Mambo matano yanazoweza kukuepusha na hila za Wanadamu

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
"Wanadamu hatuwezi kuishi kwa amani wakati wote kwa sababu kila mmoja anapambana kuwa bora zaidi ya mwingine".

Nukuu kutoka kwa mwandishi mkongwe wa vitabu vya ziada katika masomo ya elimu ya sekondari nchini Tanzania Zist kamili.

Ni jambo la wazi kuwa wanadamu hupigana vikumbo na kuzushiana kila aina ya mambo machafu ili tu wapate ufahari, riziki, vyeo na mambo mengine.

Lakini mbali na yote mtu unaweza kusimama na kujiepusha na hila za wanadamu kwakuwa na mtindo fulani wa kuishi ambao ni rafiki na unaoweza kukuepusha na hila mbalimbali za wanadamu.
zingatia mambo haya ili kujiepusha na hila hizo.

Kwanza kabisa unapaswa kujiweka karibu na Mungu. Watu wengi hujisahau kwa kujiamini sana wao wenyewe hivyo wanapopatwa na mambo magumu ambayo yamewazidi uwezo huamua kuchukua maamuzi magumu ikiwemo kujitoa uhai.

Kujiweka karibu na Mungu kunamfanya mtu kuwa na hofu ataishi kwa kutenda mema, atajiamini na ataweza kuhimili hila za watu wabaya kwake kwa sababu mtu mwenye imani ni mtu imara na hatetereki.

Pili unapaswa kujua madhaifu yako na kubali kubadilika, kufanya hivyo kutakusaidia kuishi kulingana na wakati na kuepuka migogoro ambayo ingejitokeza kutokana na mabishano na kuwa nyuma ya muda.

Usiwe hakimu wa maisha ya watu wengine kwa kuepuka usengenyaji na umbea. watu hawapendi kufuatiliwa sana hivyo ikitokea wakagundua hivyo watataka kulipiza kwa kukufanyia hila hata kama hukutenda kosa kubwa kwao.

Si hivyo tu pia jitahidi kuwa mfano watu wajifunze kutoka kwako kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo utu, hekima na busara kupitia hayo watu watakuheshimu na watakuombea mema hila dhidi yako zitapungua.

Baada ya yote hayo ishi kama watu wengine kuwa mtu wa kujishusha na kuthamini maisha ya wengine, usiwe mtu wa kujiona bora kuliko wengine kwa sababu tabia hiyo inaweza kusababisha watu washindane na wewe na kuanzisha hila dhidi yako.

Peter Peter Mwaihola.

IMG_17107828363481935.jpg
 
View attachment 2938428
Ukisoma kitabu cha machiavelli the prince utaweza kumdhibit mwanadamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom