Wakuu,
Naomba kuwafahamisha kuwa siku si nyingi tutafanya maboresho kidogo kwenye mwonekano na matumizi ya JF.
Lengo ni kuzingatia mahitaji ya wadau (ambayo yamekuwa yakiombwa), kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuimarisha zaidi uimara wa platform.
Aidha, maboresho hayo yataenda hadi kwenye kuimarisha miundombinu (infrastructure) ili kuongeza uimara wa kukabiliana na hali yoyote.
Mabadiliko mengine ya aina hii yanaweza kufanyika 2021 au 2022.
Maboresho ya Miundombinu yamepangwa kufanyika usiku wa manane wa kuamkia tarehe 26/03/2019.
Asante kwa ushirikiano mnaoendelea kutupa.