Maboresho katika utaratibu wa usajili wa watoto kupitia mpango wa toto afya kadi

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
MABORESHO KATIKA UTARATIBU WA USAJILI WA WATOTO KUPITIA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutangazia Umma kuwa, unafanya maboresho ya utaratibu wa usajili na huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya “TOTO AFYA KADI”. Kwa sasa wazazi au walezi wanashauriwa kuwasajiliwa watoto wao kama wategemezi wao kwenye bima ya afya au kuwasajili kipitia shule wanazosoma. Lengo ni kuongeza wigo wa wanachama katika mfumo wa bima ya afya kuelekea bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanachama katika makundi hayo wanajiunga kama familia au kaya au makundi ya wanafunzi kupitia shule wanazosoma.

Mpango wa Toto Afya Kadi ulianza rasmi mwaka 2016 baada ya kufanyiwa upembuzi nalengo ikiwa ni kuwajumuisha watoto kupitia shule zao. Nia ikiwa kufikia kundi kubwa la watoto walio chini ya miaka 18 ambao kitakwimu ni zaidi ya nusu ya wananchi wote ili kufikia azma ya Serikali ya watu wote kuwa na bima ya afya. (Sensa ya 2022 inaonesha watoto chini ya miaka 18 ni asilimia 31 ya wananchi wote).

Uzoefu wa miaka 7 wa kulihudumia kundi hili la watoto kupitia utaratibu wa TOTO AFYA KADI umewezesha Mfuko kufikia watoto 210,664 walio chini ya miaka 18 na umepelekea Mfuko kujifunza mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuboresha. Kati ya hayo ni pamoja usajili wa mtoto mmoja mmoja ambayo inachelewesha utekelezaji wa dhana ya bima ya afya ambayo inataka watu kujiunga kwa wingi wao. Aidha Mfuko umeendelea kushirikiana na Shule za Sekondari na Msingi ili kusajili wanafunzi na mwitikio unaonesha hii ndio njia sahihi ya kuendelea nayo ili kuhakikisha watoto wengi zaidi wanasajiliwa na kunufaika na bima ya afya.

Maboresho ya utaratibu wa usajili wa hiari kwa kundi hili la watoto walio chini ya miaka 18 ni kama ifuatavyo:-

i. Mzazi/mlezi anashauriwa kuandikisha mtoto kama mtegemezi kupitia bima zao kwa mwajiri au vifurushi vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya pamoja na wazazi wao; Vifurushi hivi vinawezesha mtu yeyote mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 kujiunga yeye mwenyewe au na mwenza wake au na watoto wake wasiozidi wanne wenye umri usiozidi miaka 18 na watanufaika na huduma za matibabu popote nchini kwenye vituo vilivyosajiliwa na NHIF kuhudumia wanachama wake.

ii. Kundi la watoto watakaokosa sifa na vigezo vya kuandikishwa kupitia bima za wazazi kwa mwajiri au vifurushi vya Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya wanaweza kuandikishwa kupitia Vyuo, Shule au vituo rasmi vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu;

iii. Kwa wa watoto chini ya miaka 5 ambao watashindwa kuandikishwa kupita ufafanuzi Na (i), ba (ii) hapo juu watumie fursa ya matibabu bila malipo katika vituo vya umma kama ilivyoainishwa kwenye Sera ya Taifa ya Afya 2007.

iv. Kwa wazazi ambao nafasi za wategemezi kwenye bima zao zimejaa kwa maana ya nne na wana watoto zaidi ambao wanahitaji kuwasajili, watashauriwa kuwasajili kupitia Vyuo, Shule au Vituo rasmi vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu vinavyotambulika kisheria. Aidha, kwa watoto walio chini ya miaka mitano, fursa ya matibabu bila malipo katika vituo vya umma kama ilivyoainishwa kwenye Sera ya Taifa ya Afya 2007 inaweza kutumika.

v. Wanachama wa Toto Afya ambao wapo katika kipindi cha kusubiri miezi mitatu kabla ya kuanza kupata huduma na wale ambao ni wanachama tayari kupitia utaratibu wa Toto Afya Kadi, wataendelea kupata huduma mpaka muda wao uanachama utakapoisha ndipo watashauriwa kujisajili kwa hiari kwenye utaratibu ulioboreshwa.

Faida za usajili wa watoto kupitia Shule zao ni kuwezesha utekelezaji wa dhana ya bima ya afya ambayo inataka kusajili watu kwa wingi wao hivyo utaratibu huu utasaidia kufikia kundi kubwa la watoto nchini. Aidha utaratibu huu utasaidia kuwapa unafuu wazazi kugharamia matibabu ya watoto wao na kuwa na uhakika wa matibabu.

Utaratibu huu Utasaidia dhana ya bima ya afya kujengeka kwa watoto tangu wakiwa wadogo. Manufaa ya kusajili watoto kupitia familia/kaya ni kuwezesha familia nzima kunufaika na si mtoto tu au baadhi ya watoto tu. Utaratibu huu utawezesha wazazi kupanga mipango ya ugharamiaji nafuu wa afya kupitia bima ya afya na hivyo kuepuka gharama za ghafla zinazosababishwa na magonjwa yanayokuja ghafla. Hii itasaidia familia kuepuka umaskini usio wa lazima.

Utekelezaji wa mpango huu umeanza tarehe 13 Machi, 2023 na Mfuko ulitoa taarifa rasmi kwa umma. Ni ombi letu kwa wanahabari kusaidia kuelimisha umma na kuepusha taharuki kwa sababu maboresho ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za bima na nia ni njema kwa pande zote. Aidha Mfuko katika ofisi zake zote upo tayari kuelimisha na kutoa ufafanuzi kwa wote wanaohitaji kufahamu zaidi . Pia tuna Kituo cha huduma kwa wateja kupitia namba ya bila malipo 199 ambacho kinahudumia masaa 24 kila siku.

 
Nawaza watoto wenye mahitaji maalumu kama vile CP au autism ambao wazazi wao hawana uwezo wa bei juu na watoto hawa huwa huwezi kuwakuta kwenye shule za kawaida kwahiyo hata kuandikishiwa shule ni ngumu!

Mungu awatetee hili kundi jamani kama huna mtoto mwenye special needs hutakaa huelewe hii point!
 
Niwe muwazi tu sijaelewa hata kidogo.

Kama wategemezi wa wazazi wao? How?

Mfano mzazi ni mtumishi wa umma na ana watoto zaid ya idadi inayohitajika kuingizwa kwenye bima ya mzazi huyu anasajikiwaje kama mtegemezi wa mzazi?

Gharama zao zikoje?

Aliyeelewa nitashukuru kwa kunisaidia
 
Hii taarifa imekaa kisiasa na kipropaganda zaidi na haieleweki..

Mfano, Kwa utaratibu wa mwanzo nadhani gharama ilikuwa tsh 50k Kwa mtoto mmoja Kwa mwaka. Baada ya hayo 'maboresho' gharama ya sasa Kwa mwaka ni ngapi?

Kuhusu hiyo hoja ya kuandikisha watoto kupitia shule, kundi kubwa zaidi la watoto wanasoma shule za serikali, yaani za Kata. Je, huo utaratibu upo huko?
 
Back
Top Bottom