Maboresho ya JF - 2019

Mkuu ombi letu la muda mrefu la kuwa na jukwaa maalum la ushirikina na mambo ya giza mlikumbuke tafadhali

Jr
Mkuu Mshana, hili ombi lako naona lilishafanyiwa kazi zamani sana.

Mambo ya ushirikina na mambo ya giza ni imani, na Jukwaa la imani lipo siku nyingine. Nadhani kitu muhimu ungependekeza thread zote za imani ziende jukwaa husika.

Hata hivyo wahusika watakuwa wamekuelewa vizuri.
 
Nashauri maboresho hayo yaimarishe usalama wetu humu ndani kwa sababu wengi tumetumia email halisia kujiunga humu so maboresho napendekeza yafanyike haraka iwezekanavyo kabla ya 2020 kwa sababu wakati wa kampeni ukianza tunataka tumwage madudu mengi mno humu ndani.

Tz kwa sasa ni hatari kutoa comments zinazopinga au kuelezea madudu ya serikali yetu kwa kuhofia kufanyiwa mbaya.

NB:TUMEZIMIWA LOCAL CHENELS KWA KISINGIZIO CHA KUTUOKOA NA GHARAMA ZILIZOKUWA ZINATOZWA KWENYE VIFURISHI KUMBE KUNA AGENDA ZA KUTUFIRIGISA TUKIWA GIZANI.

TUNATAKA LOCAL CHENELS TUNALIPIA VING'AMUZI TUNAANGALIA MA VIPINDI YA VINGEREZA YASIO NA U LAZIMA KWETU, TUNATAKA TUJUE UELEKEO WA NCHI YETU HUKU TUKIONA MATUKIO YANATOKEA KILA SIKU.
 

Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza na kuupongeza uongozi wa JamiiForums kwa kusikiliza maombi ya wanachama wenu wapendwa.

Natanguliza shukran zangu kwako kiongozi wangu Maxence Melo kwa kulifanyia kazi ombi langu na sasa hivi nimekuwa mmoja kati ya WAKUBWA wanaopatikana humu JF.

Nasubiria muongozo wa kubadilisha rank yangu kuwa aidha bronze, silver, gold au platinum member kwenye ID yangu. Nakushkuru sana mkuu.

Ahsante Sana.
 
Ziko wapi tena hizo?
Naona umemnukuu kimakosa huyo uliyemjibu kuhusu "maadili ya Kitanzania" .

Naamini hiyo nukuu ilikuwa ni kwa ajili yangu!!

Ndio maana nimeweka funga na fungua semi kwenye "maadili ya Kitanzania".

Nashukuru kwa kunielewa ndio maana ukaomba kitabu chenye orodha ya "maadili ya Kitanzania".

Nikutakie asubuhi njema!
 
Hivi tuseme mara ngapi?

1) Tulishawambia - sio lazima kutumia email yenye uhusiano kabisa na jina lako halisi; tukawashauri kutumia emails salama kupitia Protonmail na tukawaelekeza jinsi ya ku-edit profiles na kuweka email mpya (valid)

2) Tumekuwa tukieleza kuwa kila mwanachama analindwa na sera yetu ya faragha, hofu sasa inatoka wapi?
 
Tukiruhusiwa kuedit Jina itapendeza zaidi Mkuu
Leo ujiite Daudi de classic na kesho ujiite “Daudi de Classy” na keshokutwa ujiite “Mtambaa Panya” wiki mbili baadae ujiite “Mrembo wa Kigogo” mwezi mmoja baadae ujiite “Nyongo Mkalia Ini” baada ya miezi 2 ujiita “Mkapa Mpya” miezi 3 baadae ujiite “Cha Upele” etc?

Hapana, kwa JF tunajaribu kudhibiti hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…