Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

Aah sasa pale si kitaa tu tukitoka Tambaza tunapitia pale, kama mitaa miwili over, kabla KK hajahamia Hill Road Obay, kulikuwa na washkaji pale kama kwao.
Aaah aah.....mimi nilijua mpaka kule obay ulikua unafika.....Mara ya mwisho namwona KK ilikua 1995 na harakati zake za siasa...baada ya hapo ni kama umaarufu wake ulimezwa na siasa za chama tawala!!!
Afu bro nikuulize kitu???
Hv yule braza wa KU mpole mpole aliekua anaitwa Nigga one si alikua anakaa kinondoni biafra enzi hizo...1992???
Maana baadae alifariki kwa kuumwa ghafla duuuh.....ilikua sijui 1994 kama sikosei..
 
KU ilikuwa na watu kuanzia Masaki na Obay mpaka Ilala na Temeke huko.

Huyo dada utakuwa unamuongelea Regina. Alikuwa anapenda sana basketball.

Hayo mambo ya magari ilikuwa habari za Idi, akibadilisha mara Audi, mara Toyota Hilux, akipiga misele.

Idi mtu poa sana lakini kwangu, kuna siku niko darasa la nne Muhimbili, basi kuna mwalimu mkuda katuchelewesha darasani saa nane hajatuachia. Huko nje dereva wetu kakaa tu anasubiri muda mrefu. Idi akachukua dhamana ya kuchukua jina langu kwa dereva akaja mpaka darasani akamwambia mwalimu huyu jamaa anatakiwa nje kuna dereva katumwa kuja kumchukua.

Ilibidi mwalimu aturuhusu tutoke.

Kuanzia siku hiyo Idi akawa mshkaji poa sana.
 
Bro pale Aza boi ukuacha chata chooni na wewe 🀣🀣🀣????...
 
Yeah nimekumbuka...atakua sista regina na boy friend wake Patrick mcheza basket kwenye ile timu ya mzee yule white Malay aliekua anawapa ajira vijana kule posta kwenye kampuni yake .....Regina na Patrick walikua wanacheza basket pamoja sometimes!!!
Braza Iddi hv yupo tz kweli au nae upo nae ughaibuni???
 
Daah, yule jamaa yuko Korea?

Sijamuona siku nyingi sana. Yule mshikaji wangu kinoooma. Nilikuwa najiuliza yuko wapi siku hizi?

Yule jamaa ukimpeleka kokote ana shine tu.

Halafu unavyosema aligombea ubunge sawasawa ndiyo zake, yule popote lazima atake uongozi hata shule alikuwa anapenda sana ukiranja kiranja hivi.
 
Idi alikuwepo Bongo kuna wakati alikuwa ana ma limousine anakodisha. Sijui kama mpaka sasa yupo.
 
KK alihamia Obay kwa kina Cool Moe Cee kule Hill Road. Sisi tulikuwa tunaenda sana kwake Upanga pale kabla hajahamia Obay.

Nigga One najua mmoja wa wazazi wake alikuwa anakaa Ilala. Kwenye msiba nilienda Ilala. Lakini hangout ilikuwa sana mitaa ya Obay/ Masaki.
 
Kule maskani Tambaza mlikua mnamuita MKALIMANI kwa sababu ya kutema ungenge πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚.
 
Duuuh braza kweli wewe kitambo......nakumbuka braza Zafala alisema kua msiba ulikua ilala...
Kuna picha walipiga na braza yangu Kibakuli...
Nikiipata nakutumia bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…