Kumbukumbu zangu juu ya Migogoro ya Waarabu na Wayahudi

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Dec 26, 2022
9,473
12,886
Wanasema uzee dawa na ni kuona mengi katika maisha ya ubinadamu. Nakumbuka miaka hiyo ya 1965, nilikuwa kijana mdogo kabisa na nikifuatilia kwa karibu mzozo wa Mashariki ya Kati. Nilibahatika kuishi jijini Cairo na jijini Damascus na Beirut, na nilikuwa naona maandamano na miadhara ya kila siku ya Waarabu na watu wanaowaunga mkono dhidi ya Wayahudi.

Walikuwa wanajiandaa na kile walichosema kuwa ni Kiama cha Wayahudi kwa kuifuta Israeli kwenye ramani ya Dunia. Walikuwa wanajiandaa kijeshi na kipropaganda pia, na kila siku nilishuhudia mihadhara na maandamamo kila baada ya swala ya adhuhuri, na kuna nyimbo moja maarufu walikuwa wakiimba na nitaitafsiri kwa Kiswahili chepesi ndugu zangu;

"Tutafika Tel Aviv kesho,
Haifa asubuhi na mapema,
Na tutaichukua Jerusalem yote,
Kuifuta Israel ni jambo la Mungu,
Pia kuwaua makafiri ni lazima,
Mayahudi ni watumwa na adui,
Kuwaua ni lazima tukijaaliwa."


Basi nikawa najiuliza, hivi hizi nyimbo na mbwembwe za maandamamo kuanzia Rabat mpaka Beirut hawa Wayahudi watapona kweli?

Sina haja ya kuelezea kilichotokea sababu matokeo ya mwaka 1967 yalifanya mitaa ya Cairo na Beirut na Damascus iwe kimya kwa muda mrefu na zile hamasa na mbwembwe hazikuwepo tena.

Mwaka 1973 ile hali ikajitokeza tena japokuwa sikuwepo Misri ila nilishuhudia kupitia televishioni nikiwa Kigali Rwanda wale mateka wanajeshi wa Israel walivyokuwa wanapigwa picha na kufanywa kama maenyesho kwa muda, na pale wayahudi walipoanza pia kuwapiga picha mateka wanajeshi wa Misri na Syria na kuwafanya maonyesho basi zile hamasa za maandamano pale Cairo na Beirut zikakoma.

Lakini sasa ninachotaka kuelezea ni huku kwetu Tanzania bara na visiwani, Kenya na Uganda wakazi wake na hasa mihemuko ya waumini wa dini za kiislamu na kikirsto katika kushabikia mgogoro wa Waarabu na Wayahudi kupitia nyumba za ibada na mihadhara na mikutano ya injili na kupitia vijiwe vya kahawa na kwenye usafiri wa umma.

Enzi hizo kuna watu waliuana sababu ya ushabiki na kuna watu waliacha kusalimiana sababu ya ushabiki.

Kuna watu walirogana sababu ya ushabiki na kuna watu mtaani walikuwa hawasalimiani sababu ya ushabiki, ilikuwa balaa la chini chini kweli kweli enzi hizo za kushabikia migogoro ya Waarabu na Wayahudi.

Hii hali nimeona inajitokeza tena kwa sasa na kuwagawa wana Afrika Mashariki na kuwafanya wapoteze umoja wao.

Sasa kama mwandishi habari mbobefu na mwanasaikolojia wa habari za binadamu nikawa najiuliza maswali je, na sisi wana Afrika Mashariki tukipata matatizo hivi kuna watu duniani watapigana kwa ajili ya matatizo na changamoto zetu?

Watanzania wanachukiana na kutukanana kuliko hata Waarabu na Wayahudi wenyewe, na wakati huo wahusika wengine wanaendelea na maisha yao kama kawaida.

Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuushabikia huu mgogoro hapa Tanzania hakukuanza leo bali toka enzi za akina Yohana Pandiwi na Sheikh Mganyizi miaka hiyo ya 1960's na walijichosha tu makoromeo yao kwa kukwaruzana na kutukanana na kuvunjiana heshima na kukanana hadharani mbele ya sisi wadogo zao enzi hizo.

Nikajifunza duniani migogoro haitokwisha na hivyo ni upotezaji wa muda kuifuatilia na kujaribu kuishabikia.

Toka enzi za miaka ya sitini nimetazama mashabiki wa mgogoro huu na mpaka nazeeka bado mashabiki wapya wanazaliwa na hakuna kilichobadirika, sasa kama mtu mzima natambua ni upotezaji wa muda kushabikia migogoro isiyokuhusu?

Watanzania wamechukiana na kutukanana na kupigana lakini hawajabadilisha chochote toka enzi hizo kwa kumbukumbu zangu. Hivyo katika kumbukumbu zangu nimekuja kugundua uzeeni kuwa kufuatilia migogoro kama hii ni kupoteza muda tu wa kufanya mambo mengine kabisa ya msingi maishani hasa suala la kujiongezea kipato cha kiuchumi.

NB: Nawashangaa vijana wa sasa wanavyobishana kuhusu huu mgogoro na kufikia kujengeana uadui kwa mgogoro usiowahusu. Sisi tumebishana kuhusu huu mgogoro hizo miaka ya 1960’s tukiwa vijana wadogo na tukitoka hapo tunaenda disko joka pale forodhani kuruka madebe au kuangalia sinema huku makoo yakiwa yametukauka kwa ushabiki wa mgogoro usiotuhusu.
 
Wayahudi wenyewe wachache tu, kwann muwabague kisa sio dini yenu. Alafu Jewish na Arabs ni ndugu kwann mnataka kuwafuta. Haya walienda Ulaya Adolf Hitler aliwaua Ujerumani, sasa wamekuja kwenu ndugu zenu waarabu muaanza kubagua kisa dini.Dunia nzima iko mbioni kupinga Ubaguzi huu
 
Wayahudi wenyewe wachache tu, kwann muwabague kisa sio dini yenu. Alafu Jewish na Arabs ni ndugu kwann mnataka kuwafuta. Haya walienda Ulaya Adolf Hitler aliwaua Ujerumani, sasa wamekuja kwenu ndugu zenu waarabu muaanza kubagua kisa dini.Dunia nzima iko mbioni kupinga Ubaguzi huu
Mkuu unaweza kuchangia zaidi kutuelimisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom