Mabomu Yamerindima Mbarali

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,


Ni mabomu ya kutoa machozi, jana na leo.

Tafsiri yangu; hali bado si shwari Mbarali. Hata mchana huu nimeongea na walio Mbarali, wameniambia, kuwa jana FFU waliingia Ubaruku, wamerusha mabomu ya kutoa machozi. Wamewapiga na kuwajeruhi raia na hata kufanya uharibifu wa mali pamoja na uporaji pia, ingawa hali kwa alasiri ya leo ni shwari na watu wanaendelea na shughuli zao.

Kiini cha mgogoro wa raia na dola kule Mbarali kinabaki kuwa ARDHI na mgawanyo wa RASILIMALI za wananchi kupitia yaliyokuwa mashamba ya wananchi ya Mbarali. Kuyauza mashamba hayo kwa wawekezaji ambako hakukufuata matakwa ya wananchi kutabaki kuwa kero kubwa mpaka hapo litakapopatikana jawabu kubalika na walio wengi, wananchi.

Na hatari ya mgogoro wa Mbarali ni kuenea kwa chuki baina ya wenyeji wa asili na ndugu zao Waburushi. Naiona pia, hatari ya mgawanyiko na hata kupelekea mapambano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wakazi wa miji ya Rujewa na Ubaruku kutokana na kujitokeza kwa tofauti za kimisimamo katika mgogoro huu.

Hilo la mwisho likitokea, basi, litakuwa na madhara makubwa sana. Tuna kila sababu na uwezo wa kuepusha machafuko makubwa Mbarali kama kweli tuna dhamira za dhati za kusimamia haki na kutanguliza maslahi ya walio wengi.

Serikali ianze kwanza na kuwawajibisha wale wote waliotufikisha hapa.

Maggid,
Iringa.
mjengwa
 
Watasema ni CDM tena au...ngoja tusikilizie hadi kieleweke mwaka huuu...Hatudanganyiiiiiiiiiiiiiiki na wawekezaji wanaowachumia mafisadi.
 
Ifikike mahali serikali iwe ni chombo cha kusuluhisha migogoro ndani ya jamii badala ya kuwa chanzo cha migogoro kwa kuwalinda watu wachache kwa kutumia nguvu ya dola. Ni hatari sana ndani ya taifa endapo raia watajenga uhasama na jeshi la polisi au viongozi wa serikali. Migogoro ya aridhi imeshaleta madhara hapa TZ mfano Kilosa lakini sijui serikali imejifunza nini kwenye hii migogoro labda kwa sababu wanaokufa sio ndugu zao kwani ndugu zao wengi wapo mijini na wanamaisha mazuri. Uwekezaji unaoleta migogoro ndani ya jamii husika mara nyingi haina manufaa, naionya serikali ya mafisadi ya CCM itatue huu mgogoro kabla ya kuleta madhara kwa raia.
 
kwanini serikali inashindwa kutatua migogoro kwa muda mrefuuuuuuuuuu?
 


Serikali ianze kwanza na kuwawajibisha wale wote waliotufikisha hapa.


serikali yenyewe inaongozwa na watu wanaotakiwa kuwajibika;

unadhani anayetakiwa kuwajibika anaweza kumuwajibisha anayetakiwa kuwajibika?
 
Watasema ni CDM?.Lakini ukweli ni kwamba mburushi(mwekezaji)ni katili sana.Wananchi wame vumilia sana,hivyo wameona waioneshe serikali njia.
 
mbunge ni mr.Kilufu CCM
Kama anatoka chama tawala ni rahisi sana kwake kuutatua mgogoro huu,hawa Wabunge wa CCM waache kuiogopa Serikali yao kwa kuwaeleza ukweli viongozi,wanapofungwa midomo Bungeni basi wasifungwe mdomo na majmboni mwao.Wana uwezo mkubwa wa kuieleza Serikali ukweli na wakasikilizwa kwa haraka kuliko kule wanakotoka Wapinzani.Sasa kwa nini huyu Mr.Kilufi asitumie hii opportunity kabla wananchi hawaja mgeiuka 2015?
 
Tatizo la mbalali limefukuta siku nyingi wananchni wameteswa pale siku nyingi sana, kuna tatizo kama hilo Mgororo kiwanda cha Kalatasi MUFINDI Wafanyakazi walikuwa pale pia wanataabika sasa takribani miaka 15 sasa sijui Mungu ndio anajua tuendako ila CCM inanuka zaidi ya Kinyesi, wakuu wa Wilaya ni wanakula na Vingozi wetu wamejazwa ndani ya Mifuko ya Wahindi.
 
kwanini serikali inashindwa kutatua migogoro kwa muda mrefuuuuuuuuuu?

mtu dhaifu huwa hawezi kusimama imara hata kwenye jambo lililo saizi ya udhaifu wake kwa kuwa hajiamaini,
ni sawa na mpumbavu kwenye upumbavu wake kamwe hutaona hata chembe za hekima itokayo
kinywani mwake, sasa ni wazi kuwa serikali yetu ni ya kihuni ikiongozwa na kundi la wahuni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom