Tambaza tulipokuwa wadogo kutoka Muhimbili tulikuwa tunakwenda kumsikiliza Justin Kalikawe alikuwa na gita lake anafanya mazoezi kuimba nyimbo zake za reggae. Alikuwa anasoma hapo, halafu nyumbani kwao ukivuka tu barabara ya Umoja wa Mataifa.
Sasa tukienda kulikuwa na mbabe anaitwa Shetani, hapendi madogo waje maskani. Justin akawa anatutetea anasema hata Yesu alisema waacheni watoto waje kwangu, hawa rafiki zangu bwana msiwatishe.
Basi akawa anatuhimiza tujifunze kupiga instruments ya muziki au hata kwenda kujifunza kusoma notes Korean Cultural Center.
Later on, I went to share a stage with Justin Kalikawe na Jah Kimbute, Justin akafurahia sana performance yangu. Nikamkumbusha enzi za Shetani kutufukuza maskani.
Kabla ya Justin alipita hapo Tambaza Marijani Rajab Jabali la Muziki, lakini siku hizo ilikuwa kabla ya enzi zetu.