Mabomu Zanzibar.

Globu

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
8,571
2,068
Hali si shwari, polisi Unguja waaza kupiga mabomu ya machozi kila kona ya Mji. Habari zaidi kufuata.
 
Hali inaendelea. UAMSHO wafanya maandamano.
 
Wadau kama kawaida yetu tunapashana habari kila zinapotokea, na hii ndo inaifanya JF kua sehemu ya kupata habari.

Hivi sasa askari polisi visiwani hapa wamevamia mhadhara wa Uamsho na kufyatua mabomu mengi ya machozi.

Wafuasi wa Uamsho walikua wamekusanyika tokea mchana na alaasiri ilikua ni wakati wa mhadhara. Lakini ghafla wazee wamevamia.
 
Habari nilizozipata muda huu kutoka kwa jamaa walioko huko, kwamba eneo la Darajani kumetokea vurugu na sasa hivi jeshi la polisi wanatuliza fujo kwa mabomu.
 
Nasikiliza Times fm wanasema watu wa uamsho walikuwa wamejikusanya kwaajili ya kufanya dua ya pamoja kuwaombea marehemu wa ajali ya meli!Lakini hawana kibali na nasikia serikali imekataza mikusanyiko ya aina yeyote ile ndiyo polisi wamevamia kuwasambaratisha!
 
Safi sana uamsho lianzisheni tu mpaka kieleweke'kuungana na li nchi lisilo na mila wala desturi ndio tabu yake hyo'mimi mbara pyua ila pia sipendi limuungano hili naomba kila siku life tu'
 
Polisi wapiga mabomu na risasi kutawanya waislamu waliokuwa mskn wa mbuyuni wakifanya muhadhara.
Ilikuwa zamu ya amir farid kuzungumza bada kumaliza kuzungumza kwa sh suleiman haji.mara wakatokea polisi nakuanza kurusha mabomu bila sababu.bila yakuzingatia taifa kama limo kwnye msiba kwa kupoteza jama zao.

CHANZO; Makame

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom