Machache kati ya mengi kuhusu maisha

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Katika maisha nimejifunza mambo mengi, na bado naendelea kujifunza, na haya ni baadhi,

1.USIMUAMINI MTU-Wengi wetu tumeumizwa na watu ambao tuliwaamini kwa namna moja au nyingine, kwa mfano
Umetembelewa na ndugu yako lakini baada ya siku kadhaa anambaka mtoto au anakuibia nk.

2.USIMDHARAU MTU YEYOTE-Unaweza kumdharau mtu au kumchukulia poa lakini baadae akaja kuwa msaada
kwako.

3.USISHINDANE NA MTU-Katika maisha tumetofautianakwa namna nyingi ikiwemo swala la kipato, ukishindana na
na mtu mwisho wa siku utajikuta unakuwa mtumwa, ishi kulingana na uwezo wako
maisha siyo mashindano japo hukatazwi kuiga mazuri.

4.USIACHE KUOMBA/KUSALI-Mtegemee MUNGU kwa kuomba na kusali kulingana na imani yako, Mungu hawezi
kukuacha kamwe hasa nyakati za tabu.

5.IPENDE NA KUIJALI FAMILIA YAKO-Unapoijali familia yako kwa kuitunza na kuihudumia vyema, Mwenyezi Mungu
atakubariki kwa kukuzidishia riziki za kila siku.

6.ISHI KWA MALENGO-Hakikisha unaishi kwa kujiwekea malengo na kupiga hatua za maendeleo, mfano
mwaka huu umefanikiwa kununua kiwanja, mwakani ujenzi nk.

7.USIKATE TAMAA-Ni kweli wakati mwingine hali huwa ngumu, lakini jitahidi usikate tamaa, simama imara usonge
mbele, jitahidi kuwa shujaa wa maisha yako mwenyewe.

8.SAIDIA WASIOJIWEZA-Kusaidia wasijiweza ni sehemu ya ibada, saidia kadri ulivyojaliwa na mwenyezi Mungu
Pia unaposaidia usijionyeshe au kujikweza na pia usimsimange uliyemsaidia.

9.SHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII-Pamoja na ubize wa maisha, usiache kushiriki katika matukio ya kijmii kwa
mfano Misiba, kuwachangia wagonjwa wasiomudu gharama za matibabu nk.

10.USIWE MTU WA MARINGO/KUJISIKIA-Iwapo Mwenyezi Mungu amekubariki kuwa na maisha mazuri, usijisifu
na kuwaona wengine ni wazembe, ishi na watu wote kwa amani japokuwa
ni vigumu kuwafurahisha wote, maadui huwa hawakosekeni na hawana
sababu ya msingi kukuchukia.

NAWASILISHA.
 
Maisha hayana formulary mkuu,,et kwamba uishi hivi au ishi vile ndo utakuwa hivi au vile maisha hayapo hivo,.

some time ni Bora uishi kama jongoo haoni mbele wala nyuma akijigonga sehem anajua hapa Pana obstacles anachange njia anaelekea sehem sahihi Hilo ndo life

Life halina principal maalumu wakuu.
 
Hivi mtu unaposema usimuamini mtu inamaanisha usishirikiane nae au usimwambie siri zako au umfukuze au kukata ushirika hata kama nimtu mnaehusiana??au inamaanisha kua mchoyo kwake ??au uwe nae wasiwasi??hua siilewi hii point kua inawezekana vipi mtu unaeshirikiana nae halafu ukawa humuamini,nnachokiona hapa niwatu hubadirika au hugeuka au kusalitiwa!
 
Katika maisha nimejifunza mambo mengi, na bado naendelea kujifunza, na haya ni baadhi,

1.USIMUAMINI MTU-Wengi wetu tumeumizwa na watu ambao tuliwaamini kwa namna moja au nyingine, kwa mfano
Umetembelewa na ndugu yako lakini baada ya siku kadhaa anambaka mtoto au anakuibia nk.

2.USIMDHARAU MTU YEYOTE-Unaweza kumdharau mtu au kumchukulia poa lakini baadae akaja kuwa msaada
kwako.

3.USISHINDANE NA MTU-Katika maisha tumetofautianakwa namna nyingi ikiwemo swala la kipato, ukishindana na
na mtu mwisho wa siku utajikuta unakuwa mtumwa, ishi kulingana na uwezo wako
maisha siyo mashindano japo hukatazwi kuiga mazuri.

4.USIACHE KUOMBA/KUSALI-Mtegemee MUNGU kwa kuomba na kusali kulingana na imani yako, Mungu hawezi
kukuacha kamwe hasa nyakati za tabu.

5.IPENDE NA KUIJALI FAMILIA YAKO-Unapoijali familia yako kwa kuitunza na kuihudumia vyema, Mwenyezi Mungu
atakubariki kwa kukuzidishia riziki za kila siku.

6.ISHI KWA MALENGO-Hakikisha unaishi kwa kujiwekea malengo na kupiga hatua za maendeleo, mfano
mwaka huu umefanikiwa kununua kiwanja, mwakani ujenzi nk.

7.USIKATE TAMAA-Ni kweli wakati mwingine hali huwa ngumu, lakini jitahidi usikate tamaa, simama imara usonge
mbele, jitahidi kuwa shujaa wa maisha yako mwenyewe.

8.SAIDIA WASIOJIWEZA-Kusaidia wasijiweza ni sehemu ya ibada, saidia kadri ulivyojaliwa na mwenyezi Mungu
Pia unaposaidia usijionyeshe au kujikweza na pia usimsimange uliyemsaidia.

9.SHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII-Pamoja na ubize wa maisha, usiache kushiriki katika matukio ya kijmii kwa
mfano Misiba, kuwachangia wagonjwa wasiomudu gharama za matibabu nk.

10.USIWE MTU WA MARINGO/KUJISIKIA-Iwapo Mwenyezi Mungu amekubariki kuwa na maisha mazuri, usijisifu
na kuwaona wengine ni wazembe, ishi na watu wote kwa amani japokuwa
ni vigumu kuwafurahisha wote, maadui huwa hawakosekeni na hawana
sababu ya msingi kukuchukia.

NAWASILISHA.
Sawa mkuu.
 
Mke akipika chakula utakataa kula kwasababu ya kuogopa kufa ukihofia kutiliwa sumu?Tusipowaamini watu tutaishije? Maisha wakati mwingine ni pata potea! Labda pengine tuambie ni katika mazingira yapi tunaweza kutokuamini watu.
 
Back
Top Bottom