moja.
3.kuondoka na kuwa mbali ili usijiusishe.
Kwa hiyo machali na wana CDM wote nawapa BIG UP.
 
Mtoa mada ulitakiwa ulete na taarifa nzima na sio kidokezo kama hiki kwa sababu wengine tunakuwa class hatuangalii tv
 
Back
Top Bottom