Huenda wameamka baada ya kugundua kuwa serikali, kwa uzembe na ufisi wake, inawaua bila sababu tokana na kuruhusu vyombo visivyofaa kusafirisha abiria. Ndani ya mwaka mmoja meli mbili zimezama na mamia ya watu wasio na hatia wamepoteza maisha yao. Kama si hilo basi huenda wanaaanzisha changamoto la mageuzi ya kweli baada ya kuona nchi nyingine zikifanikiwa. Tuwaunge mkono maana ni kwa ajili ya ukombozi wetu bara na visiwani. Kama sababu ni kuchukia au kutotaka muungano, bado wana haki kwanini kulazimisha ndoa isiyo na faida?